Kama una miaka 40+ na unaye baba mzazi jihesabu ni mwenye bahati.

Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo,mm mzee akikuwa akinikogesha mpaka naanza kuwa na akili ya kujitambua nilikuwa nampenda sana baba, na siku moja aliniambia mwanangu wapende sana wanao kama mimi ninavyokupenda toka umezaliwa,,
Nami nafanya hivyohivyo huwezi amini wanangu wananipenda mpaka mama yao anashangaa,Tuwapende watoto wetu
 
Acheni kukwepa majukumu ya kulea familia zenu,
ugomvi wa mke wako usihamishie kwa wanao,
kinachowacost wababa wengi ni hiyo kaachana na mkewe basi anamsusa na watoto wake, anaenda kuanzisha mji mwingine na mama anabaki kulea watoto peke yake, hata kama mama ndie alikua mkorofi lakini kitendo cha kutohudumia watoto wako hakina 'excuse' lazima ukubwani watoto wakutenge na kukudharau,
Hiyo unayozungumzia ni kama wameachana na bahati mbaya ukute watoto wamebaki kwa mama,lakini kaa ukijua kuwa hata ikitokea wakibaki na baba pia bado huwezi kukuta baba anawalisha chuki dhidi ya mama yao.Kinachoongelewa hapa ni wale walioko kwenye ndoa na hawajatengana bado...
 
Ikiwa una miaka 40+ na baba yako mzazi yupo,mtumie vizuri.

Mama yangu mzazi na mama mdogo yaani mke mdogo wa baba waliniteka kwa kunishawishi na kuniaminisha kuwa baba yangu ni mtu asiyefaa na ni mojawapo wa wanaume walioshindwa kulea ama kutunza familia akiwa kijana.
Niliwaamini nikamtenga baba kwenye matunzo anayistahili kama mzazi.Baba hakuwahi kulalamika wala kuniomba msaada hata wkt akiwa anaitaji msaada.
Mtoto wa kiume nikapata changamoto ya ndoa mama zangu wakachemka.
Sikumshirikisha baba kwakuwa nilikuwa namdharau na kumchukulia kama bwege fulani hivi.
Baadhi ya ndugu wakanishauri nimshirikishe baba.Kiunyonge nikamshirikisha.Ndani ya wiki mbili akawa ametatua changamoto yangu na kuniacha nikiwa nimeduwaa.Migogoro iliyonisumbua kwa miaka zaidi ya mitatu imetatuliwa kwa chini ya wiki mbili kwa kutumia mbinu ambazo sikuwahi hata kuziota na kuniacha nikiwa salama kabisa.
Baba kawa rafiki yangu na sasa ndo nimejua madhambi ya mama zangu waliyoyafanya wakiwa vijana na kupelekea baba kuwaadhibu na kuwatenga.
Ikiwa mkeo anakusumbua ujue kuwa mama yako naye ni mke wa baba yako na alimsumbua ama anaendelea kumsumbja babako.
VIJANA WA KIUME SHIKAMANENI NA BABA ZENU MKITAKA KUJUA VIZURI TABIA ZA WANAWAKE.
SAMAHANI BABA KWA YOTE MABAYA NILIYOKUFANYIA HUKO NYUMA.
Umeongea vema.
 
Back
Top Bottom