Kama wanajadili waziwazi namna ya kukwapua Mali ya Umma, ni dhahiri walimchukia na hawakupenda hayati Magufuli awepo. Inaonekana aliwabana sana!

Mahindi mabichi yana virutubisho vingi zaidi kuliko sembe.Pia sio rahisi kula kupitiliza mahindi mabichi kama ilivyo kwa ugali.
Umekazania sana ugali. hata uwe wa mahindi, nakwambia hayo mahindi yanaliwa Ulaya, hayo mahindi yanaliwa India, hayo mahindi yanaliwa America. Tanzania tunaweza kula mahindi kwa kuyapika, au kutengeneza ugali. Kwa taarifa yako nutrients ni zile zile.
Mzungu akila mahindi yalochemshwa, au yalochomwa nawe ukapika ugali, nutrients ni zile zile. Elewa ndugu yangu, usidharau uafrica kisa ugali.
Wazungu wanakula sana nafaka. Hivi mikate inatokana na nini? Ni kupe siri tu! Tembelea shule zilizo na mchanganyiko wa waafrica na wazungu. Chunguza matokeo kama ujaambiwa black wanaongoza.
Wanaijeria wanakula ugali hata huko Ulaya, na kuna maduka ya Kiafrica. But nijeria bado wako na akili kubwa tu. Na sasa wanawasubua wazungu kwa kuiba kwa mitandao. Ukiwauliza wanaijeria kwanini wanafanya hivyo, wanakwambia wazungu waliwatawala babu zetu, wakachukua mengi toka Africa sasa tunalipiza kisasi.

Na kila siku wanawaliza wazungu, wazungu wameshindwa kuwazuia hao unaodai wana IQ kubwa. Wanaijeria wanakula ugali. Hizo akili wametoa wapi?

Unakubali unakula ugali wa mtama. Sasa unalaumu ugali wa nini! Na nina amini unaakili nzuri tu pamoja unakula ugali. Nyerere amelelewa kwa ugali wa Mtama na ulezi. Lakini alikuwa na akili hadi wazungu wanajiuliza. Tumekuwa na viongozi mashuhuri wamelelewa kwa ugali. Chenge amesoma Havard University, na kwao Bariadi wanakula sana ugali tena ule mgumu. Hivi kama ugali unaleta IQ ndogo angeweza kwenda hiko chuo?
Swala si ugali, nutrients za kwenye ugali ndo hizo unazipata katika mahindi wanayo kula huko china, Wanayo kula huko Ulaya. nadhani unajua American Gadern Product. Wana corn, ambayo ni mahindi kwenye mikebe yanalika sana. Na mengine ni maalum kwa kuchoma. Elewa ndugu yangu.

Haya maswala ya maendeleo, ni kutokuwa na uzalendo na kutekeleza mipango tunayojiwekea. Rushwa kuwa ndo msingi mkuu wa watu wengi. Ni ngumu kupata maendeleo. Siyo IQ kama unavyodhani.

Ingekuwa IQ, Japan China, India na hata Ulaya miaka ya 60 walikuwa maskini wa kutupwa. Kwani walikuwa hawali vyakula wanavyokula?
Sipo kubishana kuonekana nani ni mshindi. Ila sikubaliani na hoja yako kwamba nchi za Kusini mwa jangwa la sahara ni masikini kisa zina LOW IQ. Nakukatalia. Nimekupa mifano mingi, lakini umekalia ugali.

Kuna kanisa moja nimesali hapo Ulaya. Linamchanganyiko wa kila mataifa, Wazungu, Wakorea, Wajapan, walatino, wahindi, waafrika na wengineo. Uwa wanapika kanisani kila tunapokutana. Wanaijeria ikifika zamu yao wanapika Ugali. Na wazungu wengi upenda na mara nyingi wanapendekeza wanaijeria wapike ugali wao wanaita fufu. Nilishawahi kupata mwaliko kwa mzungu mmoja alie waalika rafiki na ndugu kuja kula ugali.
Huyu mzungu alizaliwa na kukulia Africa. Waliishi Iringa, na anasema walikula ugali kwa wingi. Na yeye alipenda sana ugali. Hivyo kila siku alikula ugali. Aliporudi Ulaya alijitahidi kupika ugali japo anasema alikuwa haoni kama unakuwa mzuri kama ule unaopikwa na watanzania. Ndo maana alinialika. Siku hiyo kulikuwa na watu kama Ishirini hivi wameharikwa. Nilipika ugali wa mahindi, kila mtu alipenda.

Wakapendekeza tuwe na special day ya kula ugali, na mihogo yaani tropical food. Huyu ndugu anafanya kazi katika moja ya vinu vya nyuklia vinavyozalisha umeme. Ni mtaalamu sana na anaakili. Alizaliwa na kulelewa Tanzania, alipenda ugali. hata ulaya leo bado anakula ugali. Angekuwa na IQ ndogo asingeweza kufanya kazi katika hiyo sekta ya nyuklia. Tumepanga siku moja anakuja Tanzania kujitolea kufanya mradi fulani wa vijana. I wish ningekukutanisha nae. Lakini niachie hapa. Endelea kuamini unacho amini nami nitaamini navyo amini.
Sijaona akili ya za watu kupungua kula ugali. Kuna maduka mengi yanauza unga wa mahindi.
 
Kumbe ukitaka uchukiwe na wanaCcm basi we ziba mianya yao ya kuiba mali ya umma.

Hayati JPM alichukiwa na wanaCcm japokuwa walicheka nae na kumzunguka hio hii ni sababu aliwabana sana juu ya rushwa na ufisadi.

Sasa wanatoa michongo namna ya kupiga madili.

Naona tangu amefariki wanachekelea tu na kukenua meno
CCM na awamu zao zote tu ni wezi. Hakuna cha mama wala shujaa.
 
Kumbe ukitaka uchukiwe na wanaCcm basi we ziba mianya yao ya kuiba mali ya umma.

Hayati JPM alichukiwa na wanaCcm japokuwa walicheka nae na kumzunguka hio hii ni sababu aliwabana sana juu ya rushwa na ufisadi.

Sasa wanatoa michongo namna ya kupiga madili.

Naona tangu amefariki wanachekelea tu na kukenua meno
Una uhakika kwamba yeye mwenyewe hakuwa na kundi lake la wezi?. Usimgeuze JPM kama vile ni malaika au kashuka kutoka mbinguni.

Aliishi na binadamu, alizungukwa na wapigaji kila kona. Alikuwa na hulka za kisiasa ambazo zilimuweka karibu na wananchi na akaaminiwa.

Lakini alikuwa ni binadamu kama mimi na wewe.
 
Una uhakika kwamba yeye mwenyewe hakuwa na kundi lake la wezi?. Usimgeuze JPM kama vile ni malaika au kashuka kutoka mbinguni.

Aliishi na binadamu, alizungukwa na wapigaji kila kona. Alikuwa na hulka za kisiasa ambazo zilimuweka karibu na wananchi na akaaminiwa.

Lakini alikuwa ni binadamu kama mimi na wewe.
Una clip yoyote akiwa na wapigaji wenzake wakujadili namna ya kukwapua?
 
Una clip yoyote akiwa na wapigaji wenzake wakujadili namna ya kukwapua?
Ukisikia trilioni 1.5 imeibiwa na serikali ya JPM unaweza kuweka ushahidi hadharani?. Wale wezi wa EPA na majengo pacha ya BOT waliiba mabilioni ya shilingi, unaweza kuweka ushahidi wowote hadharani?.
 
Ukisikia trilioni 1.5 imeibiwa na serikali ya JPM unaweza kuweka ushahidi hadharani?. Wale wezi wa EPA na majengo pacha ya BOT waliiba mabilioni ya shilingi, unaweza kuweka ushahidi wowote hadharani?.
Huna sifa ya kubishana na mimi. Kaa kimya usitafute umaarufu.
 
Back
Top Bottom