Uchaguzi 2020 Kama unajisikia uchungu kwa ushindi wa CCM mwombe Mungu akuponye na hii hali

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Najua wapo wengi wanajiuliza mustakabali wa kisiasa katika miaka mitano ijayo na kubaki wakiumia tu. Wanaumia kutokana na ukweli kwamba, nafasi karibu zote za uwakilishi wa kisiasa, zimechukuliwa na CCM.

Imefika muda tukubali tu kuwa haya ni mapenzi ya Mungu.

Viongozi wa dini wengi wanakiunga mkono chama hiki. Wasanii wengi wanakiunga mkono chama hiki. Matajiri wengi wanakiunga mkono chama hiki.

Kina mama wengi wanakiunga mkono. Wasomi wengi wanakiunga mkono. Cha kushangaza zaidi wale maskini ndio wanaongoza kutoa dhihaka kwa wapinzani walioshindwa.

Nimebaki najiuliza hawa wapinzani ni nani? Ni watu wa aina gani? Wale wasomi wa tabia za binadamu niambieni, huenda kuna watu wamezaliwa wapinzani?Kama ndivyo tusaidieni maana kama upinzani ni tabia, basi naona kabisa si tabia nzuri. Haiwezekani hata Mungu awasuse.

Maana kupigwa ni wao, kuteswa ni wao, ikibidi kufa ni wao. Hii si ishara mbaya?

Kama kuna mtu ana elimu tafadhali,atuelimishe sie. Maana imeandikwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Mungu amewakataa watu wasio na maarifa. Kama ni dhambi kuwa mpinzani tuambieni,watu wengi hawapendi dhambi japo wanaitenda. Lakini ni vibaya sana kufanya kitu ukijua ni halali Kumbe si halali.

Au wasomi mmeshindwa pia kujua kwa nini kuna wapinzani?Au adui yetu "ujinga" bado ni tishio licha ya kuongezeka kwa vyuo vikuu?

Mwisho nitoe wito kuwa,inabidi tukubali kuwa Mungu amewapa kibali ccm. Pia nawaomba ccm, kuliko kuruhusu watu kuteswa, kupigwa mabomu, na hata risasi za moto kwa vile tu ni wapinzani, fanyeni jambo moja muhimu sana; Futeni sheria ya vyama vingi. Sasa mpo wengi bungeni hakuna mtu wa kuwazuia. Epusheni watu kuumizwa kwa kuwa wao ni wapinzani. Mungu atazidi kuwabariki
 
Najua wapo wengi wanajiuliza mustakabali wa kisiasa katika miaka mitano ijayo na kubaki wakiumia tu. Wanaumia kutokana na ukweli kwamba, nafasi karibu zote za uwakilishi wa kisiasa, zimechukuliwa na CCM...
Umemaliza vizuri sana hapo Mwisho na mimi naongezea pia wafute na stutus ya zanzibar kua kama nchi

zanzibar iwe tu kama mikoa ya Tanzania nafikiri itasaidia kumaliza yanayoendelea huko.
 
Mimi kwa kweli sijaumia I'm so happy kwa kweli, waacheni wapinzani wapumzike wamepata mateso Sana Hadi umaskini wa nchi hii 60 year's wao ndio waliuleta sasa tumebski chama kimoja lazima tuendelee kwa kasi ya 5G
 
Hata zamani tulifundishwa kuwa ile njia pana na yenye watu wengi ndiyo iendayo upotovuni, tofauti na ile njia nyembamba na yenye wateule wachache ndiyo iendayo uzimani..!!
 
Najua wapo wengi wanajiuliza mustakabali wa kisiasa katika miaka mitano ijayo na kubaki wakiumia tu. Wanaumia kutokana na ukweli kwamba, nafasi karibu zote za uwakilishi wa kisiasa, zimechukuliwa na CCM...
Mungu yupi kawapa kibali cha kuiba kura kuua watu Zanzibar? Hakuna uchaguzi Tanzania kilichofanyika ni CCM kuulawiti kuubaka uchaguzi kwa njia haramu za kishetani
 
Hata zamani tulifundishwa kuwa ile njia pana na yenye watu wengi ndiyo iendayo upotovuni, tofauti na ile njia nyembamba na yenye wateule wachache ndiyo iendayo uzimani..!!
Hakuna uchaguzi Tanzania kilichofanyika ni CCM kuulawiti kuubaka uchaguzi kwa njia haramu za kishetani
 
Tanzania eeeh, nchi yangu eeeeh

Tongo recordssss.

Nakwenda Zimbabwe, Zimbabwe.

Hivi Roma mkatoliki, tumeshafika Zimbabwe, au tumefika na kupitiliza, au bado?
 
Tanzania hakuna uchaguzi umefanyika bali ni vioja na maigizo kuihadaa Dunia tu
 
Najua wapo wengi wanajiuliza mustakabali wa kisiasa katika miaka mitano ijayo na kubaki wakiumia tu. Wanaumia kutokana na ukweli kwamba, nafasi karibu zote za uwakilishi wa kisiasa, zimechukuliwa na CCM.

Imefika muda tukubali tu kuwa haya ni mapenzi ya Mungu.

Viongozi wa dini wengi wanakiunga mkono chama hiki.Wasanii wengi wanakiunga mkono chama hiki. Matajiri wengi wanakiunga mkono chama hiki.

Kina mama wengi wanakiunga mkono. Wasomi wengi wanakiunga mkono. Cha kushangaza zaidi wale maskini ndio wanaongoza kutoa dhihaka kwa wapinzani walioshindwa.

Nimebaki najiuliza hawa wapinzani ni nani? Ni watu wa aina gani? Wale wasomi wa tabia za binadamu niambieni, huenda kuna watu wamezaliwa wapinzani?Kama ndivyo tusaidieni maana kama upinzani ni tabia, basi naona kabisa si tabia nzuri. Haiwezekani hata Mungu awasuse.

Maana kupigwa ni wao, kuteswa ni wao, ikibidi kufa ni wao. Hii si ishara mbaya?

Kama kuna mtu ana elimu tafadhali,atuelimishe sie.Maana imeandikwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Mungu amewakataa watu wasio na maarifa. Kama ni dhambi kuwa mpinzani tuambieni,watu wengi hawapendi dhambi japo wanaitenda. Lakini ni vibaya sana kufanya kitu ukijua ni halali Kumbe si halali.

Au wasomi mmeshindwa pia kujua kwa nini kuna wapinzani?Au adui yetu "ujinga" bado ni tishio licha ya kuongezeka kwa vyuo vikuu?

Mwisho nitoe wito kuwa,inabidi tukubali kuwa Mungu amewapa kibali ccm. Pia nawaomba ccm, kuliko kuruhusu watu kuteswa,kupigwa mabomu, na hata risasi za moto kwa vile tu ni wapinzani, fanyeni jambo moja muhimu sana; Futeni sheria ya vyama vingi. Sasa mpo wengi bungeni hakuna mtu wa kuwazuia. Epusheni watu kuumizwa kwa kuwa wao ni wapinzani. Mungu atazidi kuwabariki
Usimuhusishe Mungu kwenye haya mambo kabisa,huko ni kumkosea heshima sababu Mungu ni haki.Mungu hashiriki kwenye wizi na dhuluma na mambo yoyote machafu ya kuumiza watu.Kama unamzungumzia mungu wa gamboshi sawa utakuwa sahihi
 
Najua wapo wengi wanajiuliza mustakabali wa kisiasa katika miaka mitano ijayo na kubaki wakiumia tu. Wanaumia kutokana na ukweli kwamba, nafasi karibu zote za uwakilishi wa kisiasa, zimechukuliwa na CCM.

Imefika muda tukubali tu kuwa haya ni mapenzi ya Mungu.

Viongozi wa dini wengi wanakiunga mkono chama hiki.Wasanii wengi wanakiunga mkono chama hiki. Matajiri wengi wanakiunga mkono chama hiki.

Kina mama wengi wanakiunga mkono. Wasomi wengi wanakiunga mkono. Cha kushangaza zaidi wale maskini ndio wanaongoza kutoa dhihaka kwa wapinzani walioshindwa.

Nimebaki najiuliza hawa wapinzani ni nani? Ni watu wa aina gani? Wale wasomi wa tabia za binadamu niambieni, huenda kuna watu wamezaliwa wapinzani?Kama ndivyo tusaidieni maana kama upinzani ni tabia, basi naona kabisa si tabia nzuri. Haiwezekani hata Mungu awasuse.

Maana kupigwa ni wao, kuteswa ni wao, ikibidi kufa ni wao. Hii si ishara mbaya?

Kama kuna mtu ana elimu tafadhali,atuelimishe sie.Maana imeandikwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Mungu amewakataa watu wasio na maarifa. Kama ni dhambi kuwa mpinzani tuambieni,watu wengi hawapendi dhambi japo wanaitenda. Lakini ni vibaya sana kufanya kitu ukijua ni halali Kumbe si halali.

Au wasomi mmeshindwa pia kujua kwa nini kuna wapinzani?Au adui yetu "ujinga" bado ni tishio licha ya kuongezeka kwa vyuo vikuu?

Mwisho nitoe wito kuwa,inabidi tukubali kuwa Mungu amewapa kibali ccm. Pia nawaomba ccm, kuliko kuruhusu watu kuteswa,kupigwa mabomu, na hata risasi za moto kwa vile tu ni wapinzani, fanyeni jambo moja muhimu sana; Futeni sheria ya vyama vingi. Sasa mpo wengi bungeni hakuna mtu wa kuwazuia. Epusheni watu kuumizwa kwa kuwa wao ni wapinzani. Mungu atazidi kuwabariki
Utajiri wa dawa haudumu.
Utafanikiwa lakini utakuja kufa masikini.
Umasikini wako utaushuhudia kabla hujafa.
 
Back
Top Bottom