Alex Fredrick
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 680
- 1,338
Majuzi tumeona vyombo vya habari ulimwenguni vimeripoti kuwa karibu 80 % ya Wananchi wa Urusi wanaunga mkono Rais Putin aongozewe muda zaidi wa kuongoza Taifa hilo.
Na sababu ya msingi ni moja tu kuwa Rais Putin ameipaisha sana Urusi kwenye medani karibu zote hasa zaidi Uchumi na imekuwa tisho kwa Nchi za Ulaya na Marekani.
Naamini sisi Watanzania mwaka 2025 baada ya Mh. Rais Magufuli kumaliza ngwe yake ya pili tuna kila sababu ya kumuongezea muda ili aendelee kutuongoza.
SGR, Stiglers pale Rufiji. Vituo vya afya karibu kila kijiji, Madawa kutoka Bajeti ya billion 34 mpka sasa billion 269, Elimu bure kutoka msingi mpka secondary, ununuzi wa ndege na kufufua Shirika la ATCL, Kubadilisha Sheria zote za madini na matokeo yake tayari tumeanza kuyaona mfano ACCACIA.
Huduma za Bima ya afya na sasa hivi Wizara ya Afya inaandaa muswada ili kila Mtanzania aweze kuwa na Bima ya afya. Nidhamu imerudi Serikali na Taasisi zote za mashirika ya umma sanjali na kuondoa wafanyakazi hewa ambao walikuwa wanaliingizia Taifa hasara kubwa.
Kwa haya na mengine yote kama Taifa tuna kila sababu ya kuendelea kumpa Mh Rais Magufuli ridhaa ya kutuongoza baada ya kumaliza kipindi chake 2025. Tuache dhana mfu kwamba Kiongozi akimaliza vipindi viwili hawezi kuendelea kwasababu ya Katiba wakati Katiba sio "MSAHAFU"
Tuomeona miongo ya hivi karibuni kwamba Viongozi wakimaliza vipindi vyao huku Taifa likiwa hoi kwenye medani za Uchumi na Ufisadi ukitamalaki kila eneo.
Tumuache Rais Magufuli andelea kuliongoza Taifa hili maana tumechezewa vya kutosha na tumebezwa vya kutosha na hata majirani zetu kwa miongo kadhaa kwamba tuna rasilimali za kila namna lakini hakuna maendeleo.
##JPM KIOO TUELEKEACHO