Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

bioto yona raphael

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2017
Messages
933
Points
1,000

bioto yona raphael

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2017
933 1,000
Kuna maprofesa 40 walipanda AIR TANZANIA ili
wasafari. Kabla ndege haijaanza kuondoka, Lilipita
tangazo kama ifuatavyo:
Ndugu wasafiri wote, ndege unayotarajia kusafiri
nayo imetengenezwa na wanafunzi wa Kitanzania.
Baada ya tangazo maprofesa wote waliteremka
isipokuwa mmoja alibaki kwenye kiti chake
Walipomuuliza ni kwanini hakuondoka akajibu kwa
haraka na furaha kuwa:
Kama ndege hii imetengenezwa na watanzania, hata
kuwaka haitawaka!
ule Marekani mume anapoenda kulala anamwambia
mke wake “goodnight baby”
Kule Uingereza mume anapoenda kulala humtakia
mke wake usiku mwema kwa kusema “sweet
dreams honey”
Kule Australia mume anapoenda kulala humtakia
mke wake usiku mwema kwa kusema “goodnight
my love”
Huku kwetu Tanzania mume anapoenda kulala
humuuliza mke wake “umefunga milango yote na
madirisha vizuri?”
===========
Mwanamke aliingia kwnye teksi akitaka huduma
akiwa uchi kama alivyozaliwa!
Dereva akawa anamshangaa,
Mwanamke: hujawahi kuona uchi au!
Dereva: Ninachoshangaa si uchi wako,najiuliza pesa
ya kunilipa utakuwa umeiweka wapi?
============
Nyerere: Kama vile nakufananisha?
Mandela: Hata mimi naona sio sura ngeni?
Nyerere: We ndie Mandela eee?!
Mandela: Ndiyo mimi haswa miaka 14 ni mingi.
Nyerere: Sana!!.
Mandela: Sasa nitakaa wapi mbona hakueleweki
huku?
Nyerere: We ngoja utapaelewa tu.
Nyerere: Eeh!! vipi huko Tanzania? ulitembelea hata
hivi karibuni?
Mandela:
Eeeh! we acha tu, huko mara Zitto msaliti, mara
Umeme mgawo miezi sita, mara mgomo wa Gesi
haitoki Mtwara, mara kifo cha Mwangosi, mara
Dawa za Kulevya, mara Meno ya Tembo, mara
kuchoma Makanisa, mara mabomu kwenye
mikutano ya hadhara na makanisani, mara Ufisadi,
mara Dr. Ulimboka na Kibanda kung’olewa kucha na
meno kwa plauzi, mara Division 5, mara Udini, mara
ngumi Bungeni, mara kifo cha Dr Mvungi, mara
tindikali kwa mapadri, mashehe na wageni, mara
Kagame kuishambulia Tanznia, Petroli
kuchakachuliwa, mara wengine wanasema eti
Muungano ulioasisi unatokana na Visiwa vya
Zimbabwe na Zanzibar na sio Tanganyika tena, mara
muungano wa serikali tatu ndio unaotakiwa, mara
Kigamboni kapewa Obama, mara Bushi na mke
wake kaja Tanzania, Clinton na mke wake kaja
Tanzania, Kamerun na mke wake kaja Tanzania,
Xiing wa uchina kaja Tanzania, mara puttin wa Urusi
kaja Tanzania. Yaani hekaya ni ndefu bora urudi
ukayashuhudie mwenyewe.
Mara Mandela alipomrushia macho swahiba wake
kumbe kashazimia saa nying
------------------------------------
Hebu fuatilia kichekesho hiki na angalia usivunjike
mbavu
Kuna Mchaga mmoja kanasa kwenye kisima
asubuhi na mapema akiwahi kibaruani. Kisima hicho
kilitelekezwa na jirani yake
Baada ya maangaiko makubwa ya kumtoa,
mmojawapo wa watoto wake alikuja na kamba na
kumtupia ili waweze kumnasua kisimani.
Mahojiano yalikuwa hivi
Mtoto: Baba ebu daka hiyo kamba uing’ang’anie ili
tukuvute mpaka utoke uko
Baba wa kichaga: Kwani hiyo kamba umenunua
shilingi ngapi na kwa nani?
Mtoto: Nimenunua Shilingi elfu moja kwenye lile
duka la mpare
Baba wa Kichaga: Alipatwa na mshangao haraka
akajibu, Eyowii!! Amekuuzia ghali sana kijana, ebu
rudisha na ukanunue kamba kwa Mosha anauza mia
tano.
Wote: Wakashangaa, wakacheka na kuvunjika
mbavu!
===========================
Kuna mambo mawili ukizaliwa na kuishi yatakuhusu
Ni ama wewe utazaliwa mwanaume
Au wewe utazaliwa mwanamke
Kama wewe utazaliwa mwanamke uko salama,
Lakini kama wewe utazaliwa mwanaume kuna
mambo mawili yatakuhusu
Aidha wewe utaajiriwa uraiani
Au utaajiriwa jeshini
Kama wewe utaajiriwa uraiani uko salama,
Lakini kama wewe utaajiriwa jeshi kuna mambo
mawili yatakuhusu
Aidha wewe utafanya kazi za ofisini
Au utafanya kazi za mstari wa mbele vitani
Kama wewe utafanya kazi ofosini uko salama,
Lakini kama wewe utafanya kazi mstari wa mbele
vitani kuna mambo mawili yatakuhusu
Aidha wewe utaua
Au Utauawa
Kama utaua mtu uko salama,
Lakini kama utauawa kuna mambo mawili
yatakuhusu
Aidha mwili wako utazikwa
Au mwili wako utatumika kama mbolea.
Kama mwili wako utazikwa uko salama,
Lakini kama mwili wako utatumika kama mbolea
kuna mambo mawili yatakuhusu.
Aidha wewe ni itatumika kwa kupanda maua
Au utatumika kupanda miti.
Kama ilitumika kwa kupanda maua uko salama,
Lakini kama itatumika kwa kupanda miti kuna
mambo mawili yatakuhusu.
Ni ama zitatumika kutengeneza karatasi za kutumia
chooni
Au itatumika kutengenezea samani za ofisini na
majumbani.
Kama zitatumika kutengeneza samani za ofisini na
majumbani ni salama,
Lakini kama zitatumika kutengeneza karatasi za
chooni kuna mambo mawili zitahusisha
Aidha zitatumiwa na mwanaume
Au zitatumiwa na mwanamke
Kama zitatumiwa na mwanaume ni salama,
Lakini kama zitatumiwa na mwanamke kuna
mambo mawili yatakuhusu
Aidha zitatumika kusafisha upande wa nyuma
Au zitatumika kusafisha upande wa mbele
Kama zitatumika kwa nyuma uko salama
Lakini kama zitatumika kwa mbele malizia
mwenyewe mambo mawili yatakayotekea…
========================
 

Careem

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Messages
19,026
Points
2,000

Careem

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2013
19,026 2,000
Katika maisha yangu sijawahi kuona Albino kachora tatoo! Naomba kwa anaejua anifahamishe alipo nikajionee

Cᵃʳᵉᵉᵐ ₜₕₑ ᴸᵉᵍᵉⁿD
 

Careem

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Messages
19,026
Points
2,000

Careem

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2013
19,026 2,000
Ace ventura in "When nature calls"
Ace Ventura: Tell them what I'm saying. [faces the Wachootoo] I come in peace!

Ouda: [in poorly-translated Wachootoo] White Devil say, "I will harm you." [The Wachootoo look suspicious]

Ace: [to Ouda] I couldn't help but notice the "equinsu ocha" part. Did you just refer to me as "white devil"?

Ouda: This how they know you.

Ace: Leave that part out from now on! [to Wachootoo] I represent the princess!

Ouda: [in poorly-translated Wachootoo] "I am a Princess." [tribesmen look confused; one young man eyes Ace with interest]

Ace: War is hell. The last thing we want... is a fight!

If you missed this, alright then sorry!


Sent using
 

Forum statistics

Threads 1,390,681
Members 528,238
Posts 34,058,740
Top