Kama wewe ni Mwanachuo mpambanaji pita hapa

Heshima kwenu wadau!

Toka serikali itangaze kuwa vyuo vitafunguliwa 01 Juni 2020 mwili wangu umeishiwa nguvu na kujawa na mawazo tele. Wakuu kuna kipindi niliandika uzi wa kuomba msaada hapa hapa. Sema kweli kipindi hicho maisha yalinichapa sana kwani baada ya kufunga chuo na kuongezewa likizo nilichapika sana kwa kukoswa pesa ya boom.

Siyo kwamba nilikuwa sifanyi kazi hapana nilipiga kazi ila akaja mjanja fulani hivi akanitapeli pesa angu kwa kunikopa. Ila namshukuru sana Mungu mawazo yenu yalinifanya nikapiga vibarua maisha yakaenda japo nilikimbia mji.

Naomba kufupisha baada ya kuona likizo imekuwa ndefu niliamua kutafuta mtaji nikawa nafanya ujasiriamali japo mtaji wangu ni mdogo but namshukuru sana Mungu nifanya kwa muda wa mwezi mmoja pekee na nikawa tayari nimeanzisha ufugaji wa Nguruwe.

Nimeanza na nguruwe wadogo 2 na nilikuwa nimejenga banda la kubeba nguruwe 3 kila nguruwe akiwa kwenye position yake. Sema kweli saiv naumia sana kurudi chuoni huku swali kubwa ni Je, hawa mifugo namuachia nani? Na hii shughuli ambazo nilikuwa napiga niziache wakati nimezoea na zinaniingizia kipato ambacho kinaniweka mjini kwa sasa?

Naombeni msaada wenu wakuu, nipo mwaka wa Mwisho ila natamani sana niachane tu chuo make sioni umuhimu kwa sasa kwa sababu ajira zenyewe mpaka utambikiye c bora nikomae tu?
Kiongozi bado semester moja umalize ,,maana take bado 3 months ..umalizee cha msngi tafuta mtu mwaminifu umkabidhi mifugo yako...Kama una mdgo wako au ndgu ...then kamalizie semester iliyobaki baada ya hapo rudi uendelezee ufugaji ..kuliko kuuza Tena ukarudi kuanza mwanzoo...unaweza kata tamaa ..maana mwanzo mgumu..

Kusanya akiba from boom ,uje uongezee mradi wako wa nguruwe ....hutatesekaa kiongozii...tofauti na wanao Rudi kuanza mojaaa
 
Back
Top Bottom