Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Kama utakipenda kimoja njoo PM tuzungumze biashara
1. Freezer aina ya Boss Tsh250000. Haina mlango wa mtungi wa gesi
.
2. Feni ya chini Tsh 15000/=. Inawaka kwa machale.. yaeza kukaa hadi masaa 2 haijaanza kuzunguka
,
3. Pasi ya umeme aina ya Phillips. Tsh 12000/=, haishiki moto kabisa hata ikae nusu saa kwny umeme na kidude cha kuregulate moto kimeharbika..

4. Meza ya plastic Tsh 75000/= ina miguu 3 na mmoja mfupi kidg.

5. Vikombe vya udongo Dozen 1 Tsh 25000/= ila vilipata ajali kidg.. vimekatika mikono na vingne vimetoboka chini
6.Redio ya caset lkini haina transiforma bei 34000
7.Flat scren bei 50000 kioo kimepasuka na haina rimot control na batan zime haribika fasta nichek
8.Simu aina ya Sumsung s7 edge 470000/= ilidondokea kwenye maji ikapiga shot, kitufe cha kuwashia hakipo na hata ukiweka kingine haiwaki, ni simu nzuri bora na ya kisasa!
9.Kamera aina ya sony mp 16 bei 62500/= haina lens, ni mbovu hata mafundi hawaitaki kama spea.
10.Bajaji aina ya tvs, bei 1400000/= haina matairi, viti wala usukani! Imetumika miaka 8 na inadaiwa kodi ya miaka 2!

Karibuni, bidhaa ni nyingi sana, zipo za aina tofauti tofauti kama magari, ndege, treni, meli, maparashuti, vifaru, n.k vyote hivyo vikiwa katika hali mbaya sana, (ikumbukwe hizi ni toys za watoto zilizotumika huko uswahilini na kutupwa kwenye majalala)
 
*Tulikua kwenye basi tunaelekea arusha, ile namcheki dereva kumbe ni best yangu na basi ilikua kwenye spidi hatari,* *nikaenda kumziba macho nikamuuliza* otea mi ni nani, kabla hajanijibu nikasikia kishindo kikubwa sana
na sasa hivi nimezinduka naona abiria wote tupo wodi namba 3 hapa KCMC Moshi nafkiri stendi imehamishiwa huku sikuizi.


*Akili zangu nazijua mwenyewe!!!*
 
Kuna vijimisemo vifupi vimeibuka huku kwenye mitandao kwa sasa, yaani ni full burudani!
Ukivisomo mwisho lazima ubaki mdomo wazi au ucheke, baadhi ya niliyokutana nayo naweka hapa, pia karibuni kwa wenye zaidi tuburudike pamoja!

Leo kidogo nipigwe na MWANAMKE baada ya LIFTI kusimama...wakati tupo kwenye lift Nilikua nayaangalia MAZIWA yake akasema "Bonyeza Moja" mi si nikalibonyeza?
Yaani had sasa
bado najiuliza nilipokosea.


Hivi Utajisikieje Utakaposikia Rafiki Yako wa Karibu Hajaja Kwenye Mazishi Yako ???!
Nadhani Mimi Sitamwongelesha Tena !!!!
I think nakaribia kupona


Nimenunua chips ili nile kwa bahat mbaya mtoto wa mama mwingine amekaa next to me akaanza kuzililia.
Imebidi nivae earphones. Napenda watoto, ila utoto ndio sipendi..


Jana nimepita njia ya mkato makaburini warembo wawili wakawa wananikimbilia wanatetemeka Eti tunaogopa kupita peke yetu na mm Nikawajibu hata mm nilivyokuwa hai nilikuwa naogopa sana . Wakazimia
Sipendagi kufatwa fatwa mm
Thanks
 
Mi si mwenyeji wa hapa....nimepotea
Hujapotea kwani wewe huna stress..?
------------------------------
nimemtembelea,rafiki yangu mida ya saa saba hivi na tayari alikuwa amesonga ugali nikamtuma nje wakati anatoka nje nikaongeza maji kwenye sufuria kumbe sikujuwa alipima maji kulingana na unga uliobaki sasa hivi tunakunywa uji hatuongeleshani .

kumbe_wote_hatupendangi_ujinga!
 
AISEE NIMEPENDA HUU UZI. NIMECHEKA BASI. UZURI NIKO PEKE YANGU LA SIVYO NINGEITWA CHIZI
Usiache kujisubscribe ili upate update kila mafataki mapya...

=====================================
Leo nimepulizia Air Fresh yenye Harufu ya Pilau nyumbani kwangu sasa watoto wa Jirani wamehamia Mlangoni kwangu ndio wanacheza hapo. Kila nikitoka wananisalimia. Mama yao ndio kanimaliza kabisa nimetoka akaniambia
Kumbe wewe ni Mpishi mzuri,
Sipendagiiiiii ujingaaaaaa mimi...
zote kali!!
 
Back
Top Bottom