Kama una kichekesho chochote tupia hapa

Akili Pesa

JF-Expert Member
Jun 18, 2014
616
854
Mimi naanza Kama ifuatavyo:

Mke:Mme wangu nikifariki utasubiri muda gani hadi
uowe mke mwengine?

Mme:Hadi udongo wa kaburi lako utapo kauka.

Mke:Unaniahidi hivyo??!!

Mme: akatabasamu akasema ndio.
Baada ya kufariki mke,

mme: akawa akiitembelea kaburi ya mkewe kila siku hadi mwaka ukakamilika kaburi ya mkewe bado
udongo ni mbichi hauja kauka!!!
Siku moja mme alipokwenda makaburini
jioni, akamkuta kaka wa mke wake-shemej makaburini akamuuliza:

Mme:Shemeji unafanya nini uku makaburini??

Shemeji:Natekeleza wosia niliopewa na dada yangu
kaniambia kila baada ya siku mbili niwe nauloweka
udongo wa kaburi lake kwa kuumwagia maji ndoo nne mpk sita za maji.
Mume akabaki hana lakusema.

(Hakika vitimbi vyao ni vikubwa wakiwa hai na wakiwa
wamefariki.).
Tupia cha kwako hpa.
 
UMEMUAGA mkeo unaenda kazini, ukapita kwa mchepuko wako, wakati unajimwaya-mwaya na mchepuko, mume wa mchepuko akagonga mlango, ikabidi ufichwe uvunguni mwa kitanda.

Wakati bado upo uvunguni ka mchepuko kakamuaga mume wake kwamba, kanaenda saloon, mume wa ka-mchepuko naye akaona ndo muda wa kuita mchepuko wake, akauita ukaja, wakajimwayamwaya kwa sana muda huo wee bado upo uvunguni. Mara mchepuko wako akarudi kutoka saloon, akagonga mlango, ikabidi mume wa mchepuko wako aufiche uvunguni mchepuko wake.

Kucheki hivi kumbe mchepuko wenyewe ndo mke wako uliyemuaga unaenda kazini, kwa hiyo wewe na mke wako wote mkawa mmefichwa uvunguni...Ukisikia vita ya tatu ya dunia, ndo hii sasa.

Kwa hisani ya Bujibuji...
 
*Doctor*:Habari yako!
*Jamaa*: Salama tu doctor.
*Doctor*: Unaweza ukaniambia unasumbuliwa na nini??
*Jamaa*: Mimi tatizo langu ni kusahau sana aisee!
*Doctor*: Tatizo hilo limekuanza lini??
*Jamaa*: Tatizo gani tena doctor??
 
frank matovu,
Ningemwambia mpe namba yangu ya simu mkeo ntakuwa namletea dawa hukohuko ili usipoteze nauli ya kumleta mpk huku, si unajua vyuma vmekaza
 
Back
Top Bottom