Kama wabunge wa chadema wangewauliza wananchi wa majimbo yao, wangetoka ukumbini?

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
199
suala la wabunge wa chadema kususia hotuba ya rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania tarehe 18 novemba 2010 limezusha hisia na maoni tofauti kutoka kwa wadau mbali mbali. Wapo wanaoona kuwa wabunge hao wamefanya sahihi lakini pia wapo wanaona kuwa wabunge hao wamekosea.

Taarifa zinazoonyesha kuwa kabla ya uamuzi huo kupitishwa wabunge wa chadema, walipitia mchakato wa kidemokrasia wa kupiga kura ambapo wale waliounga mkono kususia hotuba hiyo walishinda.

Baadhi ya wabunge ambao hawakuunga mkono uamuzi huo iliwawia vigumu sana hata kuhudhuria mkutano huo kwa hofu ya kushindwa kutekeleza uamuzi huo. (1) je nini kiliwafanya baadhi ya wabunge kuhofia kutekeleza uamuzi wa kususia hotuba ya rais, na hivyo kushindwa hata kuhudhuria kiako hicho cha bunge kabisa?

Aidha baadhi ya wabunge kama mhe zitto kabwe amelazimika kutoa maelezo yanayoonyesha kuwa binafsi hakuwa sehemu ya uamuzi huo, ila uamuzi hauo ni wa chama. Na pia hauungi mkono uamuzi wa kususia hotuba ya rais kikwete ? (2) ni kwanini mhe zitto kabwe amelazimika kutoa maelezo ya aina hiyo ambayo baadhi yetu tumeyapokea in a very negative way?

Yafuatayo ni maoni yangu binafsi kuhusu masuala hayo mawili niliyoyaweka kwa njia ya maswali (1 & 2).

Lakini kwanza niweke bayana msimamo wangu kuhusu kususiwa kwa hotuba hiyo ndipo nitakuwa huru kujadili. Tokea awali nilisikitika sana niliposikia katika mkutano na waandishi wa habari ambapo dr slaa na mhe mbowe walisema kuwa wabunge wa chadema watahudhuria hotuba ya rais. Lakini niliposikia kwa njia ya redio kuwa mashujaa wetu wamesimama na wanatoka nje ya ukumbi wa bunge furaha yangu ilikuwa ni kubwa kuliko kifani na angalau kunipunguzia madonda ya kuibiwa kura zetu.

Suala (1)
je nini kiliwafanya baadhi ya wabunge kuhofia kutekeleza uamuzi wa kususia hotuba ya rais, na hivyo kushindwa hata kuhudhuria kiako hicho cha bunge kabisa? kimsingi mbunge ni mwakilishi wa wananchi wa jimbo analotoka, hivyo hatakiwi kupeleka maoni yake binafsi bungeni kama wanavyofanya wabunge wengi wa ccm, anatakiwa kupeleka yake aliyokubaliana na waliomchagua.

Hivyo nahisi kigugumizi walichokuwa nacho baadhi ya wabunge kuhusu uamuzi huo ni kutokuwa na uhakika wa maoni ya wananchi wanaowawakilisha hapo bungeni ikikumbukwa kuwa ni siku chache tu wameachana na hawakuwa na vikao vyovyote kukubalina kuhsu uamuzi mzito kama huo. Je wananchi waliowachagua watawaunga mkono au kupinga kitendo hicho.

(2) ni kwanini mhe zitto kabwe amelazimika kutoa maelezo ya aina hiyo ambayo baadhi yetu tumeyapokea in a very negative way? kwa maoni yangu naona mhe zitto kabwe yuko sahihi kabisa kutoa maelezo ya ziada ya kujitenga na uamuzi huo wa chama kama mtu binafsi mbele ya wapiga kura wake wa kigoma. Ana haki ya kuwaonyesha kuwa ule ulikuwa uamuzi wa chama.

Kwa kufanya hivyo mhe zitto kabwe ametumia ipasavyo mapungufu yaliyopo katika katiba ya tanzania ambayo chadema tunataka ibadilishwe kujisafisha mbele ya wapiga kura wake. Nampongeza sana kwa kujali hisia za wapiga kura wake. Na ni amoni yangu kuwa wasiokuwa wapiga kura wa jimbo lake hawana haki ya kumhukumu kuhusu hilo.

Kimsingi hata wale wanaowanyooshea vidole mhe zitto kabwe na wengine waliojali zaidi matakwa ya wapiga kura wao zaidi ya chama wana hangover ya katiba mbovu ambayo inajali zaidi "party supremacy" yaani "chama kushika hatamu" badala ya wananchi kushika hatamu. Hivyo wanapaswa kupigwa msasa ili waendane na matakwa ya kubadili katiba hii mbovu.

kimsingi uamuzi ule ulikuwa mzito sana; na kufuatiwa kitendo cha kijasiri na kihistoria cha wabunge wetu walioshiriki kwa moyo wa dhati. Hivyo nawapongeza sana wabunge walioshiriki kikamilifu; lakini pia nawapongeza wale walioshikwa na kigugumizi kwa kutambua na kuonyesha kujali maoni ya wale wanaowawakilisha. Msingi wa hoja hii ni pale mbunge anapotambua kuwa kura za wanachama na wapenzi wa chadema zisingetosha kumpitisha kuingia bungeni hivyo alilazimika kuomba kura kwa wanachama wa ccm na ana uhakika kuwa wanaccm walimchagua kwa kishindo.

kimsingi chadema ndio imeibuka mshindi kwa kuonyesha kwa vitendo inajali maslahi ya taifa mbele ya wananchi. Aidha ni pigo kubwa kwa ccm kutokana na ukweli kwamba kura za wanancm ndizo zilizosabisha rais kikwete asusiwe.


naomba kuwasilisha!!!!
 

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
229
Na kama wabunge wa CCM wangekuwa wanawauliza wapiga kura wao majimboni kwamba waitetee Bungeni ufisadi unaufanywa na viongozi wakuu wangewakubalia?

Maswali mengine haya maana kabisa!
 

Epifania

Senior Member
Oct 18, 2010
132
2
Hivi wanachi wanapompa mtu dhamana ya kuwawakilisha haimaanishi kumpa kibali cha kufanya maamuzi kwa niaba yao panapokuwa na critical issues zinazohitaji maamuzi ya haraka? Hao ambao hawakutoa ushirikiano labda watupe maelezo mengine ambayo yataridhisha umma, vinginevyo mtuambie kuwa kitendo kile kilikuwa ni makosa na muainishe ili tuelewe. Mimi naendelea kuona ni usaliti iwapo Mwenyekiti wa chama ameongozana na baadhi ya wanachama wake na wengine kubaki au kutohudhuria, kwangu naona kama wako mguu nje mguu ndani hao au waliwatuma wenzao kama chambo.
 

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
199
hivi wanachi wanapompa mtu dhamana ya kuwawakilisha haimaanishi kumpa kibali cha kufanya maamuzi kwa niaba yao panapokuwa na critical issues zinazohitaji maamuzi ya haraka? Hao ambao hawakutoa ushirikiano labda watupe maelezo mengine ambayo yataridhisha umma, vinginevyo mtuambie kuwa kitendo kile kilikuwa ni makosa na muainishe ili tuelewe. Mimi naendelea kuona ni usaliti iwapo mwenyekiti wa chama ameongozana na baadhi ya wanachama wake na wengine kubaki au kutohudhuria, kwangu naona kama wako mguu nje mguu ndani hao au waliwatuma wenzao kama chambo.

ni lazima mbunge mwenye hekima apime na maoni ya wananchi anowawakilisha. Hayo ni mawazo ya kiccm kuwa ili mradi umeshakuwa mbunge basi chama kilichokusimamisha ndio kinapora uwakilishi wa wananchi. Mimi nilisimamia kura za mmoja wa hao wabunge na niano ushahidi kuwa wananccm wengi walimchagua mbunge wa chadema, hivyo ni busara akwakumbuka kila mara anapofanya maamuzi na kutekelza shughuli zake.

Ndio maan ni muhimu katiba ikabadilika haraka kabla ya chama kingine kuingia madarakani, ama sivyo kinaweza kuingia chama kingine madarakani na kikaing'ang'ania katiba hii mabovu kama watu wanavyodai sula la party supremacy zaidi ya wananchi. Shem on you all, hamstahili hata kujiita wataka mabadiliko.
 

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
199
na kama wabunge wa ccm wangekuwa wanawauliza wapiga kura wao majimboni kwamba waitetee bungeni ufisadi unaufanywa na viongozi wakuu wangewakubalia?

Maswali mengine haya maana kabisa!
ndio maana tunaikataa ccm kwa sababu ya kupora haki za wananchi kupitia katiba mbovu, sasa iweje mtake kutumia katiba hiyo hiyo kufanikisha unyanyasahi wa wabunge wa chadema? tunataka kutoka kwenye "party supremacy" kwenda kwenye "civilian supremacy" ndicho walichofanya baadhi ya wabunge wenye kuamini katika nguvu ya umma ya ukweli.
 

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
9,558
Wasingetoka nje ningerudisha kadi nisiwe na chama kabisa. Haiwezekani watangaze kutokutambua matokeo huku wanamsikiliza msanii.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom