Daby
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 33,648
- 75,732
Ni kweli ngeli ya a-wa unaongelea vitu vilivyo hai tu.Vitu hai huendana na ngeli ya "a-wa vitu visivyo na uhai ndiyo hutumia ngeli zingine jamaa naye kachemka kwenye kiswahili kidogo.
Lakini nikiri pia hili ni suala ambalo wataalamu wenyewe wa lugha wameshindwa kuafikiana nalo.
TUKI wao wanadai neno lipo kwenye ngeli ya I-ZI huku kamusi zingine hasa za wakenya wanasema lipo kwenye a-wa.
Kwangu naskia ukakasi mtu akisema.
Maiti amezikwa asubuhi ya leo.
Inayosikika vizuri kwangu ni Maiti imezikwa asubuhi ya leo.