Kama unalipwa 750,000 au chini ya hapo na bado umeng'ang'ania ajira jitafakari

Huyo ni mfanyakazi wa wapi? maana kuna miji mingine ukilipwa hiyo ni fedha nyingi sana na mtu anajenga na kusomesha kiulaini kabisa.
Na unadai akiugua atakuwa mochwari kwa kuwa hana fedha za matibabu huku umeweka gharama za bima ya afya kwenye bills zake?
Huyu jamaa hajitambuai 750000 ni nyingi sana inategemea na eneo ulilopo lakini,
Uchague moja kushinda mtaani bila kazi au kuajiriwa kwa 750000/ kwa mwezi.

Lakini Tanzania hii kuna maeneo ukitangaza nafasi za vibarua kwa mwezi 100,000/

Idadi ya watakaojitokeza watazidi idadai ya wanaohitajika.

Nchi hii ina tatizo la ajira kuliko unavyofikiria.

Labda tusubiri viwanda vilivyoahidiwa vikijengwa tatizo la ajira linaweza kupungua.
 
huo mchanganuo kabla nilikuwa naogopa hadi kuuangalia ,,,daaa, hiyo pesa unaiona kubwa lakinj ikinyambulishwa utajiona mkosefu sana
 
Afu utakuta mwandishi wa hili bandiko hana ajira wala biashara inayomwingizia kipato hata cha 300,000 kwa mwezi.Sifa namba moja ya pesa ni "Scarcity" Siku zote hela haitoshi muhimu ni kuishi kulingana na kipato chako.Mjini kuna watu wanaishi kwa mshahara wa 150,000 na wana familia
 
Inategemea na maisha uliyochagua kuishi
Na wapi unaishi kuna maeneo kodi ya nyumba. 20,000/kwa mwezi yet kaweka100,000/

Kweli mkuu mimi ninapo ishi kodi nalipa 10,000/= kwa mwezi chamsingi mtu unatakiwa kuishi kulingana na kipato yale matumaini mliyokua mkijazana wakati wachuo inabidi muyaache muishi katika uhalisia nasio maisha ya kwenye tamthilia
 
Japo kuna ukweli fulani

Ila Kumbuka
Hizi nafasi unazosema watu waache, wengine wanazililia kuzitafuta hadi kuichukia serikali/private kwa kuotangaza nafasi za kazi.

ukiwa na kazi utaiona mbaya.....wengine wanatamani hata ya kujitolea.
 
Huyo ni mfanyakazi wa wapi? maana kuna miji mingine ukilipwa hiyo ni fedha nyingi sana na mtu anajenga na kusomesha kiulaini kabisa.
Na unadai akiugua atakuwa mochwari kwa kuwa hana fedha za matibabu huku umeweka gharama za bima ya afya kwenye bills zake?

unavyoumwa malaria unatibiwa bure unafikiri kila ugonjwa unatibiwa bure.

polee sana
unadegree unalipwa laki sita ni.kigezo kikubwa kuonyesha degree yako uliipata kwa mishe
 
Huyo ni mfanyakazi wa wapi? maana kuna miji mingine ukilipwa hiyo ni fedha nyingi sana na mtu anajenga na kusomesha kiulaini kabisa.
Na unadai akiugua atakuwa mochwari kwa kuwa hana fedha za matibabu huku umeweka gharama za bima ya afya kwenye bills zake?
Tuwe wakweli kwa mshahara wa 750000 kwa mtumishi mwenye familia ya watoto watatu na mke atakuwa masikini.
 
Wafanyakazi wengi wanaendesha maisha kwa kumdokolea muajiri hapa na pale. Embu mpe mfanyakazi mshahara huo, mathalani trafiki afu mwambie akae nyumbani miezi sita asiende 'site' uone kama hajafa njaa.
Kwani mkuu trafiki akienda " site" anapata hela?
 
Back
Top Bottom