Kama unaipenda biashara yako hautausoma ujumbe huu nusu

Lazaro Samwel

Member
Apr 27, 2019
33
26
Sijui kama unajua kwamba kwa wakati huu unaweza kuwa na juhudi kubwa sana kwenye biashara yako ambayo umeanzisha na bado usifike sehemu yoyote?

Au kwa lugha nyingine tunaweza sema ukawepo sokoni lakini wateja wasikuone kupitia akili zao na mioyo yao.

Ndio huo ndio ukweli wenyewe na utanielewa kwanini nasema hivyo maana hi ni elimu muhimu sana.

Sasahivi katika biashara akili inatakiwa kutumika sana zaidi ya nguvu.

Achana na kufanya biashara kwa mifumo ya zamani ambapo hapakuwa na ushindani mkubwa sana na wafanyabiashara walikuwa wanafanya biashara kwa ku-relax.

Sasahivi wafanyabiashara ni wengi,mteja ana nafasi kubwa sana ya kuchagua wapi pa kununua na wapi asinunue.

Mteja kwa sasa ana nafasi kubwa sana ya kuangusha biashara yako tofauti na zamani kwasababu ya utandawazi ambao upo.

Ubaya ni kwamba “WAFANYABIASHARA WENGI KWA SASAHIVI WANA JUHUDI KUBWA SANA ZA KINGUVU KULIKO JUHUDI KUBWA ZA KIMAARIFA KATIKA KUFANYA BIASHARA ZAO.”

Ndio maana biashara nyingi kwa sasa hazifiki mbali,tatizo sio kwamba watu hawana hela watu wanahela lakini unachokifanya sokoni kimegusa sehemu moja kwa wateja tena kwa namna ya kizamani wakati nyakati zimebadilika kabisaa.

Katika makala zangu za mwaka jana mwanzoni kabisaa nilisema kwamba “Kwa sasa sio kwamba watu hawana hela,watu wana hela lakini umekini wa kutumia hela/fedha zao umekuwa mkubwa sana tofauti na zamani na ili uweze kuzitoa hela za watu mifukoni mwao hauitaji tena kuwagusa kihisia tuu,sasahivi lazima uguse mioyo yao na akili zako kwa namna wanavyofikiri.”

Tofauti na hapo ndugu yangu lazima utaendelea kulalamika watu hawana hela.

Huo ndio ukweli na hata wewe mwenyewe ni shuhuda katika matumizi ya hela zako kwamba hautumii hela tena kihisia tuu,kwa sasa najua unakuwa makini sana katika kununua chochote kwa kukiweka kwenye mizaji ya maisha yako ya leo na kesho.

Kuna mwanafunzi wangu mmoja kwenye PRIVATE MASTERCLASS aliniuliza “Mwalimu kwanini unakazania wafanyabiashara kutumia mitandao ya kijamii?” nilimwambia “Siwalazimishi lakini soko ndivyo ambavyo linataka wafanyabiashara kufanya.”

Yaani kwa lugha nyingine ni kwamba “Kwa mfanyabiashara yoyote yule mitandao ya kijamii sio tena option kujifunza kuitumia,kwa sasa upende usipende mitandao ya kijamii ni muhimu sana na kama utaiona sio muhimu basi endelea kujipa muda kwa biashara ambayo unaifanya uone itakuaje.”

Kumbuka haupo pekee yako na kwa sasa SIMU zimekamata hatamu,nilikuwa naangalia twakimu za instagram zinaonesha kwamba mtu wa kawaida kabisa anayetumia mtandao wa Instagram anatumia dak 30 kwa siku kuutumia mtandao wa instagram.

Na kila siku lazima ukumbuke mitandao ya kijamii kwa wengine ambao wanaweza kuwa wateja wako imekuwa chakula chao kingine katika maisha yao.

Bado nikaanbalia twakimu nyingine ambayo ilisema 81% ya watumiaji wa mtandao wa instagram wanatumia mtandao wa instagram kwaajili ya kuangalia bidhaa za kununua.

Na siku zinavyozidi kwenda mtandao wa instagram naimani utakuwa na mfumo ambao mtu anaweza fanya transaction ya huduma au bidhaa moja kwa moja.

Wewe mwenzangu ambaye unapiuzia mitandao ya kijamii sijui utakuwa wapi.

Na hata ukiangalia kwa sasahivi biashara nyingi ambazo zinafanya vibaya nyingi ni ambazo bado zinangangania mifumo ya kizamani kutafuta masoko na kuuza bidhaa zao.

Kama ni mmoja wapo nakuomba sana kwa mwaka huu hakikisha kwenye ratiba yako kujifunza namna ya kutumia mitandao ya kijamii kibiashara ni moja ya malengo yako.

Jisajili katika madarasa yetu sasa kuweza kuhakikisha mwanzo huu wa mwaka unakuwa vizuri katika mitandao yako ya kijamii.

Piga ; +255678010334

Lazaro Samwel
Author | Sales And Marketing Expert | Profesaional Copywriter
#akiliyaushindi
 
Hua nashangaaga sana mtu kusomea sales and marketing, halafu akashindwa kuuza like mtoa mada. Mkuu umei 'pack' wrongly bidhaa yako ni ngum sn kuiuza!.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom