Kama Waziri Mwakyembe Katuonyesha Hili Basi Na Mawaziri Wengine Watuonyeshe Mifano Ya Kweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama Waziri Mwakyembe Katuonyesha Hili Basi Na Mawaziri Wengine Watuonyeshe Mifano Ya Kweli

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ndallo, Jun 13, 2012.

 1. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,129
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  1:

  Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe, Mb:
  katuonyesha mfano kua naye anajali na kujumuika na wananchi kwakupanda Train kutoka Dar - kwenda Dodoma bila kusahau kuwawajibisha baadhi ya vigogo kwenye idara yake - Sawa;

  Tunataka na hawa nao waonyeshe kua nao wanajali!
  2: Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb: - Naye avae magwanda ya udaktari aingie hosptalini atuonyeshe naye anajali wagonjwa bila kusahau migomo ya madaktari iko mbioni kurudia tena kama walivyodai sikilizana uyafanyie kazi madai yao.

  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb: - Naye ashike chaki aingie darasani kutonyesha kua anajali kwakufundisha wanafunzi bila kusahau vilio vya walimu nao wako mbioni kugoma fanya hima uwasikilize.

  3:
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Bernard K. Membe, Mb - Huyu jamaa anatakiwa akaimu nafasi hii kutoka kwa Mkulu JK.

  4:
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb - Huyu jamaa anatakiwa aige mifano ya Lyatonga Mrema kwakupambana na uhalifu ndani ya nchi natumaini mnakumbuka muheshimiwa Lyatonga enzi zile.

  5:
  Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza, Mb - Naye huyu tunataka tumuone akiwa amevaa Overroli aingie mashambani kwakutoa mifano kwenye hicho wanachokiita kilimo kwanza bila kusahau vilio vya wakulima, mkulima wa Tanzania hafaidiki na kilimo ni njaa tupu.

  6:
  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fenella E. Mukangara, Mb - Huyu tunataka apambane na michezo kwakiasi kikubwa michezo imeshuka tena saaaana, isitoshe atoe tamko kali kwakupambana na viombo vya habari ambazo ni chafu kama kwenye magazeti ya kina Shigongo kwakuandika umbea Business bila kusahau na viombo vya habari kama zile redio za kina Hando na PJ na zinginezo wafuate maadili na sio kutuletea vipindi vya hovyohovyo kama vile kile kipindi alichorusha hewani dada Dina Marios sijui kunuka vikwapa na mambo mengine.

  7:
  Waziri wa Maliasili na Utalii Ndugu Khamis Kagasheki, Mb - Huyu kashatuonyesha mifano lakini tunataka wale waliohusika na usafirishaji wa zile nembo za taifa bila kusahau wale faru waliouwawa kule Serengeti na uozo mwingine wameshafikishwa kwenye vyombo vya sheria na hukumu isomwe siku moja bila kusahau hukumu itoke siku hiyohiyo.

  8:
  Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb - Nakutaka ufungue viwanda vyote vilivyokufa - General Tyre/Kilitex/Mwatex/Emco nk! kabla awamu ya JK kuisha vijana hawana ajira tembea ujionee mwenyewe!

  9:
  Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa, Mb - Baba cha kwanza ondoa noti hizi tulizonazo kwenye mzunguko kwakua hata kama nimeishiwa na karatasi ya kuchambia kweli noti hizi tulizoletewa baada ya uchaguzi ni kinyaa kwa taifa siwezi kuchambia! Bila kusahau mfumuko wa bei na maisha kuwa juu.

  10:
  Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, Mb - Sasa wewe mkuu ndio funga kazi!!! Naomba kuwasilisha na mnisaidie kwa wengine.

  Aluta Continue!


   
 2. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,223
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  hakuna lolote mawaziri wa KIKWETE unafki tu waonekane wanajaaaali, kwani huyo mwakyembe alikuwa wapi kupanda treni siku zote apande leo, au ndo anajifanya hajui matatizo ya treni zetu ndo ameenda kupata uzoefu??

  aaaah, waache kutuzuga hawa wanasiasa kuonyesha wanajua sana kutujali!!!tumechoka na siasa uchuro hizi!!!
   
 3. m

  mamajack JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  alichfanya ni kizuri,ila watanzania hawahitaji kumuona kapanda trn siku moja,maana haya mambo yanajulikana na yanayoelezwa yote ni kweli,watanzania wanahitaji utekelezaji.
  mkuu katoa namba apigiwe kama watu watatozwa pesa nyingi kwenye madaladala,ila toka siku hiyo huwa haipatikani.
  nakumbuka baba lizi nae alianza na mbwembwe ivoivo mara yupo soko la tanadale kwa kushitukiza,mara mahospitalini,tukaamini atakuwa na msaada kumbe mwizi mkubwa.mwakyembe ninaimani kidogo kwake,naamini atatekeleza kwa vitendo,ukisema waanze,wengine watapita kwenye miji na kuwahadaa watanzani kwa kutaka hata kujua wanakula nini.
  hivyo basi,mh mwakyembe afanye utekelezaji maana matatizo ya watanzania hayahitaji kutafuta uhakiki,yanajulikana na kila mtu.
   
 4. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hiyo task namba tatu ni pahala pake sawiiii maana hajulikani nani rais nani waziri wa mambo ya nje maana rais na waziri wake kutwa wapo ng'ambo
  Kama mwakyembe amefika dodoma salama basi hakuna haja tena mawaziri kumaliza pesa za mafuta ya magari chakufanya unapofika muda wa kikao cha bunge basi wabunge wapaki magari yao majimboni kwao kwa wale ambao train inafika kwao basi watumie usafiri huu japo hili linawezekana Rwanda tu kwa sababu watu wa Rwanda wana akili timamu
   
 5. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Wacha kua bendera fata upepo, hapo wanaonyesha ukarimu wa machoni, PM alilia bungeni kwa ajili ya zeruzeru je alishachukua hatua gani? Hizo ni mbinu za kuwachota wadanganyika akili
   
 6. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,269
  Trophy Points: 280
  Mnafki tu Mwakyembe hana lolote, na arudishe lile V8 atumie Vitara basi.
   
 7. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Wakati gari yake ya uwaziri imekwenda dodoma na dereva tu? dodoma anatumia boda boda? au gari ya bunge .... aache usani wa kutafuta cheap popularity
   
 8. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  V8 imekwenda dom empty na dereva tu, hahahahahahahahah huuu usani mwingine bana?
   
 9. S

  Samkyjr JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Akiweza kufanya usafiri dar uwe wa kuaminika bila kukatisha route na kuongeza nauli ovyo ndipo nitampongeza.
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Dec 1, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Mkuu Wote hao uliowataja hawataweza kumfikia Mimi ninamuita Shujaa

  Mheshimiwa Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe katika Serikali ya

  Mheshimiwa Rais J.Kikwete huyu
  Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe Mchapa

  kazi Hodari. waliobakia wengine ni majina matupu lakini hawafanyi kazi kwa moyo mmoja kama

  huyu
  Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe. Hongera Mheshimiwa Waziri wa

  Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe. Mwenyeezi mungu akulinde na maaduwi zako inshallah.
   
 11. D

  DANNY KIM Member

  #11
  Jan 12, 2014
  Joined: Aug 22, 2013
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umeona mbali wakumbushe hao viongozi wetu
   
Loading...