Kama utani Manispaa ya Bukoba na watawala wameshindwa kujenga Stendi ya Mabasi

KASULI

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
599
669
Leo nimefatilia kwa karibu sana hotuba na ziara ya mh Rais Magufuli. Kati ya mambo niliyokuwa nayatarajia ni kuona Rais akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Stendi ya Mabasi Manispaa ya Bukoba.

Hili ni jambo la kushangaza sana Kuona mkoa ambao una historia Kubwa, mkoa umezungukwa na ziwa Victoria, mkoa ulioko mpakani na Nchi ya Uganda na Rwanda, kama haitoshi Pale pale Stend iliyopo Chafu isiyoendana na hadhi ya mkoa husika, watawala wanakusanya ushuru na tozo mbalimbali magari yanapotoka stendi. Wanashindwaje kupata angalau Bilioni 25 mpaka 30 ili kujenga Stand ya Mabasi ya Kisasa.

Stendi iliyopo ni finyu, mbaya na kutokana na majira ya mkoa wa Kagera (mvua nyingi) Stendi imejaa tope jekundu muda wote....

Hayaa Rais kaondoka zake hakuna Kipya, mkurugenzi yupo, madiwani wapo, mkuu wa mkoa yupo, Mbunge yupo....au hili nalo linasubiri agizo la Rais kama Ubungo ili kuwaamsha walio lala?

Ukitembelea Mikoa na wilaya nyingi za Tanzania kuna Stendi za kisasa, Mkoa wa Kagera na Wilaya Zake, hakuna wilaya yenye Stendi ya Kueleweka. Shida ni nini Sasa.. Yaani Singida na Katavi wameweza Kujenga Stendi Bukoba Wameshindwa?

Naomba Kuwasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza Magufuli hiyo Kagera haipendi kabisaa kama anavyoichukia kaskazini. Suala la stendi analijua na toka anaingia pesa zilikuwepo zimetengwa but zilirudishwa na kipindi hicho tulidhani kwa kuwa manispaa ipo chini ya upinzani (CHADEMA) ana uwezo wa kuaamuru pesa kiasi fulani zitengwe stendi ijengwe but Bukoba haipendi mpaka kufa kwake.
 
Kwanza Magufuli hiyo Kagera haipendi kabisaa kama anavyoichukia kaskazini.Suala la stendi analijua na toka anaingia pesa zilikuwepo zimetengwa but zilirudishwa na kipindi hicho tulidhani kwa kuwa manispaa ipo chini ya upinzani (chadema) ,ana uwezo wa kuaamuru pesa kiasi fulani zitengwe stendi ijengwe but Bukoba haipendi mpaka kufa kwake.
Siku hata mavi yakikubana .
Utamsingizia huyo mzee
 
Unataka wajenge kwa pesa kutoka wapi. Pesa zote za manisipaa zinaenda serikali kuu. Serikali kuu( magufui) ndyo inaamua pesa ziende wapi na sio bunge. Unategemeaje sasa bukoba wajengewe stend wakati walimzomea JPM?
 
Back
Top Bottom