Kama unataka kuondoka kwenye umasikini, waepuke masikini kama ukoma

Ambacho hujajua,
Matajiri mitaji wote wakubwa, mitaji yao Ni watu maskini.

Kuanzia wafanyakazi, bidhaa zao Hadi Bei wanazouza sokoni Ni kwa ajili ya watu maskini
Ndiyo maana hata mleta mada anauza kitabu cha wewe/sisi jinsi ya kutajirika
 
Nakubaliana nawewe 100% Suala la Utajiri linategemea na Mungu alivyokupangia Maisha yako yaweje.
Kuna watu wanaHustle litaa eg. MACHIMBON miaka pilikichi lakin mwingine anaaanza leo anapata Jiwe ananyanyuka kiuchumi vivo hivyo kwa Wakulima.
Wanalima kila mwaka lakin wakulima wachache sana wanaotoboa maisha.

Ila nimeona mdau anatupanga tununuwe kitabu chake Anasahau Mungu ndio kila kitu katk maisha.
Teh teh teh teh
Yeye anazijua tabia za kuwa tajiri, lakini anatuuzia kitabu. Kwanini asigawe bure ili na sisi tuzijue hizo tabia za kitajiri
 
Dah...

Utakuwa na stress za maisha wewe...

Wapo wengi waliouza vitabu vya ku-inspire watu lakini mpaka leo wanauza vitabu na bado watakufa wanauza vitabu kama wewe..

Una Phd au MD lakini huna HELA unakuja kuuza vitabu kwenye mitandao..

You're are looser trying to make while everything has already fallen apart...

Sisi hatutafuti HELA kwa kuwafundisha watu wengine kutafuta HELA, bali tunatafuta HELA kwa kuwachulua watu wengine hata kile kidogo walichonacho

Nashukuru kwa kutambua kuwa kila binadamu mwenye akili timamu uendelea kujitoa UJINGA mpaka anapotoka Ulimwenguni

Yeah mimini MJINGA anayeendele kujitoa UJINGA kila siku..


Nipo hapa Oysterbay na WAJINGA wenzangu tunasafisha koo zetu
Eti anatafuta pesa kwa kuwafundisha watu jinsi ya kupata pesa
 
Nikiwaambia muache kuuliza maswali ya kijinga mnakimbilia kupaniki.
Nimekupa maelekezo hapo, bado unalazimisha kile unataka wewe.
Ndiyo maana nasema pata pesa na maswali ya kijinga kama haya hutasumbua nayo watu.
Kila la kheri.
Mwanzoni nilikuona una maana kumbe hakuna kitu, swali rahisi sana lakini wewe unapanik, jibu Utajiri ni nini kwa mtazamo wako au ili mnunuzi wa kitabu ajue huo utajiri ni waaina gani
 
Habari za sijui kuutafuta utajiri utazisikia sanasana kwenye nchi maskini kama Bongo. Ila nchi zilizoendelea ukiachana na Marekani (Nasemea hasa hasa nchi za Ulaya), huwezi kusikia hizi swagga za kutafuta utajiri maana system ya nchi yenyewe ipo katika hali ya kuwafanya watu wote waishi maisha karibia sawa. Kitakachomtofautisha mwenye pesa nyingi sana na mtu mwingine ni kuhusu tu makazi. Kwamba mtu mwenye pesa nyingi ataishi kwenye nyumba inayojitegemea na mtu wa kawaida anaishi kwenye apartments. Ila mambo mengine wapo sawa tu maana hakuna gap kubwa kati ya maskini na tajiri.

Unakuta wote wanapata mahitaji yao kwenye supermarket moja. Siyo kama Bongo wanaonunua mahitaji Mliman city ni wenye pesa zaidi. Unakuta pia Ulaya huduma za afya ni sawa kwa watu wote siyo kama Bongo mwenye pesa anapata matibabu Agakhan na makabwela wanaenda Mwananyamala. Elimu nchi nyingi za Ulaya ni bure na baadhi unalipia pesa kidogo kwa chuo kikuu. Siyo kama Bongo mwenye pesa anapeleka watoto wake Internanational school makabwela wanapeleka watoto wao Shule ya msingi Buza. Mahakama zinatenda haki kwa watu wote, siyo kama Bongo mwenye pesa anaweza kununua haki na kabwela akafungwa hata kwa ushahidi wa uongo.

Unakuta pia hata anayefanya kazi ya usafi analipwa mshahara unaomtosha kulipa bills zote kwa mwezi na kubakisha chenchi. Yaani mfanya usafi anaweza kusafiri hata kwa ndege siyyo kama bongo ili usafiri kwa ndege mpaka uwe tajiri. Sasa nchi kama hizi mtu anatafuta utajiri wa kazi gani? Hizi stori zipo tu nchi maskini.

Kwa kuhitimisha, mie huwa naona watu wanaohimiza sana watu kuwa matajiri wanataka tuendelee kuwa na mfumo wa kutengeneza nchi ya wenye nacho na wasio nacho hivyo kuendelea kumkandamiza mtu maskini. Any way... Ngoja niishie hapa kwanza kwa sasa..
Uko na akili sana kuliko mleta mada
 
Mkuu kwanza mtoa mada hataki kuelezea nini maana ya utajiri kwa mujibu wake na kitabu..

Pengine utajiri anaokusudia yeye ni kuwa na uwezo wa kufikiri na wewe unagusia utajiri wa mapesa.

Pengine utajiri anaogusia mtoa mada ni uwezo wa kutongoza mademu wengi lakini wewe unagusia utajiri wa pesa nyingi.

Pengine utajiri anaokusudia mtoa mada ni kuwa na vitabu vingi vya kiswahili vilivyoandikwa na makirita amani kumbe wewe unakusudia utajiri wa mapesa mengi.
Achana naye, mleta mada ni kama dalali hakuna anachojua, umemuuliza maswali ya msingi kaishia kupaniki tu
 
Mkuu, mbona una mawazo mgando sana.
Unashindwa kuelewa mambo madogo hivi huo utajiri utauweza kweli?
Tumeshajadiliana na kumaliza lako, lakini bado una nyongo tu.
Get a life mkuu, utakufa siku siyo zako.
And by the way, Get Money, #NothingElseMatters
Hauko serious, wewe nakuona kama masikini ambaye unauza kitabu cha jinsi ya kuwa tajiri wakati wewe ni masikini. Pole mkuu
 
Mkuu mimi na wewe tumeshamalizana.

Huonekani kama mtu mstaarabu wa kupokea mawazo tofauti badala yake unakuwa mtu wa misimamo ya hasira na kuamini kila anayekuhoji analengo la kukukwamisha,
hizo ni mindset za kimasikini sana ambazo unatuonesha hapa.

Wewe mwenyewe unaonekana una uchungu na hasira ya pesa ndio maana hutaki kuhojiwa kuhusu kitabu.

Na wewe endelea kutafuta pesa utaacha kuwasumbua watu kuhusu kununua kitabu.

Matajiri akina modewji hawalazimishi watu kununua bidhaa zao kama unavyofanya wewe hapa.
Mkuu una busara sana, pia unajua ku control hisia/hasira zako.
 
Mwanzoni nilikuona una maana kumbe hakuna kitu, swali rahisi sana lakini wewe unapanik, jibu Utajiri ni nini kwa mtazamo wako au ili mnunuzi wa kitabu ajue huo utajiri ni waaina gani
Mkuu,
Maswali ya kijinga yanapaswa kujibiwa kijinga.
Na kama majibu yanakera, tatizo siyo majibu, tatizo ni huna pesa.
Hivyo badala ya kukomaza mshipa na majibu ya mtandaoni, invest your energy in making some money.
You will thank me later.
 
Hauko serious, wewe nakuona kama masikini ambaye unauza kitabu cha jinsi ya kuwa tajiri wakati wewe ni masikini. Pole mkuu
Mkuu,
Am just having fun selling my book to get money.
And am pretty aware people have deep rooted negative bias on anything about money.
Tell people you are poor and they will sympathise with you.
Tell them you want to get super rich and they will mock you.
So in this thread, i will go over the head and bust any kind of nonsense and BS people will reply here about money.
So take this as hardcore tough love and get angry to make money.
Because, it's all that matters.
Get your money right and am sure you will have no time posting nonsense in these kinds of thread.
That's what i wish i can help you here.
If you can’t get that then you are beyond help.
And if you are happy without money theb good for you.
I didn’t come to your house and force you to read this thread.
Hope you get it.
All the best.
 
Back
Top Bottom