Kama unahitaji mtu wa kufanya naye kazi nipo hapa

Rebuke

Senior Member
Feb 20, 2018
167
48
Habari zenu wakuu,

Mimi ni mkazi wa dar nimemaliza form six, pia nipo vizuri kwenye computer basic (word and exel) pia ni dereva mzuri wa gari na pikipiki nina leseni class A B na D, na pia nina cheti cha JKT, ninatafuta kazi ya either ya ulinzi.

Delivery kwa gari/pikipiki, kumuendesha mtu na kazi nyingine yoyote unayoona inaweza ikasaidia kuniingizia kipato, nipo dar maeneo ya Makumbusho, msaada wako ni muhimu mkuu, nipo tayari kufanya kazi mda wote yaani kama ni usiku/mchana.
 
Mimi ni muumini ya kujiajiri kuliko kuajiriwa.

Jaribu kutafuta kazi ya dobi. Unakusanya nguo, dobi ana fua kisha una deliver.

Tatuta goli maarufu la chips kama American Chips Kinondoni etc ingia nao makubaliano uwe una deliver chakula majumbani kwa wateja.

Pikipiki inafanya shughuli zote tajwa hapo.

Pitia :

Laundryapp au deliveroo kwa idea.
 
Habari zenu wakuu, mimi ni mkazi wa dar nimemaliza form six, pia nipo vizuri kwenye computer basic (word and exel) pia ni dereva mzuri wa gari na pikipiki nina leseni class A B na D, na pia nina cheti cha jkt, ninatafuta kazi ya either ya ulinzi, delivery kwa gari/pikipiki, kumuendesha mtu na kazi nyingine yoyote unayoona inaweza ikasaidia kuniingizia kipato, nipo dar maeneo ya Makumbusho, msaada wako ni muhimu mkuu, nipo tayari kufanya kazi mda wote yaani kama ni usiku/mchana.
Kama una urefu at least 5.7ft nenda KK Security, ila kuwa mvumilivu na fuata masharti yao
 
Kama una urefu at least 5.7ft nenda KK Security, ila kuwa mvumilivu na fuata masharti yao
Hivi KK mshahara unaenda ngapi mkuu?? Taratibu zao zimekaaje mkuu?? Halfu nasikia kama kampuni yao imenunuliwa na wazungu kwa hiyo hata mishahara inaweza ongezeka
 
Hivi KK mshahara unaenda ngapi mkuu?? Taratibu zao zimekaaje mkuu?? Halfu nasikia kama kampuni yao imenunuliwa na wazungu kwa hiyo hata mishahara inaweza ongezeka
Yaani ww unawaza mshahara kiasi kwamba unaweza kupata kazi ukaishia kulalamika tu
 
Usiwe sana Mshahara-Oriented Mkuu maana hutafanya kazi kwa amani, maana utakuwa mtu wa kulalamika kila siku
Ni kweli kabisa ishu ni kupata kazi kwanza , baada ya hapo ndo mambo mengine yanakuja
 
Nimejaribu kwenda sema wamesitisha kuajiri mkuu
Fuatilia kwa karibu, wakifungua tu nenda, tena unaweza kupata Udereva kabisa wakihitaji. Uzuri wa KK malindo yao siyo ya kitoto unaweza kupelekwa sehemu ukajenga NETWORK, CONNECTION ukapata na kazi nyingine kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom