Kama una mtaji fanya biashara ya Mbuzi, utakuja kunishukuru

Bei imebadilika asaivi 10300 per kg kama usafili ni wako kama usafili ni wao jamaaa 10000 per kg inamaana kama unambuzi wapi sehemu ni wengi vya kutosha hutoa gari yao Kuna kuwafata Cha umuhimu ni upate tenda ya kupeleka mzigo ndio inakuwa rahisi kwako maaana tukipeleka mbuzi kichwa kichwa utakula hasara wana preference zao wanazitaka inafaaa uzizingatie
Hiyo bei ya 8000 ni ya zamani sana
Samahani chief iyo bei ya kiwanda cha wapi maana nami nataka kupekeka
 
Bei imebadilika asaivi 10300 per kg kama usafili ni wako kama usafili ni wao jamaaa 10000 per kg inamaana kama unambuzi wapi sehemu ni wengi vya kutosha hutoa gari yao Kuna kuwafata Cha umuhimu ni upate tenda ya kupeleka mzigo ndio inakuwa rahisi kwako maaana tukipeleka mbuzi kichwa kichwa utakula hasara wana preference zao wanazitaka inafaaa uzizingatie
Hiyo bei ya 8000 ni ya zamani sana
Mbuzi ki kawaida ana kilo ngapi
 
Habarini Waungwana!

Leo nimeona nitoe mchongo wa biashara ambayo binafsi nimewahifanya kabla sijapata ajira na natarajia kuendelea kufanya baada ya ajira kuisha.

Uzuri wa biashara hii, pamoja na kuwa na faida nzuri, soko lake ni la uhakika sana na changamoto zake ni chache sana na zinakabilika kwa mtu ambaye ameamua kwa dhati kutafuta.

BIASHARA YENYEWE NI KUNUNUA MBUZI NA KWENDA KUUZA KIWANDANI.

A. Upatikanaji wake
Upatikanaji wa mbuzi. Pamoja na mambo mengine ambayo Tanzania tumejaliwa ni mifugo hasa mbuzi. Kuna upatikanaji wa uhakika wa mbuzi na kondoo katika mikoa ya Dodoma (Urangini), Singida, Tanga na Tabora. Kwa kule KONDOA kuna Warangi wazuri sana madalali ambao ni waaminifu sana tofauti na madalali ambao tumewazoea katika jiji la Dar.

Kwa ushauri wangu, sehemu nzuri zaidi ya kununua mbuzi kwa bei nzuri, wenye ubora (Uzito) na faida nzuri, urahisi wa upatikanaji wake na hata urahisi wa usafirishaji ni KONDOA (Urangini). Huku kuna minada ya mbuzi kila siku na hivyo kwa siku unaweza kununua hadi mbuzi 50 na zaidi kama una mwenyeji mzuri.

B. Soko lake
Binafsi ningependekeza kupeleka kiwandani hasa kiwanda cha TanChoice kilichopo Soga, wilani Kibaha mkoa wa Pwani. Hapa utaweza kuuza idadi yoyote ya mbuzi japo huwa wanapenda walau uwe na mbuzi kuanzia 20 (hii ni idadi wakati mimi napeleka inawezekana kukawa na mabadiliko kwa sasa).
Sehemu nyingine ni Longido-Arusha katika kiwanda cha Eliya Food Ltd japo kwa Arusha kuna wanunuzi wengi hasa Wakenya wanatoa bei nzuri sana.

C. Bei ya mbuzi
Kwa kuwa mbuzi hununuliwa vijijini bei yake siyo kubwa kwani ina range kati ya 30-70 elfu. Mbuzi wa 30 elfu anaweza kukadiriwa kuwa na uzito wa kilo 7 au 6.5. Mbuzi wa 70 elfu anaweza kufikisha hadi 12Kg au 13Kg. Kiwandani hawapendelei sana mbuzi wakubwa sana kwa hiyo ni vema kuwa makini katika selection ya mbuzi wa size ya kati ili upate faida nzuri na soko la uhakika.

D. Bei ya nyama kiwandani
Wakati mimi napeleka mbuzi katika kiwanda cha TanChoice, walikuwa wakinunu kwa Tsh 7000/Kg kwa mbuzi na Tsh6800/Kg. Kwa Arusha inasemekana bei iko juu kidogo ila Arusha niseme ukweli sana information za kutosheleza kwani nilienda trip moja tu.

E. Kadirio la faida
Kama mbuzi amenunuliwa kwa kwa Tsh 50,000/= halafu akatoa Kg 9 za nyama ambazo ni sawa na Tsh 63,000/= faida yake itakuwa karibu 6,000Tsh hadi 7,000Tsh kwa mbuzi mmoja. Hapa unakuwa umetoa Gharama zote kuanzia usafiri kutoka Dar nimetumia kwa wakazi wa Dar hadi Kondoa, kulala guest, usafiri kwenda minadani, kuwasafirisha kutoka minadani hadi Kondoa mjini, ushuru wake na vibali, usafiri kwenda Dar kiwandani, chakula na mengineyo.

F. Changamoto zake
Kusema ukweli kila kazi ina changamoto zake na hasa inapokuja suala la biashara, basi changamoto haziepukiki. Biashara hii kama zilivyo biashara nyingine ina makandokando yake kama ifuatavyo;
  • Kuna wakati kunakuwa na wanunuzi wengi wa mbuzi kwa hiyo competition inakuwa kubwa sana na kupelekea wauzaji kupandisha bei na hivyo faida kukuachia kidogo sana
  • Usipokuwa makini madalali ambao wameshawahi kufika Dar basi lazima watakulalia katika ununuzi wa mbuzi. Binafsi kwa mara ya kwanza nilijikuta kwa kila mbuzi mmoja napigwa 2000-3000Tsh. Yaani mbuzi anamununua 40,000Tsh halafu ananiambia amemchukulia 43,000Tsh.
  • Kuna wakati upatikanaji unakuwa mgumu hata kama wanunuzi siyo wengi. Baadhi ya siku unakuta wanaoleta mbuzi minadani ni wachache sana na hivyo unaweza kutumia siku nyingi kupata mzigo mzuri.
  • Uwezekano wa kuibiwa mbuzi. Kumbuka munapowanunua mbuzi kutoka mnadani basi munawahesabu na kila mnunuaji anaweza label ya kwake kwenye mbuzi kwa kutumia mkazi. Mimi ilikuwa nachora herufi K ambayo ni herufi ya kwanza ya jina la wife. I love her and she knows that. Baada ya hapo munawaweka mbuzi pamoja na kumkabidhi kijana anayewaswaga kutoka mnadani(minada ipo maporini sijui kwanini) hadi kuwafikisha mjini. Baada ya hapo mbuzi wote wanawekwa kwenye gari na kupelekwa kiwandani. Wakati mwingine mnaweza kupata gari linaloishia Dodoma na kulazimika kuunganisha na wanunuzi wengine wanaofikishia mzigo wao Dom mjini na kisha kutumia gari moja kupeleka kiwandani. Sasa inaweza kutokea au kijana anayewaswaga kutoka mnadani akapiga pande mbuzi mmoja au vijana wanaowaangalia na kuwapeleka malishoni kama unanunua mzigo mkubwa kwa siku kama tatu au zaidi.
-Mbuzi kukosa uzito wa kutosha. Hapa ndo sehemu ya kuwa makini sana. Mbuzi wanaotoka Tabora kwa mfano, uzito wake ni mdogo sana wanapochinjwa tofauti na mbuzi wa Kondoa. Kwa hiyo ukinunua mzigo Tabora kwa bei kubwa kuna uwezekano ukaingia loss na kurudi hapa kunitukana na kunilaumu. Naomba kwa atakayekuwa interested aulize maswali ya kutosha na ikiwezekana afike Kondoa kufanya preliminary investigation and research. I do recommend Kondoa kwa warangi.
G. Malipo

Unapofikisha mzigo kiwandani unaandikisha idadi ya mbuzi, na label uliyowawekea. Kisha unawaachia bank account au namba ya simu kama utapenda malipo yafanyike kwa njia ya simubank. Baada ya siku moja au mbili maximum unatumiwa kiasi cha uzito uliopatikana baada ya kuchinja mzigo wako na kisha account yako inasoma. Hapa kwenye malipo mara nyingi hakuna usumbufu japo binafsi nilifikiria sana reliability yake yaani wanakwambia umepata KG 500, kwa mfano, inakuwa ni hiyo hiyo au inawekana ilikuwa zaidi?

Hitimisho
Kila biashara ina changamoto kama nilivyosema mwanzoni lakini biashara ambayo soko lake ni la uhakika na mzunguko wake ni wa uhakika basi daima huwa ni biashara nzuri. Kwa yeyote anayependa kujaribu biashara hii, nashauri afanye utafiti wa kutosha na kisha aanze na mzigo kidogo hata wa 1M kwanza aone faida yake, changamoto zake n.k.

ASANTENI KWA MDA WAKO NAKUTAKIENI MAFANIKIO KWA KAZI UFANYAYO.

Habari yako kiongozi samahani kwa usumbufu nilikua nahitaji kufahamu kuhusu hii biashara ya mbuzi, japo naona ni post ya muda mrefu kidogo, je? Hakuna vyaraka au vibali vyovyote vya kiserikali ambavyo labda vitahitajika kama utambulisho labda wa mlipa kodi ili mtu aweze kufanya hii biashara ya mbuzi.
 
Kitu kikubwa nilichokiona kwenye hiki kiwanda(nafkiri hata hiyo tanchoice ni hivyo), yani unapeleka mbuzi/kondoo wako alaf wao wanawachinja, wanawachuna nakutoa vitu vyote vya ndani, kwaiyo nyama ndo inapimwa kwenye mizani yao alaf kilo zinazopatikana ndo unalipwa sasa. kwa mbuzi kilo ni elf8. sasa kitu kibaya zaidi nlichokiobserve ni hicho kitendo cha wao kupima nyama pekee na huku material yote ya ndani hayajumuishwi na wala haupewi undoke nayo. sasa kwaiyo wao ile ngozi pamoja na material yote ya ndani ni mali yao(nafkiri unaweza kuona wanavyopata super profit kupitia wewe mletaji). kwaiyo ukinunua mbuzi kwa kufanya makadirio ya buchani haiwezekani
HIVYO VITU VYA NDANI NDIO MBASA ANACHUKUA ANATUUZIA MAINI ELFU 3
KILA KONA UKIPITA UNASIKIA KARIBU MBASA BUCHER MAINI ELFU 3, KICHWA CHA MBUZI BUKU.
 
Hakuna biashara hapo biashara ina mirorongo mingi Alafu Mimi niweke mfano laki 8 ninue mbuzi wa elfu50 wawe 16 kwenye kila mbuzi mfano awe na kilo 9 sawa na 63000 ukitoa matumizi nibaki na 6000 faida kila mbuzi kwahiyo 6000 * 16= 96000 Tsh 96000 siwezi huo ujinga biashara zenyewe na wachina sijui wahindi bado kwenye kilo wakupige
Uiishapiga hesabu wakiwa mbuzi 200 unapata kias gan kila wiki?
 
Nafuga kondoo na mpka sasa Mimi ni mtaalamu mzuri ktk ufugaji kondoo...kuna kitu naona bado kinanitesa sana ktk maisha yangu kwa sababu sijakikamilisha ipasavyo nafuga kondoo wachache tu bado sijafikia lengo na bado sijaanda mazingira ya kufuga kondoo wengi hichi ndo kitu kinantesa
Naishi kijijini ila ni kijiji ambacho umeme upo,maji yapo, Barabara zinapitikaa na usafiri wangu wa boxer kwenda mjini na kurudi unanitosha sana...kijiji chetu naweza kufuga hata kondoo 900 na zikala majani mpka zikayaacha huwa napiga hesabu nikitimiza majike ya kondoo 300- 400 na madume 5 tu hapa kijijini... Mimi ni TAJILI uwezo wa kuwa nazalisha kondoo 900-1000 kwa mwaka upo...kondoo anazaa Mara 2 kwa mwaka anabeba mimba miezi mi3 je nkizalisha 800 na nkiwauza sh50000 kwa kila kondoo moja....hapa kijijini NTATAMBA si mchezo ngoja niandae mazingira.
Umefikia lengo?
 
Mimi hapa...Niko nimeanza

Naomba na wengine wasome hapa kama hawatojali..kwa sasa mbuzi wako juu sana,ni high season wakulima wana pesa za mbaazi na dengu wanaringa hawauzii njaa..mbuzi mpk 150k kwa mbuzi mmoja na kondoo pia bei ndo ziko hvyoo....Mimi nilikua na kiasi nkaongezewa ila mpk mda huu nazunguka minadani bado sijafanya kutafura unafuu maana hakuna mbuzi wa 50k may be vile vidogo Sanaa..

Wanaofanya kwa sasa ni wazoefu tu wa business wanalinda mitaji yao na wao kwa kua wengi wanajua biashara at least wanapata faida japo kidogo sana na advantage kubwa wao huku wengi wana mini yao hvyo hawagharamii malazi plus msosi...kwa mgeni kama sisi ukiingia kichwa kichwa itakula kwako uanze laumu watu...Mimi toka Alhamis nazunguka na pesa yangu naogopa nisije nkachoma bure na kutafuta mchawi..
Msimu mzuri wa kuanza hii biashara kwa huku Kondoa ni December may be utafute chimbo lingine ila kwa huku nimeogopa..December to April mbuzi mkubwa kabisaa unampata mpk elf 60 ambae kwa sasa wanauzwa laki na 50!!!
Kaka jebel alieleza vzr kule juu namimi nakazia umakini msiseme hamjaambiwa!!
Ahsanteni

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
Update??
 
Aliyepo kanda ya Ziwa na anafanya hii Biashara naomba taarifa zifuatazo juu ya hii Biashara:-

1. Maeneo/ minada ya mbuzi inapatika wapi haswa Kwa wingi?

2. Bei ya mbuzi Kwa misimu tofauti tofauti

3. Kiwanda/ Viwanda vinavyonunua mbuzi vipo mikoa gani na Kwa kilo moja wananunua shilling ngapi?

4. Kadrio la chini la mtaji ambao mtu anaweza anza nao.

5. Kutokana na sehemu uliyopo, je gharama ya uendeshaji Hadi mbuzi kumfikisha kiwandani inaweza gharimu shilling ngapi?

Ahsante.
 
Back
Top Bottom