Kama upo kwenye kundi hili wewe ni mnyonge

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Aug 28, 2020
2,204
2,083
Mnyonge ni mimi na wewe ambao haki zetu zinadhulumiwa kwa makusudi au bahati mbaya.

Mnyonge ni mimi na wewe tusio na konekisheni ya kupewa ajira serikalini.

Mnyonge ni mimi na wewe ambao hatuwezi kusoma elimu ya juu bila kupewa mkopo na serikali.

Mnyonge ni mimi na wewe ambao tunasoma elimu duni na kupewa huduma mbaya za kiafya.

Mnyonge ni mimi na wewe ambao tunaishi maisha ya hali ya chini katika jamii.

Katika biashara mnyonge ni mtu ambaye ananyonywa katika biashara na wafanya biashara wa tabaka la juu.

Mnyonge pia ni mtu ambaye kodi anazolipa zinaliwa na watu wa tabaka la juu.
 
Hitler kwenye nchi yake alikuwa hataki kitu kinachoonekana kinyonge, mfano watu wenye maumbile madogo alifyekelea mbali, ukipewa kazi ukashindwa ku-deliver ndani ya muda unapotea, sasa huyu jamaa angetawala hii nchi yangu ya wanyonge sidhani kama wangesalimika hata watu mia tano...
 
Wewe ni kilaza mkuu vitu ambavyo ni haki yako kuvipata eti unasema kupewa ivyo basi wewe ni mnyonge, mathalani mkopo wa elimu ya juu ni haki ya huyo apatae wewe unamuita mnyonge, eti huna connection mkuu fight utoke uko jalalani uliko uingie nuruni, safisha ubongo huo kwanza na utoe dhana ya unyonge ndani mwako.

Sasa kama uko ivo mkuu papuchi utachakata kweli au nazo unawasubiri hao wa kuitwa walio juu??
 
Mnyonge ni mtu yupo kwenye nchi yake alafu inamadini lakini mzungu ndo anaefaidika na ayo madini kisha anawaachia mishimo uyo ni mnyonge na zezeta
 
Pia mnyonge ni yule ambaye bei ya vifurushi ikipanda kutwa nzima analalamika!!
 
Tafsiri ya neno "Mnyonge"
kigogo_2014_%25F0%259F%2587%25B0%25F0%259F%2587%25AA_on_Instagram__%25E2%2580%259CMumeamukaje....jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom