Kama Yanga itafungwa Champions League kichaka cha kufisha nyuso zao wanacho tayari

aaah ni kama umenpata vibaya jombaa! Uto mwaka jana kipindi Simba inapasua anga champions league ndo zilikuwa sababu zao kwamba corona ndo inawebaba sasa tunataka na wao iwabebe kama ni vyepesi hivo
Msimu uliopita tulisema Tanzania hatuna corona, hivyo ligi yetu haikusimama. Hii iliwafanya Simba wawe fiti uwanjani kuliko wale waliokuwa wamesimamisha league zao. Kule Nigeria walichukuwa timu iliyokuwa inaongoza ligi, plateau
 
Kweli kweli sema nini nawe ni wamitaa ya Jangwani sio? Kama ndo mitaa yako basi leo kazi ipo kwenu make msipowafunga jamaa zaidi ya goli moja wale jamaa kwao hawafai ni waswahili balaa huu uswahili wetu kwao cha mtoto. Nakumbuka simba tushawahi chezea tatu mtungi na Enyimba enzi za kina Clement Kahabuka ila wajomba walichinja kuku mubashara uwanjani bila kujali wala nini.
 
Mechi ya kirafiki mcheze na friends rangers halafu muende makundi? itakuwa ajabu la dunia.
 
Haitakuwa kazi ngumu kwa kocha, viongozi, wachezaji na mashabiki wa Yanga kujitetea kama ikitokea bahati mbaya wakafungwa na kutolewa kwenye mashindano ya kimataifa msimu huu. Sababu zao zitakuwa hivi:

1. Wachezaji wao 3 muhimu wamezuiwa kucheza.
2. Timu haikuwa na preseason nzuri
3. Wachezaji wengi ni wapya hawazoeana

Hivyo hakuna wasiwasi kabisa wanangu kichaka kipo kachezeji mpira bila hofu wala kitete mkifungwa sawa na mkishinda sawa.

Tuendelee kulijenga timu.
Asante studio
 
Yanga hawana kabisa maandalizi na sijui kwa nini hawafanyi maandalizi wakati wanajua wazi kwamba wamo kwenye mashindano magumu kama haya.

Sasa sijui watatoa kisingizio gani baada ya kupoteza mechi ya leo dhidi ya wanigeria ni aibu sana kucheza na timu kama Pan African wakati unaenda kupambana na timu kama Rivers United ili akuongezee nini.
 
KAMA WATAPOTEZA LEO TUTEGEMEE
KUSIKIA KAULI HIZI.
Timu haina muunganiko wa kutosha
wachezaji wapewe mda na mazoezi zaidi
Nabii alichelewesha kufanya sub
Huyu kipa bora ya metacha
Tatizo ITC imewazuia wachezaji wetu
Marefa hawana elimu ya mpira,
Ile ilikuwa offside kabisa
TFF nao inabid walaumiwe
tukienda kwao kufa na kupona (manara)
kocha atamtoaje feitoto wakat alikuwa anaupiga mwingi!

Confirmed
 
Kabla ya ligi yetu kuanza, yanga itakuwa imeshatolewa kwenye mashindano ya kimataifa...

Uto hawabebeki
Screenshot_20210912-202227_1.jpg
 
Lia lia fc,yani mlishaanza kulia lia kabla hata ya mechi. Huko TFF na Simba hamuwezi kuwabebesha Utopolo wenu
 
Msimu uliopita tulisema Tanzania hatuna corona, hivyo ligi yetu haikusimama. Hii iliwafanya Simba wawe fiti uwanjani kuliko wale waliokuwa wamesimamisha league zao. Kule Nigeria walichukuwa timu iliyokuwa inaongoza ligi, plateau
Muongo ligi zote duniani zilisimama
 
Yanga hawana kabisa maandalizi na sijui kwa nini hawafanyi maandalizi wakati wanajua wazi kwamba wamo kwenye mashindano magumu kama haya.

Sasa sijui watatoa kisingizio gani baada ya kupoteza mechi ya leo dhidi ya wanigeria ni aibu sana kucheza na timu kama Pan African wakati unaenda kupambana na timu kama Rivers United ili akuongezee nini.
Mechi ya marudiano Yanga watakwwnda kupindua meza, niamini mm
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom