Mackanackyyy
JF-Expert Member
- Mar 26, 2019
- 2,338
- 5,263
Magugumaji alikuja na akili zake za Maganda ya Korosho akijua zinalipa hapa mjini, Sasa yuko hoi bin taaban akifanya Kampeni siku 2 analala siku 5Habari za Mchana Wanajukwaa?
Kama kichwa cha habari kinavyoeleza hapo juu.
Kwa mwaka huu kampeni kwa vyama vya upinzani imekuwa rahisi kwa sababu ya MKULU kuzuia siasa tangu 2015.
Wanachofanya upinzani ni kuanika mambo mabaya ya Uongozi uliopo madarakani kisha kupendekeza njia za kutatua mambo hayo.
Kama siasa kwa upinzani ingelikuwepo tangu 2015 basi Upinzani ungelizungumzia mambo hayo kabla ya kampeni ya sasa hivyo viongozi wa chama kilichopo madarakani au viongozi wa serikali kupata nafasi ya kufafanua vizuri kwa wananchi (yaani kujibu hoja za upinzani) kama ilivyokuwa katika awamu zilizopita.
Kwa sasa Chama kilichopo madarakani kina shughuli kubwa ya kufanya kampeni muda huohuo kujibu hoja za Upinzani wakati mwingine inapelekea kujibu hoja vibaya au kwa kutowaridhisha wananchi kutokana na hali halisi ya mahudhirio ya wananchi kwenye mikutano,umuhimu wa hoja husika,muda,hali ya kweli ya maisha ya wananchi n.k.
PENDEKEZO LANGU
Napendekeza kwa Chama Chochote kitakachoshika Dola Nchini Tanzania (Nchi ya Vyama Vingi) kiruhusu Siasa wakati wote kwa ajili ya kujibu hoja mbalimbali za Upinzani.
Nawasilisha.