Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

IMG_20190620_071206_595.jpeg
 
Hahaha
HAHAHAHAHAAAAAA DUH

Ndege ilipata hitilafu angani Ndipo rubani akatoa taarifa kwamba ndege imepata hitilafu na itadondoka baada ya dakika 10. Ndani ya ndege kulikuwa na watu watano Lakini maparashuti yalikuwa manne tu.

Watu hao ni mchungaji, waziri, mwanajeshi, Msukuma na mwanafunzi wa chekechea, Mchungaji akasema yeye anategemewa na kanisa hivyo hapaswi kufa. Akachukua parachute akaruka. Waziri akasema wananchi wanamtegemea alete maendeleo, Akachukua parachute akaruka. Msukuma akasema familia inamtegamea akachukua parachute akaruka faster.

Wakabaki mwanajeshi na mwanafunzi wa chekechea. Yule mjeshi akamtazama mwanafunzi akamuonea huruma kisha akasema. Mimi najitolea kufa kwa ajili yako, we chukua hilo parachute lililobaki ujiokoe halafu mi ntakufa na hii ndege.

Yule mwanafunzi akajibu "usijali yamebaki maparashuti mawili" yule mjeshi akashangaa akauliza mawili kivipi.? Mwanafunzi akasema YULE MSUKUMA KACHUKUA BEGI LANGU LA SHULE ALIDHANI NI PARASHUTI.
 
Harusi za Marekani
Walioalikwa :100
Wanaohudhuria kanisani :80
Wanaohudhuria ukumbini :70
Wanaotoa Zawadi:65
Vitu vilivyopotea : 0
Harusi za Uingereza
Walioalikwa :50
Wanaohudhuria kanisani :50
Wanaohudhuria ukumbini :40
Wanaotoa Zawadi:40
Vitu vilivyopotea : 0
Tanzania sasa
Walioalikwa :500
Wanaohudhuria kanisani :38
Wanaohudhuria ukumbini :1300
Wanaotoa Zawadi:70
Vitu vilivyopotea : simu 20,vijiko 300,visu vya kukatia keki 15, camera 1,chupa 2 Za wine, mdada kutongozwa na kudate na Mgeni mmoja wapo, wavulana kutafuta demu mpya, zawadi kuibwa, viti vilivyovunjika 50,meza zilizovunjika 5,watu kuondoka na mapambo, wamama kuondoka na misosi na nyama kwenye mikoba sijui huwa tunakwama wapi.

noma sana
 
Rafiki yangu alikuwa
amesinzia tukiwa darasani,
nikachukua simu yake
nikabadilisha alivyosave
namba yangu nikasave "lovely
dad" (ndivyo alivyokuwa
amesave jina la baba yake
mzazi)
Nikamtumia SMS "mwanangu
nimeshinda millioni 100 toka
BIKO, na sasa hivi tutakuwa
na maisha mazuri. Acha
shule njoo tupange tutafanya
biashara gani"
Rafiki yangu baada ya
kusoma sms akanyanyuka na
kukusanya kila kilicho chake
akaanza kuondoka.
Alipofika mlangoni mwalimu
akamuuliza unaenda wapi
bila kuomba ruhusa?
Akageuka akamwonyesha
mwalimu kidole cha kati,
akaachia mfyonzo mkali kisha
akasepa.
Sasa hivi ananisaka kinyama,
nani anajua sehemu nzuri ya
kujifichia
 
317 Reactions
Reply
Back
Top Bottom