Kama una tabia hizi 10, huwezi kamwe kufanikiwa kwenye maisha

Mafanikio ni dhana pana sana kila mmoja anaweza kuyatafsiri mafanikio kwa namna yake tofauti na mwingine.

Labda umekusudia utajiri wa mali, ila nao unanjia tofauti tofauti.
Wapo waliotumia kanuni hizo na mpaka leo hawajafanikiwa kupata wanachotaka pia wapo wengi wamefanikiwa na hawakutumia kanuni hata moja kati ya kumi ulizo zitaja.

Mafanikio ya kupata mali huwa yana siri ndani yake, wakati mwingine hata huyo aliyenayo huwa hajui ni nini hasa siri ya mafanikio yake kajikuta tu kafanikiwa hata jambo lililomfikisha ktk kufanikiwa si jambo tarajiwa kwake wala kwa mwingine kama ataamua kulifanya.
Baadhi yao wanajua siri ya mafanikio yao ila si wawazi juu ya nini kilifanya wafanikiwe zaidi ya kuelezea mambo ambayo watu wengi tu wanafanya na hawajafanikiwa.
 
Kwel mkuu.Niko najifunza sana sales kwa sasa.Nimeesoma Computer science but for now sales naiona ni kitu muhim sana kwangu.Naomba ukiambatanishe hicho kitambu plz
Nimeshaambatanisha kwenye comments za juu, pitia zote utaona.
Hongera kwa kuchukua hatua hiyo, itakuwa na matunda mazuri sana kwako.
 
Dr Makirita vitabu vyako vipo kwa Hardcopy?
VITABU VILIVYOANDIKWA NA KOCHA DR. MAKIRITA AMANI.

Hapa ni orodha ya vitabu vyote vilivyoandika na Kocha Dr Makirita Amani na jinsi unavyoweza kuvipata.

VITABU VILIVYOCHAPWA (Hardcopy);

Vitabu ambavyo vimechapwa na vipo kwenye mfumo wa nakala ngumu ni kama ifuatavyo;

1. ELIMU YA MSINGI YA FEDHA (BASIC FINANCIAL EDUCATION); Maarifa Sahihi Ya Kifedha Yatakayokufikisha Kwenye Utajiri Na Uhuru Wa Kifedha. – Tsh 20,000/=

2. BIASHARA NDANI YA AJIRA; Mwongozo Wa Kuanzisha Na Kukuza Biashara Yako Ukiwa Kwenye Ajira (Toleo la Pili). – Tsh 20,000/=

3. TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA; Siri 50 Za Mafanikio, Uchambuzi Wa Vitabu 50 , Makala 50 Bora Za Mafanikio, Maarifa Ya Kifedha Na Tafakari 50 Za Kufikirisha. – Tsh 50,000/=

4. ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA; Jinsi Ya Kuanza Na Kukuza Biashara Yenye Mafanikio Makubwa. – Tsh 20,000/=

5. UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA; Tambua Uwezo Mkubwa Wa Akili Na Mwili Wako Na Jinsi Ya Kuutumia Kutenda Miujiza. – Tsh 20,000/=

6. EPUKA UTUMWA KIDIJITALI; Jinsi teknolojia mpya zinavyokufanya mtumwa na njia za kuondoka kwenye utumwa huo. – Tsh 20,000/=

Kupata vitabu hivi, wasiliana na kitengo cha mauzo kwa namba 0752 977 170 na utapewa maelekezo ya kuvipata kwa popote ulipo.

VITABU NAKALA TETE (Softcopy).

Hivi ni vitabu ambavyo vipo kwa mfumo wa nakala tete na unaweza kusomea kwenye simu au tablet yako. Vitabu vilivyo kwenye mfumo huu ni kama ifuatavyo;

1. KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI; Sababu Ishirini Na Tano Zinazokuzuia Wewe Kuwa Tajiri. - Tsh 5,000/=

2. JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA; Maandalizi, Na Njia Bora Ya Kunufaika Na Mabadiliko Kwenye Maisha, Kazi Na Biashara. - Tsh 5,000/=

3. JINSI YA KUTENGENEZA PESA KWA BLOG; Jiajiri Na Utajirike Kupitia Mtandao Wa Internet. - Tsh 10,000/=

4. KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO; Nidhamu, Uadilifu Na Kujituma. - Tsh 10,000/=

5. MIMI NI MSHINDI; Misingi Ya Kuishi Maisha Ya Ushindi Na Mafanikio Makubwa. - Tsh 10,000/=

6. BIASHARA NDANI YA AJIRA; Anzisha Na Kuza Biashara Yako Ukiwa Bado Umeajiriwa (Toleo la Kwanza). - Tsh 10,000/=

7. IJUE BIASHARA YA MTANDAO (NETWORK MARKETING); Miliki Biashara Kubwa Kwa Kuanza Na Mtaji Kidogo. - Tsh 5,000/=

8. PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU; Una Muda Wa Kutosha Kufanya Chochote Unachotaka Kufanya Kwenye Maisha Yako. - Tsh 5,000/=

9. TABIA ZA KITAJIRI; Tabia za kuishi kwenye kila siku yako ili kufika kwenye utajiri na mafanikio makubwa. - Tsh 10,000/=

Vitabu hivi vya nakala tete vinatumwa kwa email. Tuma fedha kwenda namba 0717 396 253/0755 953 87 kisha tuma ujumbe wenye vitabu ulivyolipia na email yako kisha utatumiwa.
Karibu sana.
 
Moja ya njia ambayo mtu yeyote anaweza kuitumia kutoka chini na kufanikiwa sana ni mauzo (sales).
Kama huna pa kuanzia kabisa, basi tafuta chochote na kiuze.
Jenga ushawishi na uza kama kichaa.
Mkuu kamwe usimdharau salesman yeyote yule, unaweza kuona anauza kitu cha kijinga, lakini akawa anapata kamisheni nzuri kuliko mshahara wa mtu anayekaa ofisini.
Japo unaweza kuwabeza na kuwacheka wanaouza vitu unavyoona siyo vya hadhi yako, jua kuna thamani wanatoa na kuna kitu wanaingiza.
Jifunze sales mkuu, soma kitabu cha Brian Tracy cha psychology of selling na kamwe hutokaa umbeze anayeuza chochote, huku kikikusaidia kupiga hatua.
Nakuambatanishia kitabu hapa kama utajali na ukisome.
Asante.
Ambatanisha mkuu
 
Umeongea vema Sana..kaka mungu azid kukubariki..nlikuwa natafakari..mnoo juu hiz comments za watu..nikaelewa mnoo..kwa Nini Hadi Leo tumeshindwa kutengeneza gari.
Ukisoma comments za huu Uzi ndio utajua IQ ya watanzania kwanini iko chini sana.

Kama mtu anashindwa ku-logic na kuwa analytical kwa hizo hoja kumi (10) anaenda kuhoji utajiri wa mleta mada na kuuza vitabu !!! Basi sishangai tunapata Viongozi wanaenda kujenga international airport Chato.


Ili uamini IQ ya watanzania Ni ndogo nimechukua huu Uzi nikamtupia rafik yangu mkoja mkenya Feedback ambazo kanipa ni tofauti na yanayoandikwa humu.


Watanzania tutahidi kuwa analytical. Simaaninishi ni lazima ukabaliane na Uzi ila kuwa na critics zilizojiegemeza kwenye hoja na sio mtu. Kuelekeza critics kwa mtu badala ya hoja hizo 10 ni moja ya dalili uwezo wetu wa kujenga hoja ni mdogo.

Haya ndio Mambo hata kwenye interview allkisimama mtanzania na mkenya tunaishia kuduwaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom