Kama Wanasimba tunajiamini tuna timu imara, kwa nini tunaombea tukutane na Al Ahly Tripoli, siyo TP Mazembe au Orlando Pirates?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,518
108,793
Si tunajiamini kuwa Simba ni Timu Bora kabisa na tumepita CAFCC jana Aprili 4, 2022 kwa uwezo wetu na tuna jeuri ya kucheza na timu yoyote Afrika, sasa kwa nini karibia 99% ya Wanasimba wanaombea wakutane na Al Ahly Tripoli ya nchini Libya na kamwe siyo TP Mazembe ya Congo DR au Orlando Pirates ya South Africa?

Tukisema ukweli kuwa kwa kiwango cha Simba SC kwa sasa na kwa aina ya wachezaji tulionao pamoja na uwekezaji wetu mchanga kwa hizi timu tatu ambazo moja wapo tutacheza nao Simba SC 'hatutotoboa' kwenda Nusu Fainali ya Shirikisho mnanitukana na mnatutukana tuliowazidi upeo, maono na jicho kali la uchambuzi wa michezo ( hasa Mpira wa Miguu wa Tanzania) na masuala mengine.

Ninasisitiza hapo ndiyo mwisho Wetu!
 
Si tunajiamini kuwa Simba SC ni Timu Bora kabisa na tumepita CAFCC Jana kwa Uwezo wetu na tuna Jeuri ya Kucheza na Timu yoyote Afrika sasa kwanini karibia 99% ya Wanasimba wanaombea wakutane na Al Ahly Tripoli ya nchini Libya na kamwe siyo TP Mazembe ya Congo DR au Orlando Pirates ya South Africa...
Akiyekuambia hizo habari ni nani na mlikuwa wapi?
 
Kwani hao TP mazembe unafikiri wao wanapenda wakutanishwe na sisi?

Unataka kusema Mazembe ni mkubwa sana kuliko Al Ahly?

Au ile welcome form one tuliyowaachia kwenye simba day ndio inakuzuzua?

Au unafikiri hofu ipo kwetu tu, hapo ni miamba kwa miamba yeyote anaweza akapasuka na ndio maana kila mmoja anamgombea kibonde

Ni bahati tu yanga hayupo kwenye haya mashindano ila angekuwepo saizi usingemuongelea Al Ahly Tripol kama kibonde
 
Si tunajiamini kuwa Simba SC ni Timu Bora kabisa na tumepita CAFCC Jana kwa Uwezo wetu na tuna Jeuri ya Kucheza na Timu yoyote Afrika sasa kwanini karibia 99% ya Wanasimba wanaombea wakutane na Al Ahly Tripoli ya nchini Libya na kamwe siyo TP Mazembe ya Congo DR au Orlando Pirates ya South Africa...
Kumkwepa mpinzani mgumu hatumaanishi kuwa hatuiamini timu au mbaya bali ni hali ya kutaka hope na uhakika.

Unaweza aTripoli na ukatoka same unaweza kupewa Mazembe na ukapita football ina matokeo ya ajabu sana.

Me nadhani wanasimba kwasasa wawekeze kwenye kuisapoti timu na wachezaji kwanini kila sababu ya kuweka historia mpya tunayo.
 
Kwani hao Tp mazembe unafikiri wao wanapenda wakutanishwe na sisi?

Unataka kusema Mazembe ni mkubwa sana kuliko Al Ahly...
Kuwaachia? Umesahau zile 4 msimu ule mkatoka robo? Halafu hiyo ni Ahl Tripoli ya Libya sio Ahly ya Misri usiwafananishe na Mazembe tafadhali.
 
Huyo Simba damu sema akili zake haziko sawa soon ataanzisha UZI wa kueleza waganga walivyojipanga kuifunga MAZEMBE
Haaaaaahaaaaaaa wewe ndio umeongea sasa nashangaa wanasimba wanaomshambulia jamaa nani asiyemjua kama jamaa ni mnyama?
 
Kwani hao Tp mazembe unafikiri wao wanapenda wakutanishwe na sisi?

Hivi huwa mnajionaje mzee? Mnajiona kama kina Al Ahly hivi?

Wewe kutoka robo ni mafanikio. Lakini kwa timu kama TP Mazembe, Esperance, Wydad n.k kutoka robo ni kutofikia malengo na kocha anafukuzwa kabisa.

Ebu chill. Know your place.

Acha kujenga ghorofa kichwani.

Jipange ili malengo yafike angalau nusu fainali michuano ijayo.

Kwa hapa ulipofikia, tayari ushatimiza malengo. Huko kwengine ni kuwakilisha tu.
 
Si tunajiamini kuwa Simba SC ni Timu Bora kabisa na tumepita CAFCC Jana kwa Uwezo wetu na tuna Jeuri ya Kucheza na Timu yoyote Afrika sasa kwanini karibia 99% ya Wanasimba wanaombea wakutane na Al Ahly Tripoli ya nchini Libya na kamwe siyo TP Mazembe ya Congo DR au Orlando Pirates ya South Africa...
Sema mwisho wako usituchanganye na sisi. Simba Iko byeeee yoyote tutakae kutana nae tu tunamtwanga.
 
Hivi huwa mnajionaje mzee? Mnajiona kama kina Al Ahly hivi?

Wewe kutoka robo ni mafanikio. Lakini kwa timu kama TP Mazembe, Esperance, Wydad n.k kutoka robo ni kutofikia malengo na kocha anafukuzwa kabisa...
Kwamba Pablo asipovuka robo finali anabaki?? We ndez kweli
 
Kwamba Pablo asipovuka robo finali anabaki?? We ndez kweli
Ukiitwa mpumbavu uone unatukanwa na kumbe unastahili.

Level ya Simba ni robo fainali, huko kwengine ni majaliwa tu. Si lengo.

Taratibu inavyoenda na kushiriki mara kwa mara ndivyo watazidi kutanua malengo yao.

Hivi unasikilizaga hata press za afisa wa habari wa Simba au umekalia kijiweni na wenzio wa darasa la saba?

Kwa mujibu wake, Simba iliazimia kufika robo fainali na ndo' kitu walichokuwa wanaota na kukiimba kwa wachezaji.

Lengo limetimia.

Au hujui malengo huwa yanawekwaje?

Timu inajipima kwa mabavu yake ya budget na uzoefu. Timu kama Simba haiwezi ikaweka malengo sawa na Al Ahly au Mamelodi.

Hao wakiishia robo ni dhihaka wakati kwetu ni fahari.

Kusema hii Simba imelenga kubeba ubingwa ni kuwa na funza kichwani, labda kama michezo yote itachezwa Benjamin Mkapa.

Umfukuze Pablo kwa kutokufika nusu fainali kwa uwekezaji gani huo? Bajeti ya timu nzima ya Simba kwa mwaka, wakina Pyramid wanasajilia mchezaji mmoja.

Achilia mbali uhakika wa kushinda game away ni kutiatia maji, ukifanikiwa ni draw against teams like USGN.

Hiyo Robo au nusu unapita kimiujiza?

Pathetic.
 
Hahahaha mashabiki wa Simba ni wazuri sana wa kujitoa akili, kupoteza kumbukumbu ya uhalisia wao na kujitutumua kujaa kama puto wakisahau kuna kupasuka. Kwa mawazo yao tu ya Abunuasi basi kwa haraka utawagundua. Hawana huo uwezo hata kama wakicheza mechi zote kwa mkapa. Ni vizuri wakajipongeza kwa kufikia malengo na uwezo wao ulipoishia na sio kujitumumua kuwa wanaweza songa hatua zaidi ya hii.
 
Back
Top Bottom