Kama unauza vifaa vya kielectronic jaribu hii njia kujiongezea wateja

Naja naja

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
688
1,000
Kama unauza vifaa vya ki electronic sana sana vifaa vya simu, kompyuta nk jaribu hii njia kujiongezea kipato.

Nunua vifaa vya ufundi kisha muajiri fundi aje kufanya kazi kwenye ofisi yako.

Tuchukulie labda kwenye ufundi simu maana ndo ufundi wenye hela sana, ongeza vifaa vya ufundi kwenye hiyo ofisi yako ambayo unauza vifaa vya simu kisha ingia makubaliano na fundi aje kufanya kazi kwenye ofisi yako, fundi kazi yake kubwa itakuwa kutengeneza tu hizo simu ila gharama za vifaa pamoja na kodi ya pango utalipa wewe.

Kila mteja atakaye kuja kutengenezewa simu 40% ya pesa iwe yako 60% iwe ya fundi kama itatokea ameharibu simu ya mteja kwa bahati mbaya 20% utamsaidia kulipa 80% atalipa yeye.

Njia hii kwa kiasi kikubwa itakusaidia kuongeza circle ya wateja kwenye ofisi yako ,maana mteja akishamaliza kutengeneza simu utamshawishi anunue pia na vitu vingine mfano chaja, makava ,protector nk ofisini kwako.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom