Daby
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 33,648
- 75,732
Kwa upande wako utaweza kuwa upo sahihi....na kwangu nipo sahihi pia tena asilimia nyingi. Na sio kwamba sijui lugha.Kiswahili nacho haukiwezi. Maiti ni binadamu. Hauwezi kusema "Maiti itazikwa" unasema "Maiti atazikwa". Heshima ya binadamu akiwa hai inaendelea hata akiwa katika umauti. Hata kama maiti ni wengi (nasema wengi, siyo nyingi), utasema "Maiti watazikwa", siyo "Maiti zitazikwa". Oh, jamani siku wahenga tukiondoka, hizi lugha sijui itakuwaje. Kiswahili hamkijui, Kiingereza ndio basi kabisa. Kilugha ndio basi... Mmeachia Wasukuma tu.
Kuna wataalamu wanaweka maiti kwenye ngeli ya I-ZI.
Ambapo kwangu ni sahihi na nimechagua upande wao kwa maana hapa yanaingia majina yote yasiyo na viambishi vya wingi ila ndani yake kuna wingi.
Wengine kama ulivyosema wanaiweka kwenye ngeli ya A-WA.
Ila hii ngeli imejaa majina yenye uhai.
Kwangu inasikika vibaya saana mtu akisema maiti.
Maiti atazikwa??
Maiti amezikwa??
Maiti alizikwa?? Hapana siwezi kisema hivi.
Maiti tatu zimeopolewa. Nitachagua hii
Maiti wa/tatu wameopolewa hapana.