Kama viongozi wa bodi ya mamlaka ya mapato wanafanya haya tutapataje kupona kiuchumi??

Mwaikibaki

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,975
3,623
Wanabodi

Nimesikitika na kufadhaika baada ya mkuu wa kaya kutoa waziwazi pasipo kificho sababu iliyopelekea kuivunjilia mbali bodi ya mamlaka ya mapato.

Kwa hali hii napata mashaka kua tutawezaje kufikia malengo yetu ya viwanda kama tunaowategemea kutuongoza kukusanya mapato wanafanya waliyofanya.

Hii inanifanya nitilie shaka hata takwimu za mapato ambazo wamekua wakitoa.Ultimately hata takwimu za GDP nazo zinaacha maswali kadhaa.

Imefika pahala sasa tutoe mawazo namna ipi bora ya kusafisha uozo ulioko kwenye mifumo yetu.

Ikumbukwe vita ya wala rushwa..mafisadi haiwezi pigwa na mtu mmoja,ni ya muda mrefu na ya ushirikiano.
 
Ungeweka wazi hiyo sababu tafadhali maana wengine wetu hatukupata fursa ya kusikia kilichosemwa mkuu.
 
Back
Top Bottom