Kama una rafiki yako ametokea Moshi na Gari BMW white namba T223 DPU amepata ajali Mombo

Dereva wa gari yupo chini ya ulinzi, jiulize kwa nini? Jibu simple tu sababu amevunja sheria ya usalama barabarani

Jiulize kwa nini hiyo chini ya ulinzi hajawekwa dereva wa treni?

Kumbe hata kusoma ni shida kwako. Narudia tena. Ni usiku kuna giza, nimefika hapo mwenye crossing, hakuna taa,treni haina taa,haijapiga honi, nitaionaje? Mnapenda tu kulaumu na kuhukumu.

Railway crossing yenyewe inatakiwa iwe na taa nyekundu,kengele na barrier ya auto au manual.
 
Dereva wa gari yupo chini ya ulinzi, jiulize kwa nini? Jibu simple tu sababu amevunja sheria ya usalama barabarani

Jiulize kwa nini hiyo chini ya ulinzi hajawekwa dereva wa treni?
Kuwa chini ya ulinzi haina maana you are guilty.
 
Dereva wa gari yupo chini ya ulinzi, jiulize kwa nini? Jibu simple tu sababu amevunja sheria ya usalama barabarani

Jiulize kwa nini hiyo chini ya ulinzi hajawekwa dereva wa treni?

Kuwa 'chini ya ulinzi' sio 'proof' ya kutenda kosa linalotajwa.

Hiyo chini ya ulinzi hajawekwa dereva wa train kwasababu kuna Sheria gandamizi and/or law enforcers wana uelewa kwamba Train, at 'any circumstances' huwa haigongi. Kitu ambacho sio sahihi na ni unfair.

Kiuhalisia, kuna circumstances ambapo Train inakuwa imegonga!

Endapo ni kweli Sheria ipo strict kuwa "at any circumstances, train huwa haigongi"... basi suala hili ni totally unfair. Inahitajika reforms kwenye Sheria na Sera kuhusu suala hili.

-Kaveli-
 
Ushawai kufanya kazi kampuni ya bima yeyote.. au umewai somea mambo ya insurance..

Bima hailipi lipi ovyo.. sio kila mwenye bima kubwa analipwa kwenye janga.. hata kama ni uzembe wake..

Ajali kama hii hakuna kampuni ya bima itakayolipa.. sababu sheria haiko upande wa dereva wa gari..

Sheria ya usalama wa barabarani ya mwaka 1970 na imefanyiwa marekebisho mwaka 1995 inasema toa kipaumbele kwa wa kulia kwako na lazima utoe kipaumbele kwa gari moshi..

Sheria ya usalama barabarani inailinda treni kwamba haigongi gari bali gari ni lazima iipe treni kipaumbele.. kwa kusimama kwenye makutano ya reli na kusubiri mpaka treni iwe haipo kabisa ndio ipite..

Yaani hapo kampuni ya bima inachekelea faida ya bure kama jamaa ana bima kubwa.. maana hawamlipi hata senti.. sheria inawalinda..
Mkuu comprehensive inalipa ukigonga au ukigongwa hapanunaelewa nn? ajali nyingi Zina element ya uzembe Kama unachokiongea kina ukweli Basi watu wasingekuwa wanalipwa.
 
Treni haisimamagi kupisha gari
Na kama madereva watakuwa na ufahamu huo eti treni iwapishe watazidi kuchinjwa kama kuku

Ova
Yesu wangu kweli kabisa kuna watu wanataka kuleteana ubavu na treni humu?
Kuwa eti kwanini treni isipishe gari?!?!

Endeleeni tu kuendesha kwa mentality hiyo, ipo siku yatakukuta.

Nyie ndio huwa mnachomekea lori za mizigo mkidhani eti na yeye atasimama ghafla akupishr.

Au mnashindana na lori kwenye kona kana kwamba na yeye anaweza kukunja kona bila kuvuka upande wa pili.

Asilimia kubwa ya udereva ni kuwa aware na mazingira yako na limitations na capabilities za vyombo vingine mnavyoshare navyo barabara. Mentality za kibabe hizo hazina nafasi barabarani, otherwise hayo yanakukuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu leseni wanapata kwa rushwa... madereva wengi wana uzembe sana Tanzania.. tuna amini vifo anapanga Mungu...kumbe vingine ni uzembe tu..

Una leseni ya gari umeipata kwa rushwa hujui hata defensive driving ni nini ? halafu unapata ajali unasema Mungu kapanga

Hujui hata sheria ya barabarani inasemaje? Hujui hata alama za barabarani zipo makundi mangapi na zinasemaje? Hujui hata basic of mechanics.. majuu hadi upate driving licence lazima wakuone umeelewa udereva makini ni nini? Ndio maana huwezi ona ajali za gari na treni au ajali za kipuuzi puuzi
Watu wengi Wanajua kuendesha tu sheria hawazijui........

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani gari haliko kwenye njia yake?

Kumbuka haya ni MAKUTANO ya reli na lami.

Nchi za watu treni haiwezi kuua halafu ikabaki salama kwa kigezo cha "ilikuwa kwenye njia yake."
Dah....naomba nikuite Dr. Bu'yaka ...kuanzia leo

Sent using Beretta ARX 160
 
Mkuu comprehensive inalipa ukigonga au ukigongwa hapanunaelewa nn? ajali nyingi Zina element ya uzembe Kama unachokiongea kina ukweli Basi watu wasingekuwa wanalipwa.

Umeshawi kufuatalia madai yeyote insurance ukaona taratibu zao mpaka wakulipe zikoje?

Unajua bima kubwa inakulipa baada ya taratibu gani kukamilika?

Unajua kama bima ipo kisheria na inalipa kwa kufuata sheria..

Nenda kasome sheria ya bima za magari, kifungu namba 4 (1) na (2) cha motor vehicle insurance ordinance cap 169 ili uelewe vizuri kuhusu bima inaingiliana vipi na sheria ya usalama wa barabarani ya mwaka 1970 katika kulipa madai..

Maana naona wengi mnaendesha magari kwa leseni za kuletewa... mnajiita madereva bila kupita Veta wala NIT

Ukiona ajali ya uzembe imelipwa na bima ni sababu uchunguzi umedanganya kwenye ripoti baada ya kupokea rushwa.. yaani traffic aliyepima ajali kwenye ripoti yake adanganye na wachunguzi wengine uwape rushwa ili ripoti zao zidanganye.. hapo sheria inawalazimisha bima kukulipa sababu ya ripoti za uchunguzi zitakuwa upande wako mwenye gari.... kwa case kama hii ambayo imetokea katika makutano na reli hakuna ripoti itakayokubeba mwenye gari hata ukitoa rushwa.. sababu sheria ya usalama barabarani haikuruhusu kuvuka makutano ya reli bila kusimama.. kutazama kushoto na kulia.. na kutoa kipaumbele kwa garimoshi..

Kwa sheria zetu za Tanzania treni imepewa upendeleo mkubwa.. ndio maana tunasema trenu haigongi bali gari inagongwa treni.. sababu treni imepewa kipaumbele katika sheria ya usalama barabarani
 
Bwana wa Majeshi akawaponye. Doreen kulikuwa Chuma Cha reli halafu shule mtoni u know Aston Uni....

FB_IMG_1583244480831.jpeg

Mkuu tunajifunza kila siku. Leo nimejifunza kwako kitu kipya. Lakini nimeuliza mtu mmoja alikuwa kwenye insurance business alichojibu ni hiki hapa chini nimepata hata Google.
Screenshot_20200303-173322.png
 
Vizuri kwa ku google.. najua options hizo zipo nchi zilizoendelea...

Majuu wametuacha mbali sana kwenye customer service.. huwezi linganisha na huku africa..

Neno mteja ni mfalme majuu lipo kweli sababu serikali zao haziingilii vitu vingi vya wafanyabiashara.. kule mtoa huduma anaweza kujiwekea added value ili apate wateja na awachaji kwa bei anayoyataka bila bugudha na serikali zao mradi analipa kodi.

Tanzania vitu vingi vipo kwa sheria za nchi.. huku mtoa huduma hana nguvu ya kufanya anachotaka.. ndio maana dala dala au bus unanunua wewe kwa bei unayoijua wewe.. ila sumatra wanakupangia nauli..

Hizo bima za kukulipa hata kama umegonga makusudi zipo huko majuu ulipo google.. ila bongo ni ngumu.. kwanza lazima ujue kampuni za bima za bongo hazipend kulipa lipa.. so huwa wanatafuta pa kuchomekea ili wasikulipe... na kesi kama umefanya uzembe ndio wanafurahia sana maada wasipokupipa wao bima wanapata faida zaidi.. na hilo ndio dhumuni lao kuanzisha biashara ili wapate faida.. hawajaanzisha biashara ya bima ili wawe wanalipa lipa kila ajali wapate hasara..

Majuu bima zao zina maamuzi.. bima kama hiyo wanayosema wanakulipa hata kama ni uzembe wako.. ujue inachaji hela nyingi .. sio wajinga walee uzembe

Mkuu tunajifunza kila siku. Leo nimejifunza kwako kitu kipya. Lakini nimeuliza mtu mmoja alikuwa kwenye insurance business alichojibu ni hiki hapa chini nimepata hata Google.
View attachment 1375604
 
Vizuri kwa ku google.. najua options hizo zipo nchi zilizoendelea...

Majuu wametuacha mbali sana kwenye customer service.. huwezi linganisha na huku africa..

Neno mteja ni mfalme majuu lipo kweli sababu serikali zao haziingilii vitu vingi vya wafanyabiashara.. kule mtoa huduma anaweza kujiwekea added value ili apate wateja na awachaji kwa bei anayoyataka bila bugudha na serikali zao mradi analipa kodi.

Tanzania vitu vingi vipo kwa sheria za nchi.. huku mtoa huduma hana nguvu ya kufanya anachotaka.. ndio maana dala dala au bus unanunua wewe kwa bei unayoijua wewe.. ila sumatra wanakupangia nauli..

Hizo bima za kukulipa hata kama umegonga makusudi zipo huko majuu ulipo google.. ila bongo ni ngumu.. kwanza lazima ujue kampuni za bima za bongo hazipend kulipa lipa.. so huwa wanatafuta pa kuchomekea ili wasikulipe... na kesi kama umefanya uzembe ndio wanafurahia sana maada wasipokupipa wao bima wanapata faida zaidi.. na hilo ndio dhumuni lao kuanzisha biashara ili wapate faida.. hawajaanzisha biashara ya bima ili wawe wanalipa lipa kila ajali wapate hasara..

Majuu bima zao zina maamuzi.. bima kama hiyo wanayosema wanakulipa hata kama ni uzembe wako.. ujue inachaji hela nyingi .. sio wajinga walee uzembe
Kwa mara ya pili nimemuuliza mtu mwingine yuko kwenye big insurance company, kasema Comp insurance hata ukiwa na makosa unalipwa. Kusema ukweli wewe ndio mtu wa kwanza namsikia akisema ukiwa na makosa hulipwi hata ukiwa na comp insurance.
 
Ninaweza ku-confirm kwamba kama ajali imetokea kwa fault, mteja analipwa kama ni comprehensive insurance.

Hapo kuna tofauti ya ajali basing on fault, na ajali ya kutengeneza.
 
Back
Top Bottom