Kama unategemea ndoa kwa mwanaume kama huyu basi tafuta kiti ukae mko wengi

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,445
Kama uko kwenye mahusiano na mwanaume ambaye karibu kila siku anakuomba pesa, wala hata si pesa nyingi kihivyo kiasi cha kukufanya ushtuke unaibiwa. Hapana atakuomba elfu kumi, mara atakuambia umeme umesha, mara nimekwama hiki na nimekwama kile. Huyu hata ukimnyima hakasiriki sana lakini atajifanya kupoteza mood kutokana na tatizo alilokuombea pesa.

Kwa mfano, alikuambia “Nina shida ya elfu ishirini Mama anaumwa…” Basi kama ukimuambia huna anakua haongei vizuri na ukimuuliza kwanini hayuko sawa basi anakujibu “Hali ya Mama inanichanganya!” Mwingine analazimishia hata umpe lakini wengi ni wajanja, hawalazimishii, atapoteza furaha tu mpaka mwenyewe utajisikia viibaya, utajiona kama shetani kumnyima.

Kahela kenyewe kadogo tu elfu hamsini, sasa si ushamzoe, kwasababu mwanaume kama huyu anajua kuongea bwana, hatoi pesa ila anavyojali yaani mpaka nywele zinakusimama. Anapiga simu, anachat na wewe, akiwa online ukimtext anakujibu, anakujualia hali na anakudekeza kwa maneno. Sasa maneno yake mara nyingi yanaelekeza kuwaza ndoa, hakuambii moja kwa moja kua atakuoa lakini utasikia anasema; “Huuu mwaka lazima nioe, namiss tuwe sehemu moja, nikiwa na wewe nawaza kutengeneza maisha, inabidi nijipange nikikamilisha kitu flani, nioe.” Dada yangu najua kutokana na anavyokujali, hujawahi mfumania au ni kwa nadra sana na mara nyingi ukimfumania na vimeseji atakuambia wanawake wanamtaka tu yeya hawataki. Dada yangu kama una mwanaume ana tabia hizi basi huyo ni msanii balaa.

Nina uhakika, narudia najua hutaamini kwakua kwa namna anavyokuonyesha anajali, humshtukii basi unajiona wewe ila dada yangu huyo mtu anaigiza, nina uhakika kuna wanawake wengine si chini ya watano ambao anawafanyi hivyo hivyo, anawaomba vihela kwa zamu. Unaweza kumuona si muombaji sana ila yuko makini anaanza mmoja mmoja kisha anaendelea taratibu mpaka akirudi kwao ushasahau hata alikuomba.
 
Back
Top Bottom