Kama unaamini uwepo wa Mungu, usiipite hii!

Unataka ajifunue ubongo alafu afe au unamanisha akili gani
ndiyo atueleze sasa...hata nabii Mussa alipewa uwezo wa kuongea na Mungu haikutosha akataka amuone Mungu live,ombi lake lilikubaliwa lakini kilichomtokea kabla ya kumuona Mungu ile nuru yake tu hakutamani tena kutaka kumuona
 
Mnaanzaga na logic lakini mkiulizwa logic mnaleta porojo.

Huyo muhusika nikikukuuliza kaundwa na nani utajibu Mungu, na nikikuuliza huyo Mungu kaundwa na nani.. utaniletea ngonjera za biblia sijui Quran.
Mungu Ni energy never created no destroyed, tatzo din zmetufunga ili tuwe wapumbavu et Mungu yupo mbinguni kwenye kiti Cha enzi , dah Mungu hayupo limited hivyo ndo maana akili ya kawaida inakataa maswal ya dini uongo mwingi unapoteza ukwel, Mungu Ni energy , ambayo pia inaoperate ndan yako
 
Mpumbavu husema moyoni mwake kuwa hakuna MUNGU.

" Eeeh Mungu uliyetuumba sote tunaomba msamaha kwa uchafu, maovu na machukizo mengi tukutendayo.

Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake si nyingi lakini Ibilisi amepitisha maovu yake kwetu kila siku tunajinasibu na kujilisha upepo eti Mungu haupo wakati kila mtu anajua upo. Tukiwa hai kwa pumzi hii unayotujalia tunajiona tunayaweza yote. Nimewahi simuliwa juu ya binadamu wenzetu flani wakati wanakaribia kuumaliza mwendo walianza kuona moto na hali ya kutisha huku wakipiga kelele kabla ya Umauti kuwasibu, hayo yote na mifano mingineyo inatosha kutufanya tujue kuna maisha ya heri au shari baada ya vifo vyetu."

Tangu enzi na enzi pasipo kujalisha unaamini kwa njia ipi lakini jamii zote duniani walikuwa wanaamini kuwa yupo Mungu ambaye ndie mkuu na aliyeumba vyote.
Kuna watu siku hizi wanaojiita wasomi wa mawazo ya binadamu wenzao wanaokuja kuhadaa wengine waamini ujinga na nadharia ziangamiazo nafasi zao huko mbeleni.
Binafsi ninajua jana na sasa yangu ila baadae yangu siijui yeye aliyenipa pumzi hii aweza ichukua muda wowote, hivyo hakika mimi na nyumba yangu tunamuamini Mungu yupo na amekuwa akitusaidia katika maisha yetu yote.

Eeh Mungu utujalie mwisho mwema na tusipate kibri cha uzima tukakuasi na kukukana mbele za watu.
"Watu wote tuseme AMINA."
 
Huwezi kuelewa wala kuamini uwepo wa Mungu mpaka yeye mwenyewe aamue kukuelewesha. Kwa akili zako huwezi. Ukizitumia akili zako utaishia kusema hayupo. Ila ukitaka kumwona Mungu, chukua biblia anza kusoma, soma kuanzia mwanzo mpaka mwisho non stop. Baada ya wiki uje hapa tena.
 
Kama kweli unaamini uchawi tupe chanzo chake maana mimi siamini uwepo wake.

Ukiweza kunifundisha mm nitamkana Mungu leo
 
Hivi wewe mkuu kungekuwa na mungu au kuna kwenda mbinguni unadhani wazungu wangegawa biblia bure au waarabu wangegawa hizo qurani bure au unadhani wanakupenda sana. Kwanini wasitafsiri vitabu vya kemia bailogia na jiographia wao wakakutafsiria biblia mpaka ya kabila lako? Hukiulizi ni mchezo huo wa kukutawala fikra zako. Wewe ndio umesoma alafu hukaelimika mzungu akupe kitu bure toka lini au mwarabu
Kabla ya wazungu, mababu zetu waliabudu, wapo walioabudu Miti, jua, bahari n.k.

Huko kote ni kutafuta mungu,

So suala sio mungu yupo au hayupo, suala lako ni mungu yupi ndo wakweli.

Hilo suala n mjadala mrefu, Ila believe me mungu yupo, just use your imagination and thing of how perfect the life is. There must be a mighty to make everything this perfect.
 
Elezea kidogo kwanini unaamini uchawi upo, binafsi uchawi ni matokeo ya uwezo mdogo wa hasa sisi wenye ngozi nyeusi katika kuchanganua changamoto mbalimbali tunazokutana nazo, mf umaskini, magonjwa, nk. Kwa aina ya mada uliyoleta na kusema unaamini uchawi nakushangaa
 
Hata wale atheist wasio amini kwamba kuna Mungu kimsingi wanaamini kwamba kuna supernatural being ambayo kimsingi ndo huyo huyo Mungu sema wamegoma tu kumacknowldge...sasa sembuse itakua huyu mleta mada...😂😂😂😂 asiejitambua...🤣🤣🤣🤣
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom