Kama wewe ni dereva gari kubwa au dereva wa gari kubwa za mizigo, soma hii inakuhusu

Redpanther

JF-Expert Member
Feb 23, 2019
1,208
2,000
Asalaam aleikum warahmatullah wabarkatuh kwa Wakristo Tumsifu Yesu kristo.

Ni matumaini yangu kuwa wanajamvi wenzangu mko salama salimin na kwa yeyote aliyekatika kuugua au changamoto za maisha pole yake.

Eee bhana, mie nina pikipiki yangu boxer 50 huwa naitumia kusafiri kutoka nyumbani hadi ofisini ninapofanya kazi. Boxer hii niliinunua mwaka jana mwezi wa Novemba, kiukweli naugurahia sana usafiri wa Boxer. Kwahiyo mie ni commuter.

Nikiwa barabarani, kuna changamoto ambayo naamini waendesha pikipiki wenzangu mtakuwa mmewahi kukumbana nayo. Kuna hawa jamaa wenye gari zao za binafs na wale waendesha Mabasi ya Abiria yatokauo mkoa mmoja hadi mwingine, Hawa jamaa wengi wao hawajali kabisa usalama au Maisha ya Waendesha pikipiki.

Majuzi kati niliamua kutimba Morogoro kwa Boxer yangu nikitokea DSM, aseee inasikitisha sana vile ambavyo madreva hawa wanavyoendesha vifaa hivyo hasa hasa pale kunapokuwa na gari jingine katika uelekeo ule ule huwa ni hatari sana. Haijalishi kuna nini mbele, hawa jamaa huwa wana overtake bila kujali usalama wa watu wenye pikipiki. Nikiwa maeneo ya Mbezi dakika chache baada ya kuingia barabara kuu hawa jamaa asee walikuwa wanaendesha kwa fujo sana na mwingine hadi alifikia hatua ya kunibana kabisa na kusababisha ajari ambapo niliingia mtaroni na kuumia vibaya sana.

Lakini kwa sababu, kilichokuwa kinanipeleka Moro kilikuwa cha muhimu nililazimika kusafiri tu ila Kiufupi maaskari wa Usalama barabarani wanapawa waongeze kuwabana hawa madreva magari hasa hasa magari makubwa maana Ajari zitokeazo nyingi wasababishao ni Madreva.

Basi Naomba sana nyie mlio na Magari Tuheshimuni na tupeni haki yetu ya kutumia barabara kama wasafiri wengine.

JIONI NJEMA WATU WA JF..
#BAKI NYUMBANI #NAWA MIKONO YAKO KILA MARA

#COVID-19 IPO NA INAUA

IMG_2403.JPG


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom