Kama unawaza namna hii sahau kufanikiwa

Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,563
3,708
Baadhi ya watu huwaza namna hii

“Nitafanya kazi kwa maarifa zaidi, lakini si kwa juhudi kubwa” ❌

Wengine huwaza namna hii

"Nitafanya kazi kwa juhudi kubwa"✔

Kiuhalisia nani atafanikiwa kirahisi!

Katika dunia hii ya mwendo kasi najua umesikia sana hadithi za fanya kazi kwa akili tu na maarifa na utafanikiwa hata kama usipoweka juhudi kwa nguvu sana, haya ni maneno ambayo yamekuwa yakisemwa sana.

Kuna wakati huwa nafikiri wenye mawazo hayo na kuanza kuyajadili na ambao wanatafuta hiyo ‘work smart not work hard’ hawa wanawaza nini. Inafika mahali ninakuwa naamini pengine watu hawa wanaota ndoto za mchana kweupe.

Kuna wakati unapaswa kujua kutafuta mafanikio kwa maarifa tu peke yake na kusahau kufanya kazi huo ni uvivu, tena mkubwa. Hiyo tukiwa na maana kwamba hatukatai maarifa ni muhimu lakini kazi ni lazima kazi iwekwe ili kutoa matokeo yanayoeleweka.

Ni wazi tu kusema kwamba kama umekuwa kila siku ukijidanganya kwamba mimi natumia akili na sitaki kufanya kazi sana, unajidanganya na tayari utakuwa umeshaingia kwenye kundi la kuanza kurudi nyuma kimafanikio.

Kubali kutumia maarifa kweli kwenye kazi zako, lakini hata hivyo usisahau kuchapa kazi. Kazi unatakiwa kuifanya haswa na hakuna mbadala wake, zaidi ya wewe kujituma na kufanya kazi kwa nguvu zote na kwa jinsi unavyojua.

Ongeza bidii katika kazi hakika utafanikiwa haijalishi elimu wala nafasi ukiingiza leo elfu mbili kesho jitaidi kuingiza elfu tatu.
 
Kazi ni nn? Ni fikira potofu kufikiria kuwa kufanya ni kutumia nguvu pekee, kuna kazi hazihitaji nguvu kufanyika bali ni maarifa na taarifa sahihi tu.
 
Back
Top Bottom