Kama wewe ni kijana pitia hapa inakuhusu

Moyibi

JF-Expert Member
May 11, 2012
1,054
710
Jipime Maisha yako unayoishi, juhudi zako katika kuleta mabadiliko, Mawazo yako na zaidi watu wako wa karibu, je ni ASSETS au LIABILITIES.

ASSET ni kitu kinachokuingizia wewe kipato au fedha mfukoni na LIABILITYni kile kinachofanya fedha iondoke kwako au mfukoni mwako.

Mfano kama una nyumba umeipangisha watu wanatoa kodi ya mwezi hiyo tayari ni ASSET lakini kama we umepanga na unatoa kodi kwa mtu iyo ni LIABILITY.

Ukinunua gari binafsi la kusafiria lazima uwe unanunua mafuta so iyo ni LIABILITY, but gari la abiria ni ASSET maana watu wanatoa nauli kulipanda gari lako, Ardhi ni ASSET na mengine ya namna kama hiyo, lakini ukinunua vitu vya starehe saa za vito, mikufu ya shingoni, nguo za gharama kubwa kupita kipato chako, nk hayo yote ni LIABILITIES.

Rafiki anayekupa mipango ya kuangalia movie masaa10 kwa siku na anayekupa ratiba za kwenda kutumia pesa kwenye starehe huyo ni LIABILITY muepuke kama ukoma lakini yule anayekuonyesha fursa na namna ya kuwekeza huyo ni ASSET mshikirie usimwache.

Simaanishi kuwa na LIABILITIES nyingi ni makosa HAPANA ila lazima tuangalie ni wakati gani, na hali gani ya maisha umo kwa wakati huo, kama unaanza kujenga miradi, au unaanza maisha, au miaka 5 ya ajira na ukaweka kuwa na LIABILITIES nyingi kuliko ASSETS ujue umepoteza Ila kama ulianza na ASSETS na uko katika wakati mzuri wa kimaisha apo kugeukia LIABILITIES hutakua hujapoteza kitu.

Hapa ni kwamba ASSETS ulizonazo zitakupa wewe LIABILITIES unazozitaka na SIO kinyume yake.

Ukiona we una LIABILITIES nyingi kuliko ASSETS jua Unaelekea kushindwa but kama una ASSETS nyingi kuliko LIABILITIES jua unaelekea kwenye mafanikio.

Kumbuka huwezi kubadilisha jana ila unaweza fanya kitu leo kitakacho badilishe kesho yako, so kama ulikuwa na LIABILITIES nyingi kuliko ASSETS usijilaumu sana ila sasa badilika uanze kuweka juhudi kuwa na ASSETS nyingi na punguza LIABILITIES.
 
"Ukiona we una LIABILITIES nyingi kuliko ASSETS jua Unaelekea kushindwa but kama una ASSETS nyingi kuliko LIABILITIES jua unaelekea kwenye mafanikio" ... hapa umenikosha sana.
 
Vijana ,ukiwa ni pamoja na ww uliendika Hii Post ..nendeni mkasome Kitabu cha Robert T Kiyosaki.

Guide to Investing / What the Rich Invenst In,that the Poor and Middle Class Do Not !
 
Vijana ,ukiwa ni pamoja na ww uliendika Hii Post ..nendeni mkasome Kitabu cha Robert T Kiyosaki.

Guide to Investing / What the Rich Invenst In,that the Poor and Middle Class Do Not !
Asante ntakitafuta hicho kitabu,
 
Mkuu we tafuta hela kisha ukae nazo tu maana hata kulipiia nyumba unayoishi pia unaona liability bila kaagalia faida zinazotokana na kuishi ndani ya nyumba. Lala nje na hela zako halafu uone kitakachotokea
Na si kutumia gari ni hasara wkati mwingine ata kama hupakii abiri lakini pia kuna faida kwa kuwa kunarahisha ufanyaji wa kazi zako na hiyo hukupa faida pia, au ndio nyie wenye dhana kwamba kumiliki gari ni utajiri. Wakati mwingi mtu inabidi uisha maisha ghali zaidi ili uweze kutafuta fursa za kupata fedha
 
Back
Top Bottom