Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Umeongea point ndg tena naumia sana.nakujibu kama ifuatavyo masikini tunaroho mbaya sana ukimuachia hiyo pesa badala yakushukuru ataenda kwasangoma akushushe kupitia pesa yako ndio maana matajiri wanajitenga na masikini.
Kuna dada mmoja akiwa katika gari lake njiani alikutana mzee aliyekuwa anauza mayai "Dada alimuuliza,'unauza bei gani yai moja?'Mzee akamjibu Tsh 250 mwanangu..!'akamwambia nitachukua mayai 6 kwa 1000 badala ya 1500 kama haukubali naondoka,,!' " Mzee akamjibu:'njoo uchukue kwa bei yako mwanangu yamkini huu ni mwanzo mzuri sababu sijauza toka asubuhi" : "Akachukua mayai na kuondoka huku akijiona mshindi,akaingia kwenye gari lake akaelekea mgahawa wa jirani na marafiki zake,hapo wakala na kunywa na kuagiza kila walichokihitaji,wanakula kidogo na kubakisha kingi kwa vile walivoagiza,akaenda kulipa bill,akaambiwa anadaiwa 95000 akatoa laki moja na kumwambia mmiliki wa mgahawa keep change(sitaki chenji)" : "Tukio linaezaonekana kawaida sana kwa mmiliki wa mgahawa ila lisionekane kawaida kwa mzee muuza mayai" ~Pointi ni hii~"Kwanini tunapenda kujionesha kuwa wenye nguvu tunaponunua kitu kwa watu wa hali ya chini ambao ndio wenye uhitaji zaidi na tunajionesha kutokujali tunaponunua kwa wasio na uhitaji" : "Wakati mwingine upo tayari ukanunue kilo ya sukari super market kwa bei ya 3500 wakati mtaani kwako kuna kijana ana kibanda kilo ya sukari anauza 2700" ~Upendo ni kitu kimoja,utu ni kitu kingine,ubinadamu ni Upendo uliofungamana na utu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hellow hakikaa.
Wanasayansi waliwahi kufanya utafiti ili kupima nguvu ya “self-belief”(Hali ya kujiamini katika kufanya mambo).Waliamua kumchukua tembo aliyezaliwa na kumfunga kwa kamba kwenye mti tangu siku ya kwanza alipozaliwa.Tembo yule kila alipojaribu kutoka,kamba ilimzuia na kumuwekea mipaka ya umbali ambao anaweza kwenda.Baada ya Muda alijikuta anazunguka kwenye umbali unaoendana na urefu wa Kamba yake tu. . Tembo yule alikua mkubwa na kutokana na UZITO na UKUBWA wake angeweza KUKATA ile Kamba kwa kujivuta na kuwa HURU lakini cha kushangaza HAKUJARIBU KABISA kufanya hivyo.Hata pale alipowaona wenzake wakubwa kama yeye wakiwa HURU yeye aliamini hawezi kufanya lolote lile zaidi ya kubakia kwenye urefu wa ile kamba nyembamba. . Watu wengi wana UWEZO mkubwa sana ila WAMESHIKILIWA na KAMBA NYEMBAMBA ambazo haziwaruhusu kufanya mambo MAKUBWA. . Kwenye kila OFISI kuna watu wameshajiwekea MIPAKA ya UWEZO wao kutokana na UZOEFU,ELIMU ama mambo yaliyowahi kuwatokea huko nyuma.Kuna watu hawapigi hatua kwenye BIASHARA kwa sababu kuna Kitu wanaamini KINAWAZUIA hata kama hakina UWEZO wa kuwazuia.Kuna watu wana KAMBA kuhusiana na MAFANIKIO YAO YA KIFEDHA,wengine hawaamini kama wanaweza kuwa na MAHUSIANO MAZURI yenye FURAHA TENA n.k . Watu wenye Kamba utafanya tu,kila siku utawasikia “Hiki Hakiwezekani”,”Hii nilijaribu nikafeli”,”Fulani alifanya hakufanikiwa” n.k Wengi wenye kamba huwa wanataka wakufunge na wewe kwenye kamba zao.Uwe makini! . Wengi wana UWEZO ila wameruhusu KAMBA ziwafelishe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatarrrrr
IMG-20190401-WA0046.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
*Mwalimu mmoja aliita wanafunzi wake akawaambia''Kesho kila mwanafunzi aje na nyanya kulingana na idadi ya watu anaowachukia, Yaani kama unamchukia mtu mmoja uje na nyanya moja kama ni wawili basi njoo na nyanya mbili vilevile.* *Nyanya hizo mtazibeba kwenye mabegi yenu ya kubebea madaftari na vitu vingine vya shule* *"Wanafunzi wakakubali halafu kesho yake wanafunzi wakazibeba zile nyanya vizuri kabisa wengine walibeba moja,wengine mbili na wengine nyingi sana.* *Kama mwalimu alivyosema zile nyanya zikapewa majina ya watu ambao wanafunzi wanawachukia*. *Baada ya kuzipa hizo nyanya majina mwalimu* *akawaambia kila mwanafunzi azirudishie nyanya zake kwenye begi lake halafu aziache humo humo ndani ya begi kila siku awe anakuja nazo shuleni na kurudi nazo nyumbani.* *Baada ya siku kadhaa wanafunzi wakaanza kulalamika hasa wale waliobeba nyanya nyingi kuwa nyanya ni nzito sana na zinatoa harufu mbaya na zinaharibu vitu vyao vizuri walivyoweka kwenye mabegi yao* *Mwalimu akawaambia hivi ndivyo ilivyo mtu unapoweka watu usiowapenda moyoni* *kama mtu huwezi kuvumilia kukaa na harufu ya nyanya* *kwenye begi vipi kuhusu madhara ambayo moyo wako unayapata kwa kuubebesha mzigo wa chuki dhidi ya watu.?* *Moyo unapata madhara makubwa sana unapobebeshwa chuki kila wakati kila siku moyo unakuwa na chuki na hapo ndipo unaharibika* *na kusababisha kuharibu hata vitu vingine vizuri vilivyokoko moyoni mwako. Moyo ni kama lile begi la kubebea madaftari unahitaji kubeba vitu vizuri na visivyo na chuki ndani yake* *Safisha moyo kwa kusamehe wanaokukosea, jifunze kusamehe maana ni moja ya virutubisho vya moyo wako,Samehe kwa kila anayekukosea na kukukwaza.*
Good

Love and peace
 
Back
Top Bottom