Kama watanzania hatuna uwezo wa kusomesha watoto wetu, je serikali itaweza?

Nkobe

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
2,162
3,162
Kuna wakati huwa nafikiria. Hivi serikali inayotokana na watu masikini inaweza kuhudumia watu wake kwa kiwango cha kutosha?, Prof Mkumbo alisema jamii ya wajinga uchagua viongozi wajinga. Vivyo hivyo naamini jamii ya watu masikini uzalisha serikali masikini maana kodi ya serikali inatokana na watu wake

Hivi ni asilimia ngapi ya Watanzania wana uwezo wa kusomesha watoto wao hata elimu ya chuo kikuu?, au ni asilimia ngapi wana uwezo wa kusomesha watoto wao hadi sekondari?, au ni asilimia ngapi ya Watanzania wana uwezo wa kujigharamia huduma ya Afya? Baada ya serikali kutangaza kuwa elimu ya msingi ni bure tumeshuhudia mafuriko ya watoto madarasani. Hi kwa kuwa wananchi wenyewe hawawezi kusomesha watoto wao, basi tusitegemee serikali itakuwa na uwezo huo.


Sasa najiuliza kama asilimia kubwa ya Watanzania hatuwezi kusomesha watoto wetu, je serikali itaweza? Hivyo sioni ajabu Serikali kushindwa kuwapa wanafunzi mikopo ya elimu ya juu
 
Tatizo si uwezo ila ahadi. Aliahidi kwamba tatizo la mikopo akiwa raisi litakua historian. Je inamaana alikua anadanganya ili apate kura? Si angekua mkweli tu kuwa hali ni ngumu tushirikiane? Kumbuka pia kauli YAKE " Nchi hii ni tajiri yaweza kuikopesha hata marekani" je hiyo kauri Leo inabadirika na kusema serikali na masikini, hata ni maajabu. MBIO ZA SAKAFUNI HUISHIA UKINGONI
 
Back
Top Bottom