Kama utekelezaji wa Bajeti ndio huu,kuna haja gani ya kuwa na Bunge la Bajeti awamu hii?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,987
144,319
"Mwaka wa fedha 2018/19 Wizara ya madini iliidhinishiwa sh. Bilioni 19.620 kw ajili ya miradi ya maendeleo, fedha iliyopokelewa kutoka hazina hadi kufikia February, 2019 ilikuwa ni sh. milioni 100 tu, sawa na 0.5% ya bajeti yote ya fedha" Silinde.

Ni bahati mbaya sana kwamba Serikali hii ya awamu ya tano inatekeleza uchumi wa viwanda kwa kupeleka asilimia 6 ya fedha za maendeleo kwenye Wizara ya Viwanda; na pia bila aibu haipeleki chochote kwenye Idara ya biashara na uwekezaji." Silinde.

"Idara ya Biashara na Uwekezaji Fungu 60 ilikuwa imetengewa shilingi bilioni 7 kwa ajili ya maendeleo; lakini hadi Machi, 2019 hakuna hata shilingi moja iliyokuwa imepokelewa. Hii ina maana kwamba bajeti ya maendeleo katika idara hii haikutekelezwa kabisa." Silinde

"kwa mwaka 2018/19 Tume ya Ardhi ilitengewa sh. bilioni 5 kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo; lakini hadi kufikia Januari, 2019 hakuna hata senti moja iliyokuwa imetolewa na hazina." Silinde



D8JDWUXWkAM8MJN.jpg
 
Yaani tunaon ndege,SGR na kugharamia chaguzi ndogo zinazotokana na watu kuunga mkono juhudi ndio muhimu kuliko haya mambo mengine yote!!!
 
Yaani tunaon ndege,SGR na kugharamia chaguzi ndogo zinazotokana na watu kuunga mkono juhudi ndio muhimu kuliko haya mambo mengine yote!!!
Tunakuunga mkono kwa hoja uliyoileta, tunatenga budget ya nini, kama uwezo wa kupeleka hizo pesa haziko.
 
Wenyewe CCM wanasema fedha za jiwe na kuzipata lazima unyenyekee na kupiga magoti mpaka yachubuke!!
 
Misitu ina kaa Dodoma miezi ikitusha vijembe na kula posho huku ikijadili bajeti hewa. Mwenye bajeti yake anangoja kufuja kodi zetu kwa kujitafutia sifa binafsi
 
Back
Top Bottom