Kama yametokea Italy, na Greece, sisi tutanusurika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama yametokea Italy, na Greece, sisi tutanusurika?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The Hunter, Nov 8, 2011.

 1. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Wadau nimejikuta nafikiria hatma ya nchi yetu pendwa Tanzania, haswa kutokana na yanayojiri ulimwenguni leo, sijiiti mtabiri lakini nikiwa mmoja ninae amini katika uhalisia, naamini nchi yetu itakwama muda si mrefu kiuchumi, na tutarajie anguko kubwa sana hii ni kutokana na kuzidi kuporomoka kwa uchumi wa dunia, ambao umeshazikumba nchi za ulaya, leo kama Italy, na Greece zimefilisika vipi nchi yetu hii ambayo haijawahi kuwa tajiri! Taasisi za uchumi zinatabiri uwepo wa great depresion katika majira mafupi yajayo.

  Shule hazitaendesheka, vyuo halikadhalika, mahospitali yetu yatakosa uwezo wa kuhudumia wagonjwa na hii nikutokana na kuyumba kwa uchumi.
  Marekani na China zimeshatangaza misimamo yao ya kutokuisadia nchi yoyote ya ulaya itakayofilisika je wataweza kutusaidia sisi wa huku bara la tatu.
  Kweli Serikali hii ya masharobaro isipoamua kutulia na kutafuta solution za kunusuru uchumi, janga litakalotokea itachukua milongo kurekebisha hali hii.
   
 2. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Kaka umesahau?MASIKINI HAFILISIKI
   
 3. P

  Piazza jr Member

  #3
  Nov 8, 2011
  Joined: Oct 30, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Me nahisi ajui, sasa cc 2filisike 2na hela gani wakati madini na vi2 kibao wanachukua wao
   
 4. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  maskini hana Allergy! Kila kitu anameza.allergy ni kwa matajiri eti samaki ngozi inawasha!
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Kuna nchi za Ulaya tutazipa misaada sasa hivi maana watafilisika kuliko sisi tulivyo maskini....just wait and see
   
 6. S

  Sngs Senior Member

  #6
  Nov 8, 2011
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hilo nalo neno!!
   
 7. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Mimi ninaifurahia hali hiyo kwa sababu hizi zifuatazo
  1.Safari za kila kukicha za matanuzi ambazo husingizia kuwa wanaenda kuhemea vibaba/vibakuli zitaisha kwa kuwa sasa hakuna atakayetupa tena faranga na hawataweza kwenda tena majuu kufanya nini ?huwezi kwenda kuomba jamvi msibani
  2.Wale waliokuwa wanatutishia kuwa hawatatupa msaada mpaka tuukubali USHOGA sasa itakuwa imekula kwao kwani hiyo misaada hawaezi kutoa tena kwetu kwani nao hali ni dhufli hali itabidi wakae na USHOGA wao.
  3.Inatufundisha kuwa tutumie rasmali zetu wenyewe bila kutegemea wafadhili,kwetu sisi viongozi wetu wansingekuwa na wagumu kama ngozi ya kiboko wangebadilika kutokea hiyo hali ilivyoikumba Marekani huko nyuma,kwa rasmali tulizonazo sikuona sababu ya wakubwa kuhemea vibaba,na hivyo vibaba vinawanufaisha wao tu na si wananchi
   
Loading...