Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
10,024
24,374
Kuna vijimisemo vifupi vimeibuka huku kwenye mitandao kwa sasa, yaani ni burudani tupu.

Ukivisoma mwisho lazima ubaki mdomo wazi au ucheke, baadhi ya niliyokutana nayo naweka hapa, pia karibuni kwa wenye zaidi tuburudike pamoja.
Tuanze na hivi:-

1. Leo kidogo nipigwe na mwanamke baada ya lifti kusimama, wakati tupo kwenye lifti Nilikua nayaangalia maziwa yake akasema "Bonyeza moja" mimi si nikalibonyeza yaani hadi sasa bado najiuuliza nilipokosea?

2. Hivi utajisikieje utakaposikia rafiki yako wa karibu hajaja kwenye mazishi yako? Nadhani mimi sitamwongelesha tena!
nafikiri nakaribia kupona

3. Nimenunua chips ili nile. Kwa bahati mbaya mtoto wa mama mwingine amekaa karibu na mimi akaanza kuzililia. Imebidi nivae earphones. Napenda watoto, ila utoto ndio sipendi.

4. Jana nimepita njia ya mkato makaburini, warembo wawili wakawa wananikimbilia wanatetemeka eti tunaogopa kupita peke yetu na mimi nikawajibu hata mimi nilivyokuwa hai nilikuwa naogopa sana. Wakazimia.

Sipendagi kufatwa fatwa.
 
mkuu umesema watu wenye stress tupitie hapa
Okay, kumbe unaielewa hali yako!
Karibu..

Niliwahi kusikia kuwa maji na mafuta havichangamani, na pia mafuta huwa yanaelea juu ya maji... Basi jana mimi nikaamua kupaka mafuta mengi tu miguuni kisha nikaingia baharini ili niweze kutembea juu ya maji maana nilihisi ningeelea na kuweza kufanya chochote.

Sikumbuki nini kilitokea lakini nilijikuta nimelala mchangani watu wakiwa wamenizunguka huku wakisema niwashukuru sana wavuvi. Nadhani watakuwa wamenipa samaki wa bure.
 
Leo nimeenda kuchangia damu hospitalini,mara wananambia soda na biskuti zimeisha..!
Sa hii nipo zangu njiani na damu yangu kwenye blood bag naelekea nyumbani. Bora niwapelekee mbu take away..


wala sijawahi vutaga bangi Mimi
 
Mimi sina stress nimejikuta tu hapa
Basi utaondoka na stress..!

Stress ni nini??
Stress ni pale umeenda kijijini kwa bibi ako huku umebeba jeans zako tano zile ja mtindo wa kuchanika (chanika jeans) sasa siku ukazifua ukazianika ukaenda zako kutembea ile unarudi jioni unakuta bibi yako kazianua afu kazishona zote!


Future
 
317 Reactions
Reply
Back
Top Bottom