Kama Yanga haikualikwa basi ni kweli TFF ina chuki/mgogoro dhidi ya Yanga

Mti Dawa

Member
Aug 10, 2022
6
20
Miongoni mwa habari ambazo zimeshtua baadhi ya wadau wa soka nchini ni habari inayohusiana na kutoalikwa kwa klabu ya Yanga katika Mkutano Mkuu wa Kawaida wa 44 wa CAF uliofanyika jijini Arusha na kufikia kilele tarehe 10 Julai, 2022.

Binafsi nimestaajabishwa si tu kwa kutoalikwa kwa klabu ya Yanga bali pia baadhi ya wadau wengine muhimu katika soka la Tanzania hasa tukizingatia kuwa Mkutano huu wa Mwaka umefanyika katika ardhi ya Tanzania.

Kwa nini nastaajabu? Ninaomba kuelezea shaka yangu kwa mujibu wa namna utaratibu wa uandaaji wa mikutano ya Kimataifa (Multilateral Conference) unavyofanyika.

Kimsingi uandaaji wa mikutano ya kimataifa kama huu wa CAF huratibiwa na pande mbili ikiwa mkutano kama huo unafanyika nje ya makao makuu ya taasisi husika.

Utaratibu upo hivi, chama cha soka/nchi mwanachama inayotaka kuomba kuandaa Mkutano Mkuu wa Mwaka itaiandikia taasisi husika (kwa muktadha huu ni CAF) kwamba inaomba kuandaa Mkutano Mkuu wa Kawaida wa Mwaka (Ordinary General Assembly).

Maombi rasmi yataandikwa kwa Katibu Mkuu wa taasisi kwa maandishi si chini ya miezi sita kabla ya mkutano kuanza.

Kwa mantiki hiyo TFF iliandika kuomba kuandaa Mkutano huu Mkuu wa 44 wa Kawaida wa CAF miezi sita iliyopita (labda Januari, 2022).

Kuthibitisha hilo, Rais wa TFF Warrace Karia aliweka wazi alipohojiwa na waandishi wa habari na hapa ninamnukuu;

"Mimi niliomba mkutano Serikali ikanikubalia..." Mwisho wa kunukuu.

Hivyo baada ya TFF kukubaliwa na Serikali na pia kukubaliwa na CAF taratibu za awali kuandaa mkutano (pre-meeting) zilianza.

Hapo nchi husika au chama cha soka cha nchi husika (kwa muktadha huu TFF) huandaa tarehe na eneo la kufanyika Mkutano kwa mashauriano na mamlaka husika.

Taasisi husika huandaa ajenda ya Mkutano na mlolongo (schedule) ikiwemo kanuni za mwenendo na kuzituma kwa nchi mwanachama au chama cha soka mwanachama.

Baada ya hapo kutakuwa na uratibu wa Mkutano husika.

Kikanuni, uratibu (Coordination) wa Mikutano Mikuu ya Taasisi ya Kimataifa (kama CAF) ambayo hufanyika nje ya Makao Makuu ya Taasisi hufanyika kwa usimamizi wa pande mbili yaani Nchi inayoandaa (kwa muktadha huu TFF) na Taasisi ya Kimataifa (CAF).

Kamati ya uratibu ya nchi husika iliyoandaliwa kusimamia mkutano itahusika kwa huduma zote na vifaa vyote vilivyoahidiwa na nchi inayoandaa katika barua ya maombi ya kuandaa iliyotumwa makao makuu ya taasisi na kukubaliwa na taasisi husika (CAF).

Huduma hizo zitahusisha utawala, usalama, malazi, vifaa mbalimbali, lojistiksi, usafiri n.k (Rejea OAS, 2017: 15).

Hivyo basi kwa mujibu wa kanuni za uandaaji wa Mikutano ya Kimataifa nchi mwanachama (kwa muktadha huu ni chama cha soka mwanachama TFF) hushirikiana na Sekretarieti ya Taasis ya Kimataifa (kwa muktadha huu ni CAF) katika uandaaji na usimamizi wa mkutano mzima kuanzia mwanzo mpaka unapofikia tamati.

Kwa mfano ukisoma muongozo wa mikutano ya OAS inaeleza hivi, 'The General Secretary will present an organization outline and it is hoped that the host country will appoint counterparts responsible for various activities.' (OAS, 2017: 16).

Hivyo basi mkutano wowote wa Kimataifa hauandaliwi na upande mmoja peke yake pale ambapo mkutano huo unafanyika nje ya makao makuu yake. Kwa mantiki hiyo TFF wameratibu mkutano huu kwa kushirikiana na CAF.

Miongoni mwa mambo muhimu yanayozingatiwa katika mikutano kama hii ni wageni wanaoalikwa.

Tukitazama mkutano wa mwaka wa 44 wa CAF tunaona kuwa mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa.

Kitendo cha kualikwa kwa Waziri Mkuu maana yake Mkutano huu ulikuwa na usalama wa hali ya juu.

Kwa mantiki hiyo hakuna mtu yeyote au taasisi yoyote ambayo ingeweza kuomba kushiriki Mkutano huu wa CAF pasina kualikwa na TFF au CAF.

Kwa mujibu wa kanuni za uandaaji wa mikutano ya Kimataifa CAF walikuwa na wajibu wa kualika viongozi wa Kimataifa huku TFF wakialika wadau mbalimbali wa Tanzania kwa kuzingatia muongozo wa uratibu wa pamoja.

Hivyo kitendo cha Yanga kutoalikwa kinatoa ishara kuwa TFF ama kwa bahati mbaya ama kwa makusudi haikuialika klabu ya Yanga jambo ambalo ni la kustaajabisha. Kwa nini ni la kustaajabisha?

Rejea maneno ya Rais wa CAF Patrice Motsepe pindi alipohojiwa na waandishi wa habari na kuambiwa 'Welcome to Tanzania' (Karibu Tanzania) hakupenda kuambiwa hivyo badala yake akawataka waseme 'Welcome home' na kuandelea kuwaambia:

"Tanzania is my home, Tanzania is his home (akimshika bega Gianni Infantino Rais wa FIFA), Tanzania is home of alla of us! Very special country! Very special history"

Rais wa CAF Patrice Motsepe anawakumbusha watanzania na dunia kuwa Tanzania si nchi ya ugenini kwake bali ni sawa na yupo nyumbani kwao Afrika Kusini kwa nini Motsepe anaamini hivi?

Motsepe aliendelea kusema:

"I'm from South Africa and the relationship between the people of Tanzania and the people of South Africa, their contribution towards our freedom...so we have got a deep deep emotional past."

Motsepe alijaribu kuwakumbusha watanzania jinsi Afrika Kusini inavyoiheshimu Tanzania na ahadi aliyoacha Mzee Nelson Mandela kuwa siku zote za maisha yao waikumbuke Tanzania na wawakumbuke watanzania.

Miongoni mwa mambo ya muhimu katika historia hii adhimu aliyotukumbushia Rais Motsepe (Rais wa CAF) ambayo labda viongozi wa TFF hawaifahamu au labda wanaifahamu lakini wameamua tu kudharau kwa utashi wao ni ushiriki wa Klabu ya Yanga katika harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika ikiwemo Ukombozi wa Afrika Kusini dhidi ya Walowezi wachache.

Inawezekana wachache kati ya watanzania wengi wanaotambua kuwa wakati wa harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika jengo la klabu ya Yanga lilitumika kama eneo la vikao vya siri baina ya Mwalimu Nyerere na wapigania Uhuru wa Tanganyika huku nje ya jengo hilo kundi la Taarabu la Egyptian Musical Club likitumbuiza ili kuwapumbaza wakoloni wakati ndani vikao vikiendelea (Rejea kitabu cha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Chimbuko, Misingi na Maendeleo (2022) ukurasa wa 48 mpaka 49.

Inawezekana wengi ndani ya TFF hawafahamu kuwa Yanga ndiyo klabu iliyokataa kutumiwa na vibaraka wa wakoloni ili kuzorotesha harakati za Uhuru wa Tanganyika tofauti na watani wao ambao walikubali kutumika.

Na inawezekana kabisa kuwa wengi ndani ya TFF hawafahamu kabisa kuwa Klabu ya Yanga imetambuliwa na Umoja wa Afrika (African Union) kama alama ya Urithi wa Ukombozi Afrika katika Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ijulikanayo kama "The 'Roads to Independence in Africa: The African Liberation Heritage Programme''.

Hivyo Motsepe anatambua vema umuhimu wa Tanzania katika Ukombozi wa Afrika na hivyo uwepo wa Yanga katika Mkutano huo wa CAF ulikuwa na umuhimu wa kipekee kutokana na historia ya Yanga katika harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika.

Lakini labda kama hayo yote yangekuwa hayana maana, basi labda Yanga ingealikwa kama klabu iliyobeba kombe la ligi kuu mara nyingi kuliko klabu yoyote nchini au labda ingealikwa kama klabu bingwa ya ligi kuu ya Tanzania msimu uliopita huku ikiwa imefanikiwa kunyakua makombe yote yaliyogombewa msimu wa 2021/2021.

Vinginevyo, nina shaka kama Yanga haikualikwa katika Mkutano huo wa CAF ni wazi kuwa kuna chuki/mgogoro wa TFF dhidi ya Klabu ya Yanga hasa tukizingatia utaratibu wa uandaaji wa mikutano kama hiyo na nani mwenye mamlaka ya kualika washiriki wa mkutano.

Rejea OAS (2017) Operational Handbook for the Organization of Meetings and Conferences away from Headquarters.
 
Umemaliza kila kitu,,ambae atokuelewa atakuwa na shida ndani ya ubongo wake,,Na mimi nawasihi yanga wafocus na mipango yao ndani na nje ya uwanja waachane na mambo ya karia na genge lake, kwasababu anajivua nguo yeye mwenyewe,,Yanga ni kubwa aiwezi na wala aijawai kunajisiwa na mtu yeyote na mtu uyo akabaki salama, karia na genge lake kwasasa watajiona wako kwenye kilele cha utukufu lakini awe na akiba ya badae, vita aliyoianzisha dhidi ya yanga aitokaa imuache salama na atoweza kuishinda zaidi ya kuishia pabaya
 
Na nyie mnapenda kulalamika Sana sasa kama hawajatambua uwepo wenu kwa nini mlazimishe uwepo wenu.kwan kule wanagawa hela kwamba mmezikosa acheni uswahili na ushamba usio na maana
 
Acheni lawama kama watoto wa kambo. Shukuruni tu kwamba Simba imeiweka Tanzania kwenye ramani ya soka mpaka mikutano mikubwa kama hiyo inafanyika nchini.

Lawama hazitawasaidia kitu. Pambaneni mpate recognition uwanjani sio kulia lia mitandaoni mkiingia uwanjani game ya kwanza tu preliminary round mmeshatupwa nje.
 
Mnapenda kulalama kama watoto wa kambo.yani nyie mmeshaona kana kwamba simba na yanga ni kurwa na doto kwamba simba akipata iki na yanga lazima apate .mwacheni uswahili na ushamba wenu caf hakuna mambo kama hayo
 
Umemaliza kila kitu,,ambae atokuelewa atakuwa na shida ndani ya ubongo wake,,Na mimi nawasihi yanga wafocus na mipango yao ndani na nje ya uwanja waachane na mambo ya karia na genge lake, kwasababu anajivua nguo yeye mwenyewe,,Yanga ni kubwa aiwezi na wala aijawai kunajisiwa na mtu yeyote na mtu uyo akabaki salama, karia na genge lake kwasasa watajiona wako kwenye kilele cha utukufu lakini awe na akiba ya badae, vita aliyoianzisha dhidi ya yanga aitokaa imuache salama na atoweza kuishinda zaidi ya kuishia pabaya
".... ambae atakuelewa atakuwa na shida..."
 
Upuuzi mtupu, Super league na Harakati za Ukombozi wa Africa zinahusiana nini? Umeambiwa ile ni Pan Africanism conference?

Hebu acheni ujinga watanzania, Team haijawah kushinda hata friendly match ya Kimataifa alaf leo hii ialikwe kwa ukubwa upi? Viongozi wake wahuni kila siku kuleta fujo na kukiuka maagizo ya TFF unadhan hata huruma zitatoka wapi?

Hebu weka mpira wacha maneno
 
Yanga ya MANARA
Upuuzi mtupu, Super league na Harakati za Ukombozi wa Africa zinahusiana nini? Umeambiwa ile ni Pan Africanism conference?

Hebu acheni ujinga watanzania, Team haijawah kushinda hata friendly match ya Kimataifa alaf leo hii ialikwe kwa ukubwa upi? Viongozi wake wahuni kila siku kuleta fujo na kukiuka maagizo ya TFF unadhan hata huruma zitatoka wapi?

Hebu weka mpira wacha maneno
 
Miongoni mwa habari ambazo zimeshtua baadhi ya wadau wa soka nchini ni habari inayohusiana na kutoalikwa kwa klabu ya Yanga katika Mkutano Mkuu wa Kawaida wa 44 wa CAF uliofanyika jijini Arusha na kufikia kilele tarehe 10 Julai, 2022.

Binafsi nimestaajabishwa si tu kwa kutoalikwa kwa klabu ya Yanga bali pia baadhi ya wadau wengine muhimu katika soka la Tanzania hasa tukizingatia kuwa Mkutano huu wa Mwaka umefanyika katika ardhi ya Tanzania.

Kwa nini nastaajabu? Ninaomba kuelezea shaka yangu kwa mujibu wa namna utaratibu wa uandaaji wa mikutano ya Kimataifa (Multilateral Conference) unavyofanyika.

Kimsingi uandaaji wa mikutano ya kimataifa kama huu wa CAF huratibiwa na pande mbili ikiwa mkutano kama huo unafanyika nje ya makao makuu ya taasisi husika.

Utaratibu upo hivi, chama cha soka/nchi mwanachama inayotaka kuomba kuandaa Mkutano Mkuu wa Mwaka itaiandikia taasisi husika (kwa muktadha huu ni CAF) kwamba inaomba kuandaa Mkutano Mkuu wa Kawaida wa Mwaka (Ordinary General Assembly).

Maombi rasmi yataandikwa kwa Katibu Mkuu wa taasisi kwa maandishi si chini ya miezi sita kabla ya mkutano kuanza.

Kwa mantiki hiyo TFF iliandika kuomba kuandaa Mkutano huu Mkuu wa 44 wa Kawaida wa CAF miezi sita iliyopita (labda Januari, 2022).

Kuthibitisha hilo, Rais wa TFF Warrace Karia aliweka wazi alipohojiwa na waandishi wa habari na hapa ninamnukuu;

"Mimi niliomba mkutano Serikali ikanikubalia..." Mwisho wa kunukuu.

Hivyo baada ya TFF kukubaliwa na Serikali na pia kukubaliwa na CAF taratibu za awali kuandaa mkutano (pre-meeting) zilianza.

Hapo nchi husika au chama cha soka cha nchi husika (kwa muktadha huu TFF) huandaa tarehe na eneo la kufanyika Mkutano kwa mashauriano na mamlaka husika.

Taasisi husika huandaa ajenda ya Mkutano na mlolongo (schedule) ikiwemo kanuni za mwenendo na kuzituma kwa nchi mwanachama au chama cha soka mwanachama.

Baada ya hapo kutakuwa na uratibu wa Mkutano husika.

Kikanuni, uratibu (Coordination) wa Mikutano Mikuu ya Taasisi ya Kimataifa (kama CAF) ambayo hufanyika nje ya Makao Makuu ya Taasisi hufanyika kwa usimamizi wa pande mbili yaani Nchi inayoandaa (kwa muktadha huu TFF) na Taasisi ya Kimataifa (CAF).

Kamati ya uratibu ya nchi husika iliyoandaliwa kusimamia mkutano itahusika kwa huduma zote na vifaa vyote vilivyoahidiwa na nchi inayoandaa katika barua ya maombi ya kuandaa iliyotumwa makao makuu ya taasisi na kukubaliwa na taasisi husika (CAF).

Huduma hizo zitahusisha utawala, usalama, malazi, vifaa mbalimbali, lojistiksi, usafiri n.k (Rejea OAS, 2017: 15).

Hivyo basi kwa mujibu wa kanuni za uandaaji wa Mikutano ya Kimataifa nchi mwanachama (kwa muktadha huu ni chama cha soka mwanachama TFF) hushirikiana na Sekretarieti ya Taasis ya Kimataifa (kwa muktadha huu ni CAF) katika uandaaji na usimamizi wa mkutano mzima kuanzia mwanzo mpaka unapofikia tamati.

Kwa mfano ukisoma muongozo wa mikutano ya OAS inaeleza hivi, 'The General Secretary will present an organization outline and it is hoped that the host country will appoint counterparts responsible for various activities.' (OAS, 2017: 16).

Hivyo basi mkutano wowote wa Kimataifa hauandaliwi na upande mmoja peke yake pale ambapo mkutano huo unafanyika nje ya makao makuu yake. Kwa mantiki hiyo TFF wameratibu mkutano huu kwa kushirikiana na CAF.

Miongoni mwa mambo muhimu yanayozingatiwa katika mikutano kama hii ni wageni wanaoalikwa.

Tukitazama mkutano wa mwaka wa 44 wa CAF tunaona kuwa mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa.

Kitendo cha kualikwa kwa Waziri Mkuu maana yake Mkutano huu ulikuwa na usalama wa hali ya juu.

Kwa mantiki hiyo hakuna mtu yeyote au taasisi yoyote ambayo ingeweza kuomba kushiriki Mkutano huu wa CAF pasina kualikwa na TFF au CAF.

Kwa mujibu wa kanuni za uandaaji wa mikutano ya Kimataifa CAF walikuwa na wajibu wa kualika viongozi wa Kimataifa huku TFF wakialika wadau mbalimbali wa Tanzania kwa kuzingatia muongozo wa uratibu wa pamoja.

Hivyo kitendo cha Yanga kutoalikwa kinatoa ishara kuwa TFF ama kwa bahati mbaya ama kwa makusudi haikuialika klabu ya Yanga jambo ambalo ni la kustaajabisha. Kwa nini ni la kustaajabisha?

Rejea maneno ya Rais wa CAF Patrice Motsepe pindi alipohojiwa na waandishi wa habari na kuambiwa 'Welcome to Tanzania' (Karibu Tanzania) hakupenda kuambiwa hivyo badala yake akawataka waseme 'Welcome home' na kuandelea kuwaambia:

"Tanzania is my home, Tanzania is his home (akimshika bega Gianni Infantino Rais wa FIFA), Tanzania is home of alla of us! Very special country! Very special history"

Rais wa CAF Patrice Motsepe anawakumbusha watanzania na dunia kuwa Tanzania si nchi ya ugenini kwake bali ni sawa na yupo nyumbani kwao Afrika Kusini kwa nini Motsepe anaamini hivi?

Motsepe aliendelea kusema:

"I'm from South Africa and the relationship between the people of Tanzania and the people of South Africa, their contribution towards our freedom...so we have got a deep deep emotional past."

Motsepe alijaribu kuwakumbusha watanzania jinsi Afrika Kusini inavyoiheshimu Tanzania na ahadi aliyoacha Mzee Nelson Mandela kuwa siku zote za maisha yao waikumbuke Tanzania na wawakumbuke watanzania.

Miongoni mwa mambo ya muhimu katika historia hii adhimu aliyotukumbushia Rais Motsepe (Rais wa CAF) ambayo labda viongozi wa TFF hawaifahamu au labda wanaifahamu lakini wameamua tu kudharau kwa utashi wao ni ushiriki wa Klabu ya Yanga katika harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika ikiwemo Ukombozi wa Afrika Kusini dhidi ya Walowezi wachache.

Inawezekana wachache kati ya watanzania wengi wanaotambua kuwa wakati wa harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika jengo la klabu ya Yanga lilitumika kama eneo la vikao vya siri baina ya Mwalimu Nyerere na wapigania Uhuru wa Tanganyika huku nje ya jengo hilo kundi la Taarabu la Egyptian Musical Club likitumbuiza ili kuwapumbaza wakoloni wakati ndani vikao vikiendelea (Rejea kitabu cha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Chimbuko, Misingi na Maendeleo (2022) ukurasa wa 48 mpaka 49.

Inawezekana wengi ndani ya TFF hawafahamu kuwa Yanga ndiyo klabu iliyokataa kutumiwa na vibaraka wa wakoloni ili kuzorotesha harakati za Uhuru wa Tanganyika tofauti na watani wao ambao walikubali kutumika.

Na inawezekana kabisa kuwa wengi ndani ya TFF hawafahamu kabisa kuwa Klabu ya Yanga imetambuliwa na Umoja wa Afrika (African Union) kama alama ya Urithi wa Ukombozi Afrika katika Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ijulikanayo kama "The 'Roads to Independence in Africa: The African Liberation Heritage Programme''.

Hivyo Motsepe anatambua vema umuhimu wa Tanzania katika Ukombozi wa Afrika na hivyo uwepo wa Yanga katika Mkutano huo wa CAF ulikuwa na umuhimu wa kipekee kutokana na historia ya Yanga katika harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika.

Lakini labda kama hayo yote yangekuwa hayana maana, basi labda Yanga ingealikwa kama klabu iliyobeba kombe la ligi kuu mara nyingi kuliko klabu yoyote nchini au labda ingealikwa kama klabu bingwa ya ligi kuu ya Tanzania msimu uliopita huku ikiwa imefanikiwa kunyakua makombe yote yaliyogombewa msimu wa 2021/2021.

Vinginevyo, nina shaka kama Yanga haikualikwa katika Mkutano huo wa CAF ni wazi kuwa kuna chuki/mgogoro wa TFF dhidi ya Klabu ya Yanga hasa tukizingatia utaratibu wa uandaaji wa mikutano kama hiyo na nani mwenye mamlaka ya kualika washiriki wa mkutano.

Rejea OAS (2017) Operational Handbook for the Organization of Meetings and Conferences away from Headquarters.
Tatizo lipo kwa Waziri wa Michezo anamakengeza katika kusimamia soka nchini yeye ni Simba lialia ndio maana hana cha kuwafanya TFF.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom