[/hatareeh]Okay, kumbe unaielewa hali yako!
Karibu..
Niliwahi kusikia kuwa maji na mafuta havichangamani, na pia mafuta huwa yanaelea juu ya maji... Basi jana mimi nikaamua kupaka mafuta mengi tu miguuni kisha nikaingia baharini ili niweze kutembea juu ya maji maana nilihisi ningeelea na kuweza kufanya chochote.
Sikumbuki nini kilitokea lakini nilijikuta nimelala mchangani watu wakiwa wamenizunguka huku wakisema niwashukuru sana wavuvi. Nadhani watakuwa wamenipa samaki wa bure.
Daaah nimecheka sanaKama utakipenda kimoja njoo PM tuzungumze biashara
1. Freezer aina ya Boss Tsh250000. Haina mlango wa mtungi wa gesi
.
2. Feni ya chini Tsh 15000/=. Inawaka kwa machale.. yaeza kukaa hadi masaa 2 haijaanza kuzunguka
,
3. Pasi ya umeme aina ya Phillips. Tsh 12000/=, haishiki moto kabisa hata ikae nusu saa kwny umeme na kidude cha kuregulate moto kimeharbika..
4. Meza ya plastic Tsh 75000/= ina miguu 3 na mmoja mfupi kidg.
5. Vikombe vya udongo Dozen 1 Tsh 25000/= ila vilipata ajali kidg.. vimekatika mikono na vingne vimetoboka chini
6.Redio ya caset lkini haina transiforma bei 34000
7.Flat scren bei 50000 kioo kimepasuka na haina rimot control na batan zime haribika fasta nichek
8.Simu aina ya Sumsung s7 edge 470000/= ilidondokea kwenye maji ikapiga shot, kitufe cha kuwashia hakipo na hata ukiweka kingine haiwaki, ni simu nzuri bora na ya kisasa!
9.Kamera aina ya sony mp 16 bei 62500/= haina lens, ni mbovu hata mafundi hawaitaki kama spea.
10.Bajaji aina ya tvs, bei 1400000/= haina matairi, viti wala usukani! Imetumika miaka 8 na inadaiwa kodi ya miaka 2!
Karibuni, bidhaa ni nyingi sana, zipo za aina tofauti tofauti kama magari, ndege, treni, meli, maparashuti, vifaru, n.k vyote hivyo vikiwa katika hali mbaya sana, (ikumbukwe hizi ni toys za watoto zilizotumika huko uswahilini na kutupwa kwenye majalala)
noma sn hii..!!KESI YA MIRATHI ILIYOMALIZIKA HARAKA.
Kesi ya Mirathi ilipelekwa Mahakama ya Mwanzo huko Tanga.
Kijana wa miaka 20 alikuwa anataka kupewa mgao wake wa mali za marehemu baba yake.
Ni kweli alikuwa na mgao wake, ila mjane wa marehemu, ambaye ni mama yake mzazi, alikuwa anamuona bado mdogo kuweza kumiliki mali nyingi kiasi kile.
Marehemu alikuwa ameacha magari na nyumba kadhaa.
Basi yule kijana baada ya kuona mama yake hataki kumpa mgao wake akafungua kesi Mahakamani.
Kufika mahakamani Hakimu akamuuliza yule kijana:
"Unamtambua huyu Mwanamke?"
Kijana Akajibu: "Ndiyo. Ni Mama yangu Mzazi."
Na mama akaulizwa, "Unamtambua Huyu Kijana?"
Mama akajibu,: "Ndio ni Mwanangu wa Kumzaa."
Hakimu akamuuliza yule Kijana: "Kijana, Eleza Mahakama Madai Yako ni Yepi?"
Kijana akajibu: "Madai yangu nina taka nikabidhiwe mgao wangu wa mali za marehemu baba. Ila Mama nimemwambia amegoma kunipa."
Mama akaulizwa na Hakimu: "Unasemaje Kuhusu Haya Madai ya huyu Kijana!?"
Mama akajibu: "Huyu ni Mwanangu wa Kumzaa, ila Sikumzaa na Huyo Aliyeacha Hizo Mali."
Kesi ikaishia hapo hapo...Kina Mama wakiamua wanaweza
Hatariijana nmetoka kuangalia movie ya kivita,na mm nkajiona kama nmeshakua stering vle..nkachkua mwiko nkatokea nao barabaran nkasimamisha difenda la FFU nkawauliza mnatoka wapi na mnaenda wap?
Hadi sasa hivi nupo kitandan napewa matibabu, @@@AKILI YANGU NAIJUA MWENYEWE!!!!...
Mkuu umesema watu wenye stress tupitie hapa
🤣🤣🤣1. Leo kidogo nipigwe na mwanamke baada ya lifti kusimama, wakati tupo kwenye lifti Nilikua nayaangalia maziwa yake akasema "Bonyeza moja" mimi si nikalibonyeza yaani hadi sasa bado najiuuliza nilipokosea?
Ha ha .Jirani yetu aliponunua gari wife alinilazimsha nami ninunue basi nikajibana nikanunua baada ya muda jirani yetu akaongeza nyumba kwani alikuwa na uwanja mpana kama wetu basi hilo nalo likawa kero mpaka nasi tukaongeza jengo sijakaa sawa jirani akamuhamishia mtoto wake shule ya feza hilo nalo lilisumbua sana mpaka nikanyoosha mikono kijana wetu nikamuhamishia feza wife akasisitiza huo ndio uanamume kuiga mambo mazuri na jirani yetu ni mfano wa kuigwa sasa jana jirani kaongeza mke wa pili wife alikuwa amekwenda safari ndo namsubiri.
Ulikosea ungepaka ka pipa moja la grease!! sasa wewe unapaka ya mgando kawaida??Okay, kumbe unaielewa hali yako!
Karibu..
Niliwahi kusikia kuwa maji na mafuta havichangamani, na pia mafuta huwa yanaelea juu ya maji... Basi jana mimi nikaamua kupaka mafuta mengi tu miguuni kisha nikaingia baharini ili niweze kutembea juu ya maji maana nilihisi ningeelea na kuweza kufanya chochote.
Sikumbuki nini kilitokea lakini nilijikuta nimelala mchangani watu wakiwa wamenizunguka huku wakisema niwashukuru sana wavuvi. Nadhani watakuwa wamenipa samaki wa bure.