Kama wewe ni mjasiliamali soma hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama wewe ni mjasiliamali soma hapa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Cotan, Mar 21, 2010.

 1. C

  Cotan Member

  #1
  Mar 21, 2010
  Joined: Feb 11, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Ukosefu wa Uaminifu katika Biashara ndiyo tatizo kubwa sana linalo gharimu sana katika biashara, Biashara nyingi sana zimekufa kutokana tatizo hili.

  Uaminifu unamaana kubwa sana ktk nyanja hii, mfano km wewe ni mmiliki wa Duka, Bar, Mgahawa, Genge, Kiosiki, nk. Basi unaajiri watu au mtu kwa ajiri ya kukusaidia katika biashara yako au unamchukua ndugu yako au rafiki yako unamuweka katika biashara. Mnakaa mnakubarina kiwango cha mshahara au manufaa atakayoyapata kutoka kwenye biashara hiyo.Pia mnakubariana namna ya kuendesha kazi yaani kanuni za kuendesha biashara husika..

  Basi na kuhakikishia usipokuwa macho utaibiwa tu, utafilisika tu, watu siku hizi hawaaminiki.usifikirie kwamba kwa vile ni Mke wako, Dada yako,Mdogo wako, Kaka Yako, Mjomba wako, Rafiki yako, au Mlokole mwenzio basi hawezi kukuibia, ndg hilo unajidanganya tu. Weka uzibiti maalumu wa Biashara yako hakikisha kila siku unafanya mahesabu km huwezi kufanya kila siku basi fanya angalau kwa kila wiki au kila mwezi au kila baada ya miezi mitatu. Usichelewe sana kufanya mahesabu kwani kadiri utakavyo chelewa ndo kadri hasara itakavyokuwa kubwa hatimae biashara itakufa.

  Usifanye biashara kwa mazoea tu, jifunze namna ya kutunza kumbukumbu za biashara yako. Wajasiliamali wengi hawaweki kumbukumbu katika biashara zao hili ni tatizo kubwa sana. Matokeo yake ni kufa kwa biashara au kudumaa kwa biashara, kila mwaka utakuwa unapiga makitaimu uko pale pale tu, au unapanda kidogo tu.

  Unapo weka kumbukumbu za biashara yako inakusaidia wewe kujua namna biashara yako inavyokua au inavyoanguka. Kwa hiyo unakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihihi kwa mda muafaka. Usifanye biashara kwa kuangalia kwa macho tu, bila ya kufanya mahesabu.yaani kuna baadhi ya wafanyabiashara hasa hasa wenye maduka huwa wanaangalia tu jinsi bidhaa ilivyojaa kwenye ngazi za duka au jinsi stoo ilivyojaa basi wanaamini kuwa wanasonga mbele kumbe wapi. Huwezi kujua hasara au faida kabla ya kufanya mahesabu (STOCK TAKING).

  Pia tatizo lingine linalowakabiri wa fanyabiashara ni kuchanganya madeni mfano, wewe unaenda kukopa pesa Bank mathalani unakopa Tsh 4ml na liba ya Tsh 760,000/= jumla umekopa 4, 7600, 000/= lazima pesa hiyo uilipe hiyo sio sadaka, usianze kufanya mambo yaliyoinje na malengo ya mkopo, mfano usiende kulipia karo ya mototo au kununua makochi utafungwa bure.Pia lazima uwe na kikomo cha ukopaji usipende kukopa tu kila mahali mfano, Bank umekopa, kwa John umekopa, kwa Musa umekopa ,kwa IDDI umekopa na kwa Masawe umekopa pia.je utaweza kumeneji madeni yote hayo kwa wakati mmoja?. Matokeo yake ni kukimbia tu.au kufirisiwa utaanza kuishi km digidigi.

  Pia km unaweka bidhaa stoo basi kuwa makini sana kwani wafanyabiashara wengi wanafirisika kutokana na kukosa udhibiti wa mali iliyoko stoo( gharani) hakikisha unakuwa na hesabu kamili ya vitu vilivyoko stoo weka kumbukumbu ya kila kinacho toka na kuingia stoo.usipokuwa makini utafirisika tu, watu wanaibiwa sana kuwa makini.Pia hakikisha vitu vinakaa kwa usalama bila kuharibika .pia usiwe mbali sana na biashara yako, angalau uwepo kila mara kuhakikisha mambo yanaenda sawa.Usiamini watu tu eti watakufanyia kila kitu hakuna biashara ni wewe mwenyewe.

  Usitafute mchawi kwenye Biashara yako elewa kuwa Mchawi ni wewe MWENYEWE wala USITAFUTE MGANGA WA BIASHARA YAKO ELEWA KUWA MGANGA NI WEWE MWENYEWE. Ninasema hivi kwa sababu ya baadhi ya wafanyabiashara kupenda sana mambo ya ushirikina wakiamini kwamba bila ya kwenda kwa mganga mambo hayawezi kwenda veme hii ni imani mbaya sana wengi imewakwamisha wengi wameangamia pia wameangamiza ndugu zao kwa ujinga huu.

  Hakuna mganga anaejua dawa ya biashara hakuna bali kuna mazingaombwe tu, na kulishwa imani mbovu. Km huyo mganga anajua dawa ya utajiri kwa nini yeye awe masikini au kwanini watoto wake wawe masikini.mnadanganyika bure tu, hakuna miujiza katika biashara usidanganyike.Dawa ni kufanya kazi kwa bidii na kuwa Mkalimu kwa wateja na kujitaidi kuweka kumbukumbu za biashara vizuri. Pia kujitaidi kuwa muaminifu ukikopa kumbuka kulipa usipokuwa muaminifu watu hawatakuamini elewa kuwa biashara ni uaminifu.Pia weka malengo ya biashara yako.

  ASANTENI.
   
 2. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  you said it all. Anayekusaidia japo unamlipa anataka ahamishie mtaji kwake. Wtz tumekuwa wezi watupu.
   
 3. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2010
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ni ushauri mzuri kabisa...Ubarikiwe kwa hilo. Mie ngoja nikalipe deni la watu la dola 1,500 mwisho wa mwezi.
   
 4. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ushauri uliotoa ni mzuri kaka yangu na ndivyo wajasiriamali inavyotupasa kufanya.
  ila kama humuamini hadi mkeo ni nani basi utakayemuamini hapa duniani.?
   
 5. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Hilo nalo neno
   
 6. Q

  Qsm JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 400
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  mhh nimekurupuka kuomba msaada wa kuendesha duka la nguo kumbe tiba ipo hapa
   
 7. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  asante kaka
  wengi tunafilsika bila kujua kosa liko wapi.
   
 8. J

  Jafar JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Swala la uaminifu ndio hasa biashara yenyewe. Nakuunga mkono kwa hoja hii kwani mimi yamenikuta siku si nyingi. Ushauri wangu kwa wajasiriamali wenzangu: Usitafute mwanaume kushika fedha zako wakati haupo, tafuta mdada au mmama - wanawake wanaweza kudokoa lakini ni wagumu sana kufanya maamuzi ya kukimbia na fedha kama wanaume.
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
  Nadhani hoja yake ya msingi hapa ni kuwa makini na kila kitu kinachotokea kwenye biashara yako. Take it from me, ukikaa vibaya hata mkeo/mumeo (kama ni mdokozi) anaweza kukuliza tu!
   
 10. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Tumekusikai mkuu na tutayafanyia kazi; ila swala la mke ni gumu zaidi kwa sababu namhesabia kama mdau wa moja kwa moja ; kwa maana hata mahesabu naweza kumwachia akayafanya.
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  thanks mkuu sread yako ina mafunzo
   
 12. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,828
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Kukosekana uaminifu ni tatizo kubwa kwakweli na ndio chanzo cha uhasama kwenye biashara. Asante kwa somo zuri
   
 13. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #13
  Mar 26, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,828
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Hapa uko sahihi kabisa Mkuu, umenena jambo ambalo wengi hawatalipenda. Big Up kwa kutoa ukweli
   
 14. E

  Edo JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Don't fool yourself: Hao unoadhani ni nafuu ndio balaa kabisa. Uliza hata kitengo cha upelelezi polisi wakupe data, utazimia !
   
 15. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...kwenye suala la uaminifu hata wewe mwenyewe ukikosa nidhamu ya biashara utajifilisi tu.

  ...kwenye mipango yako, jiwekee nidhamu ya usimamizi, ufuatiliaji na urekebishaji pale penye mapungufu.
  Hawakuwa wajinga waliosema 'mali bila daftari, hupotea bila habari', ndiyo maana kuna profit and loss account, etc etc...

  ...kumbuka lengo, nia na madhumuni ya kuanzisha hiyo biashara. Kama ilikuwa ni kuganga njaa tu, hasara haitokuwa ajabu kwako.
   
 16. M

  Malila JF-Expert Member

  #16
  Apr 9, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Mkuu salama,
  kumbe upo. kila kona kilio ni uaminifu,uaminifu,uaminifu. nidhamu kwa kila ufanyacho ni muhimu. Neno nidhamu ni pana sana bandugu.
   
 17. babalao

  babalao Forum Spammer

  #17
  Apr 13, 2010
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Asante kwa ushauri Ila la mke na mtoto hawa ni wadau muhimu kwako kwani hata unapotafuta unatafuta kwa ajili yao,usipomwamini mkeo hutamwamini mtu! hawa wadau ni walengwa moja kwa moja. Uzoefu nilio nao ni kwa ndugu hao waogope kama ukoma
   
 18. Edgartz

  Edgartz JF-Expert Member

  #18
  Apr 13, 2010
  Joined: Feb 26, 2010
  Messages: 241
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu tunakushukuru kwa hii post umetufungua macho mkuu mungu akubariki uwe na moyo huo huo!!
   
 19. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #19
  Apr 13, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Post ya Cotan ina mashiko wakuu! Someni na kuielewa.
   
 20. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #20
  Apr 16, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mkuu no comment msg send hapo huo ni mpango mzima
   
Loading...