Kama wewe ni binti na una miaka 25 au zaidi na hujui kabisa nani atakuoa na hamna dalili, usichukulie poa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Copy and pasted kama ilivyo.............................

Kama wewe ni binti na una miaka 25 au zaidi na hujui kabisa nani atakuoa na hamna dalili, usichukulie poa. Lazima kutakuwa na shida mahali. usinyamaze kimya hakikisha wewe na Mungu mpaka mmeelewana vizuri.. maana utafiti wangu Mdogo unaonesha wengi mnajichelewesha wenyewe na:-

1. Tutabia tudogo dogo kama kuomba omba hela wanaume. maana kuna wadada wanajua kupiga mizinga yaaani hatari. Atadai umpe hata hela ya kununulia oxygen wakati Mungu katupa bure.

2. Wengine tutabia twa uchafu uchafu. utakuta mwanamke nywele zinanuka hatari au Asubuhi binti ananuka kikwapa...kweli?

3. Wengine mavazi yaan manguo wanayovaa.
Mtu unavaa nguo kama mzee halafu unasema unamsubiri Mungu...my dear kiukweli utamsubiri sana.

4. Wengine wanataka kuolewa na malaika.
Eti wanasema wanaume wote ni waongo, ko wanasubili Mungu amletee mtu sahihi. Labda hawajui kuna wakati tunadhani tunamsubiri Mungu kumbe na yeye Mungu anatusubiri sisi tubadilike

5. Wengine kiburi tu na ujuaji ndo unawachelewesha. Aisee raha ya mwanamke ni kujidai mshamba kidogo. Vingine unapotezea. sio kila kitu unajua na unataka haki yaaani.

6. Wengine wanagawa sana uroda na hawajui kwamba wanaume huwa tunasimulianaga mambo. Na ni ngumu sana mwanaume kuoa mwanamke ambaye anajua amewahi kutembea na MTU ambaye anamjua

Lakini saivi wanaume wamebadilika wengi huwa hawafuatiliagi sana huko nyuma mwanamke wake aliwahi kutembea na nani. ukishamwambia tu kwamba wewe sio bikira basi anaishia hapo. maana wanajua ukitaka kumla bata usimchunguze sana. Ukishajua ni bata basi inatosha kinachofuatia ni Kula.

Ukichunguza sana unaweza kugundua hata rafiki yako wa karibu amepita kwa mwanamke wako halafu unapojisifia sifia mbele yake umeoa yeye anakuchora tu hahahahaha, na mbaya zaidi ujue kwamba yeye anakuchora. Unaweza kwenda kununua nguo kwenye kiwanda cha sigara.

Share
 
Hapo kwenye [HASHTAG]#Oxygen[/HASHTAG] umenigusa. Lakini mi naona wadada now days wamekuwa wajuaji sana tena sana. Sasa we waache wale maisha ya ujana wao then wakifika 30+ wawe single mother, maana ujuaji mwingi sana.

Ulimbukeni unawamaliza wasichana
 
Tatizo mabinti wanachagua sana, kiukweli kila mtu akisema atulie sehem na mtu wala kusingekuwa na malalamiko ya wao kutokuolewa
 
Ukweli ni huu wanawake wengi wamekuwa ni wachaguzi, wanapenda kijana mtanashati, mwenye elimu, mwenye kazi nzuri.

Hivyo vyote si rahisi kuvikuta kwa kijana mmoja.

Unakuta kijana kasoma lakini kipato chake hakieleweki.

Kuna wengine wanataka ndoa kwanza. Hawa ndio watasubili sana. Maisha ni kujitoa mhanga.
 
Back
Top Bottom