Kama wenye VVU/AIDS wanasaidiwa na serikali na Albino je? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama wenye VVU/AIDS wanasaidiwa na serikali na Albino je?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KIDUNDULIMA, Oct 2, 2010.

 1. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Ndugu zangu nimeuliza swali hili kuhusu namna ambavyo ndugu zetu Albino wanavyotendewa katika nchi yetu ya Tanzania. Tunajua wazi kuwa tatizo kubwa walilonalo wenzetu albino ni magonjwa ya ngozi ambayo yanaweza kutatuliwa na kupakaa mafuta maalumu ya ngozi. Na tukijua wazi kuwa wengi wa maalbino kipato chao ni cha chini kabisa hivyo hushindwa kumudu gharama za mafuta hayo. Cha kushangaza serikali imekaa kimya kuhusu tatizo lao wala hakuna agizo la kuhakikisha kuwa albino wanapatiwa mafuta hayo ili kuwaondolea mateso yatokanayo. Kama wenye VVU/AIDs wanasaidiwa na serikali kupunguza makali ya virusi kwanini albino nao wasisaidiwe?Je ni kwa vile hakuna albino ambaye ni waziri katika serikali wa kuweza kuwatetea? Maana mawaziri kibao tunao wenye VVU/AIDs hivyo kwao ni raisi kujipendelea kuliko kuwapendelea albino.

  Tafadhari serikali saidieni albino nao ni watanzania.
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Unatakiwa ujiulize kwanza nani ni decision makers Tanzania. Kwanza angalia ni asilimia ngapi ya members wa cabinent ni HIV positive, na angalia ni asilimia ngapi ya members wa cabinet ni albino, angalia ni asilimia ngapi ya ya HIV positive people have access to centres of decion making, na ni asilimia ngapi ya Albino have that access. Jibu liko wazi. Kisiasa tunasema Albino ni wenzetu ni ndugu zetu, kivitendo tunawaonesha kuwa they are useless human beings, ndio maana tulianza kushughulikia mauaji ya Albino pale international media ilivyoanza kusema. pure and simple.
   
Loading...