Kama unalipwa 750,000 au chini ya hapo na bado umeng'ang'ania ajira jitafakari

NSSF 75,000
PAYE 90,650
BODI YA MIKOPO 112,500
CHAMA CHA WAFANYAKAZI 15,000
BIMA YA AFYA 37,500
Kodi ya nyumba 100,000
Maji 10,000
Umeme 15,000
King'amuzi 10,000
Nauli kazini 40,000
Vocha 10,000

Jumla = 515,650
Sasa 750,000 - 515,650 = 234,350

Hapo ukiweka chakula kwa mwezi ni sawa na ukichukua
234,350/31 = 7560 sasa hii ndo ule wewe na familia yako kwa siku....
HAPO UKIUGUAAAAA TUNAKUOKOTEA MOCHWARI MAANA HATA SENTI TANO YA AKIBA HAKUNA.....LAKINI TUWE NA SUBIRA LABDA MAMBO YATAKUA POA HAPO BAADAE.
Life is not such constant, kuna malupulupu, allowance, commission na mapochopocho kibao .Halafu vijana wa siku hizi wengi wao utakuta wana kisehem wamejiari kam Tigopesa kwa mfano tu
 
naona umekaa ukawaza tarehe salary hizi ukaamua uje na uzi wa uchochezi...
haa haa mkuu mi kazi siachi hata iwaje, maana hata ukisema ufanye biashara haimanishi kua huwezi fanya kazi, ila itaongeza njia za kupata kipato!!!
 
NSSF 75,000
PAYE 90,650
BODI YA MIKOPO 112,500
CHAMA CHA WAFANYAKAZI 15,000
BIMA YA AFYA 37,500
Kodi ya nyumba 100,000
Maji 10,000
Umeme 15,000
King'amuzi 10,000
Nauli kazini 40,000
Vocha 10,000

Jumla = 515,650
Sasa 750,000 - 515,650 = 234,350

Hapo ukiweka chakula kwa mwezi ni sawa na ukichukua
234,350/31 = 7560 sasa hii ndo ule wewe na familia yako kwa siku....
HAPO UKIUGUAAAAA TUNAKUOKOTEA MOCHWARI MAANA HATA SENTI TANO YA AKIBA HAKUNA.....LAKINI TUWE NA SUBIRA LABDA MAMBO YATAKUA POA HAPO BAADAE.
Mkuu wapo wa chini ya hapo na wanaishi .. hapo ndo utajua kuwa wabongo ni wa ajabu sana! Wizi mtupu .. wao wanaita dili.
 
kumbukeni tumeipenda wenyewe vp mbona mapema inamana hapo tu namba imesomeka mbona mapema sana ndio kwanza mwaka 1
 
Huyo ni mfanyakazi wa wapi? maana kuna miji mingine ukilipwa hiyo ni fedha nyingi sana na mtu anajenga na kusomesha kiulaini kabisa.
Na unadai akiugua atakuwa mochwari kwa kuwa hana fedha za matibabu huku umeweka gharama za bima ya afya kwenye bills zake?
Napenda analysis zako mkuu, naomba kuwa mgeni katika PM yako tafadhali!
 
Afu utakuta mwandishi wa hili bandiko hana ajira wala biashara inayomwingizia kipato hata cha 300,000 kwa mwezi.Sifa namba moja ya pesa ni "Scarcity" Siku zote hela haitoshi muhimu ni kuishi kulingana na kipato chako.Mjini kuna watu wanaishi kwa mshahara wa 150,000 na wana familia
 
Wote huo wengine tunabaki na negative Kabisa

Maisha ni mipango tu hata ulipwe sh ngapi haiwezi kutosha ni kuishi ndani ya kipato Chako na kuangalia other source of income unajiwekezea kidogo kidogo unapunguza ukali wa maisha
 
Unajua wafanyakazi wanaolipwa hiyo laki 7 unusu na chini ga hapo ni asilimia ngapi hapa tanzania. Ni watu zaidi ya laki moja. So unawashuri nini hawa watu 100000+ wakajiajiri?
 
Back
Top Bottom