Kama wewe ni Mwana Dar es Salaam, hili linakuhusu

KooZito

JF-Expert Member
Dec 14, 2020
396
1,377
Naomba kuzungumza na wenyeji wa jiji la Dar na viunga vyake hususan wafanya biashara. Ni hivi, ujambazi wa kutumia silaha umerejea kwa kasi sawa na maambukizi ya Corona.

Na ujambazi wa safari hii ni wa pekee. Yaani hata Shilingi 200,000/= inakutoa roho.

Tayari huko Segerea meneja wa Baa ameuawa kwa kupigwa risasi akifunga baa usiku akitakiwa kutoe hela za mauzo na alipozingua akatobolewa kwa risasi.

Huko Tabata mfanyabiashara wa bidhaa za jumla amefuatwa nyumbani kwake mara tu alipofika getini akaoneshwa "mguu wa kuku" akitakiwa kutoa hela na silaha. Hakuwa na silaha akatoa hela. Huko Chanika nako kuna tukio la namna hiyo. Hatujui leo wataenda wapi.

Chanzo: Ni kutoka ndani ya jeshi letu la Polisi kwa sharti la hifadhi ya jina.

My Take: Ni vizuri kila mmoja kuchukua tahadhari kushirikiana na Jeshi letu la Polisi. Ni vizuri Polisi wakaweka namba zao wazi ili mtu aonapo dalili za mtu asiyeeleweka kutoa taarifa ili wanaohisiwa kunyakuliwa kabla hawajafanya uharibifu mkubwa.

Polisi nao watoe elimu ya watu kumtambua mtu anayeweza kuwa ni jambazi ili wawahiwe. Hatuwezi kupangiwa muda wa kufanya kazi na kulala na majambazi. Tuwape Polisi ushirikiano.

Hofu yangu ni, isijekuwa ni "beep" ya yule Kamanda aliyeshushwa cheo na kupelekwa Dodoma kusoma magazeti sasa anakomoa. Nawaza kwa sauti.
 
Wizi ni mwingi sana kuna sehemu waliiba Kunduchi ya mbezi gari vts na wakarudi tena waka fanya uharibifu tuna tatizo inabidi watu wasi wafiche wezi
 
Ni vizuri kuweka CCTV camera maeneo muhimu kama bar na nyumbani kwa wafanya biashara au pesa nyingi
 
Jambazi ni jina yoyote anaweza kuwa jambazi ukiwa unatoa taarifa angalia nani unampa hiyo taarifa usiridhike na vazi lake ikawa ndio wampa taarifa toa taarifa kwa watu sahihi
 
Polisi watafundisha raia kwamba jambazi ana sura flani ngumu hivi alafu ina makovu kama yote.....sidhani kama wanywa gongo tutasalimika
... Rejea bongo movie
 
Jambazi ni jina yoyote anaweza kuwa jambazi ukiwa unatoa taarifa angalia nani unampa hiyo taarifa usiridhike na vazi lake ikawa ndio wampa taarifa toa taarifa kwa watu sahihi
Sio vazi tu anko.. Hadi sura nayo ni changamoto
 
makonda anatakiwa sana kwenye hili jiji.

Huyu Kunenge ni Mwepesi sana yaani hata ukikutane kwenye kumi na nane zake bado atababaika tu.
 
Back
Top Bottom