Kama wana CHADEMA 'wanaozunguka' kuomba 'Kura' za Halima Mdee 'Kawe' wana 'Udhaifu' huu, basi 'namtabiria' Askofu Gwajima Ushindi asubuhi tu!

Halafu sijui hii hulka ya kumwambia mbunge hakuleta maendeleo watu wanaitoa wapi ?

Yaani karne ya 21 watu bado hawaelewi na kutofautisha majukumu na hisani.

Mwingine anakusanya kodi yako halafu maendeleo anabembelezws kuleta ila asiyepokea hata mia ndio anatakiwa kuleta maendeleo.

Hili ni tatizo la wananchi kukaa kusaidiwa saidiwa badala kudai haki ya kodi yao ndio maana wanaona maendeleo ni hisani au msaada kutoka kwa yeyote.

narudia tena,huu uiinga cdm unakwenda kuwaponza sana.

kama kazi ya mhunge ni kwenda kukata viuno bungeni,tutajua mwaka huu.

unaandika nini wewe???
 
Jana nilibahatika Kukutana na wana CHADEMA baadhi ambao nadhani ( nahisi ) walipewa 'Jukumu' la Kupitapita Kawe hasa katika 'Nyumba' za Watu na Kumuombea 'Kura' Mgombea Ubunge CHADEMA Halima Mdee. Sina tatizo na 'Mbinu' yao hii ila GENTAMYCINE nina tatizo Kubwa sana na 'Competence' ya hawa wana CHADEMA wanaozunguka.

Huku nikiwa katika 'harakati' zangu za hapa na pale na jana nikiwa Jimbo la Kawe nilibahatika Kukutana na hawa wana CHADEMA kwa 'nyakati' tofauti ambapo wote kila walipokuwa wakikutana na Watu na Kuwaelezea 'Sera' zao ( CHADEMA ) na 'Kumnadi' Mgombea wao Halima Mdee walikuwa wanaonyesha 'Udhaifu' wa wazi wazi katika 'Kuchambua' na 'Kufafanua' Mambo ( Masuala )

Nilipishana na mwana CHADEMA 'mzungukaji' wa Kwanza ambapo alimsimamisha Mama Mmoja hivi na kuanza 'Kujinadi' na 'Kumnadi' Halima Mdee ambapo aliulizwa na huyo Mama kuwa ampe tu 'Tathmini' fupi ya 'Mema' yanayoonekana yaliyofanywa na Mdee ambapo kwa 'Masikitiko' yangu makubwa Yule Kijana aliishia 'Kujiumauma' tu na 'Kujilamba' mdomo kama Chatu wa Gamboshi.

Wakati naikatiza Mitaa ya Kawe mbele tena nikakutana na wana CHADEMA 'wanaozungukazunguka' na kuna Mmoja nikamuona 'kambananisha' Mzee wa Watu huku 'akimnadi' Halima Mdee amnbapo nilimsikia Yule Mzee akimuuliza Je, anadhani Siasa anazozifanya Mdee zinaendana na 'nyakati' tuliopo Kimaadili na Kimaendelea Jamaa akabadili 'Mada' na Kuanza Kuzungumzia Mechi ya Leo ya Yanga SC na Kagera Sugar.

CHADEMA Kawe nilikuwa nawaamini na kuwa na 'Imani' nanyi ila kwa 'Udhaifu' huu tu mchache niliouona Askofu Gwajima ni Mbunge rasmi Kawe.
mkuu, sisi wakazi wa Kawe siyo kama wa huko kwenu Buza. huku kwetu tuna jambo letu na MATAGA - hata Bashite aliufyata.

Bashite alijipitishapitisha huku kwa kununulia watu na makanisa magari, majenereta, nk... akaona bado hatusomeki akakimbilia Kigamboni.

seuze huyu steringi wa movie za X?
 
Watu wanamlaumu mtoa mada while sio yeye aliekua anauliza maswali au kuyajibu maswali...

Yeye amefanya kutoa report tu habari km ilivyo, and probably kutoa angalizo vijana wanolewe kwanza, wakirudi field wawe wameiva...Mtoa mada amekua mjumbe tu,na mjumbe hauwawi...heb tujifunze kuchukua mapungufu yetu na kuyafanyia kazi instead of being defensive on them.

Anything negative abt upinzani watu wanatoka mapovu km yote, hili linanipa waswas upinzani ukishinda hali itakuaje...Je utakua teyari kukosolewa? au ndo itakua tunatoa mbabe mmoja tunaweka wengine...??

Anyway ni mtazamo wangu tu,Great thinker msijenge chuki..tupo hapa kujenga nyumba moja Tanzania no need for hate or Matusi.
 
Swala liko hivi: kinachotakiwa ni kwamba watu tupige kura nyingi dhidi ya ccm ili tuwaondoe madarakani kusudi tuone akina Halima nao wakiwa na serikali watafanya nini.

Hapo ndipo tutakuwa tumewatendea haki akina Halima maanake sasa wao ndio watakaokuwa wanakusanya kodi zetu, lkn hili la kumlaumu sasa sio haki.

Nchi hii kwa ujumla bado maendeleo ni changamoto kubwa sana katika maeneo karibu yote ya nchi kiasi kwamba kama ni kulaumu wabunge basi leo hii tusingepaswa hata kwenda kwenye uchaguzi kupiga kura. Itakuwa ni kupoteza muda tu.
 
Kwa umri wako bila shaka ni mtu mzima ilo sina shaka nalo!!kinachonipa mashaka ni uelewa wako!!yaani kwa umri huo hujui hata kazi za mbunge ni zipi?!!unakaa unaamini kabisa kuwa mbunge anaweza kukuletea maendeleo?!!nimekudharau sana,wale mbuzi waliokuwa wanatafuna mabango ya picha ya tapeli gwajima,wanakuzidi maarifa.
 
Halima hafai
Gwajima hafai zaidi...
Halima hafai kuwa mbunge.
Gwajima hafai kuwa hata mgombea tu..

Kawe mwaka huu I wish wawakatae wote
Tuna mtihani sana mkuu. Binafsi nimemuunga mkono Gwajima ili kuona kama walau tutapata msemaji wa mambo ya Kawe.

Halima alijisahau sana, jimboni haonekani, bungeni ni madongo kwa "jiwe" tu huku Kawe haisikiki kabisa ikisemewa.

Chaguzi zote nilimchagua Mdee ila safari hii HAPANA.
 
Jana nilibahatika Kukutana na wana CHADEMA baadhi ambao nadhani ( nahisi ) walipewa 'Jukumu' la Kupitapita Kawe hasa katika 'Nyumba' za Watu na Kumuombea 'Kura' Mgombea Ubunge CHADEMA Halima Mdee. Sina tatizo na 'Mbinu' yao hii ila GENTAMYCINE nina tatizo Kubwa sana na 'Competence' ya hawa wana CHADEMA wanaozunguka.

Huku nikiwa katika 'harakati' zangu za hapa na pale na jana nikiwa Jimbo la Kawe nilibahatika Kukutana na hawa wana CHADEMA kwa 'nyakati' tofauti ambapo wote kila walipokuwa wakikutana na Watu na Kuwaelezea 'Sera' zao ( CHADEMA ) na 'Kumnadi' Mgombea wao Halima Mdee walikuwa wanaonyesha 'Udhaifu' wa wazi wazi katika 'Kuchambua' na 'Kufafanua' Mambo ( Masuala )

Nilipishana na mwana CHADEMA 'mzungukaji' wa Kwanza ambapo alimsimamisha Mama Mmoja hivi na kuanza 'Kujinadi' na 'Kumnadi' Halima Mdee ambapo aliulizwa na huyo Mama kuwa ampe tu 'Tathmini' fupi ya 'Mema' yanayoonekana yaliyofanywa na Mdee ambapo kwa 'Masikitiko' yangu makubwa Yule Kijana aliishia 'Kujiumauma' tu na 'Kujilamba' mdomo kama Chatu wa Gamboshi.

Wakati naikatiza Mitaa ya Kawe mbele tena nikakutana na wana CHADEMA 'wanaozungukazunguka' na kuna Mmoja nikamuona 'kambananisha' Mzee wa Watu huku 'akimnadi' Halima Mdee amnbapo nilimsikia Yule Mzee akimuuliza Je, anadhani Siasa anazozifanya Mdee zinaendana na 'nyakati' tuliopo Kimaadili na Kimaendelea Jamaa akabadili 'Mada' na Kuanza Kuzungumzia Mechi ya Leo ya Yanga SC na Kagera Sugar.

CHADEMA Kawe nilikuwa nawaamini na kuwa na 'Imani' nanyi ila kwa 'Udhaifu' huu tu mchache niliouona Askofu Gwajima ni Mbunge rasmi Kawe.
Kama Halima Mdee anaonyesha kwa dhahiri kabisa kuwa hatoshi kwa kipindi hiki, na huku Gwajima naye ni "reject" basi ni lazima wana Kawe tujielekeze kwa mgombea wa ACT - Wazalendo. Huyu "second runner up" ndiye mtu sahihi kwetu, kwa sababu ya msimamo thabiti wa Maalim Seif.
 
Mkuu nisikufiche hii 'post' yako imeanza 'Kunishawishi' tarehe 28 Oktoba 2020 nimpige tu 'Kura' yangu Rais JPM, ila kwa 'Ubunge' nisipoteze Muda.
Mkuu mbona wewe mjanja? Kwa nini unapoteza kura yako hiyo ya urais kwa kumpa aliyeshindwa tayari?
 
Back
Top Bottom