Kama wasomi wenyewe ndio hawa wasiojua Kiswahili fasaha na wanaandika kihuni ni heri waendelee kukosa ajira

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,580
7,938
Kijana mhitimu wa Shahada, stashahada au astashahada hajui Kiswahili fasaha, cha ajabu wengine chuo kikuu wamesoma Shahada ya Elimu na Lugha. Ukipitia kurasa zao Facebook au instagram utaona wameandika hovyohovyo halafu utamsikia anamlaumu Magufuli.

Unataka uwe mwalimu ukawafundishe upumbavu watoto wetu?. Sisi tuliozaliwa kijijini zamani mwalimu wa shule ya msingi alikuwa anatufundisha kuandika au kuongea Kiswahili fasaha sasa kijana mwenye shahada anaandika hovyo tutegemee nini?.

Maneno kama ucku, xmas, xaxa,p, yap yanatokaje kichwani mwa msomi? Kijana wa leo anayetafuta nafasi ofisini huandika Juwa badala ya jua, anaandika ninajuwa badala ya ninajua, huandika kura badala ya kula, huandika ntakuja badala ya nitakuja, barabara huandika balabala, cm badala ya simu, bahalini badala ya baharini.

Msomi hajui kutenganisha kati ya maneno haya; Nipo na niko, hicho na hiko aya na haya. Msomi eti anaandika iko badala ya hiko, uko badala ya huko. Mtu anashindwa kutofautisha neno kwenda na kuondoka.

Analazimisha neno liandikwe kwa kifupi bila kujali miiko ya lugha husika. Kijana mmoja alikuwa katibu wa kikundi hivyo ndiye aliyepaswa kuandika risala, ile risala nilipoipitia nilikutana na makosa mengi mpaka nilishangaa inakuwaje mtu aliyesoma HKL aandike kipumbavu namna ile!

Risala kaandika lisala
Waalikwa kaandika waarikwa na makosa mengine mengi niliyaona.
Vijana wengi hawajui kuandika wasifu(C.V) mzuri na badala yake huhariri C.V walizoziweka watu mtandaoni.

Barua za maombi ya kazi nyingi ni za hovyo , ashukuriwe Mungu maafisa Utumishi wanasoma kichwa tu. Wangesoma neno moja hadi jingine wangekuwa wanacheka sana.
 
Kuna hoja kabisa imeileta jukwani.Atakayepinga akili yake ina walakini.

Wanaudhi sana!!!Wanaandika kiufupi ufupi utadhani visichana vinavyobalehe.

Narudia kusema upo sahihi mkuu bonde la Ufa (siyo Bonde la Baraka).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umekosea kusema wanamlaumu Magufuli! We ungewashambulia wao tu!
Magufuli lazima alaumiwe, alichaguliwa na waliomchagua na hata ambao hawakumchagua lazima wamlaumu waliona mambo hayaendi sawa!! Hata kama hawajui kusoma na kuandika lazima wamlaumu... kwamfano kuacha kujenga madarasa na kuamua kununua mindege cash bila kufuata sheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika tutapata tabu sana Mana wapumbavu ni wengi sana akiwepo mleta uzi.
Kiswahili ni kigumu mno. Yani mleta uzi unashindwa kuelewa kuwa wasomi wengi tunasoma mitaala ya kingereza mashuleni.

Nifafanulie loop the loop kwa kiswahili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom