Kama Umeya wa Jiji ni Hivi, Vipi Urais?

Maswala

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
560
225
Wadau, zengwe la umeya ya Jiji la Dar na Urais wa Zanzibar,, sasa unafanya kuhojia matokeo ya kura za urais, ubunge na udiwa uliopita.
1. Kwanza, sioni demokrasia, na kwa mtindo huu CCM mtazidi kuchukiwa sana msipojenga utamaduni wa kuheshimu maoni na wananchi.
2. Kwa mtindo huu, sioni haja ya kuwa na uchaguzi unaogharimu pesa nyingi. CCM tuwaachie wakae vikao vyao na kuamua nani awe kiongozi.
3. Yawezekana kuna madudu mengi endapo UKAWA utachukua Jiji, siri itafichuka.
4. Yawezekana kuna maslahi ya watu binafsi yataharibiwa endapo upinzani utaongoza.

Kwa vyovyote vile, wananchi wanachotaka ni maendeleo yanayowagusa moja kwa moja. Hivyo basi ikiwa mliona vema kuwapa fursa kuamua kwa kura, uamuzi wao uheshimiwe. Vinginevyo, wahusika mjue mnawapa wapinzani wenu haja ya kuwaangusha zaidi hata nje ya Dar.

Ila kwa hali ilivyo, mjue wananchi wamechoshwa na ubabe wa aina hii. Maamuzi ya wananchi yasipoheshimiwa, ipo siku wananchi wakengeuka na kukaidi kuwasikiliza viongozi na hivyo kupelekea machafuko.

Katika kampeini za uchaguzi uliopitan wana CCM wengine walijinadi kuwa tukichagua UKAWA tungekuwa kama Libya, Misri, Tunisia, au Syria. Naamini CCM walijiandaa kufanya hivyo ikiwa zoezi la kufanikisha ushindi wao zingekwama hadi upinzani kushinda, wangeingia msituni.

Mwenyekit wa CCM alidai kuwa hawezi kukabidhi mchi kwa makaratasi, kauli aliyoitumia Museven pia kule Uganda--hizi ni kauli hatari sana kwa hatima ya demokrasia ya kweli. Mh. JPM sasa hivi anaonekana kama mpinzani ndani ya chama tawala.

Kwa nama hii, siwezi kutarajia mema kutoka CCM. Hawa jamaa ni sikio la kufa. Hizi ni dalili za hali ya juu kabisa A uchanga wa siasa za kidemokrasia ndani ya chama tawala. Chama hakina mawazo kuwa siku moja nchii yaweza kuongoza na watu nje ya CCM. Wakto tayari kumwaga damu, kuliko kuheshimu maamuzi ya wananchi. Hii ni hatari.

CCM, fanyeni tafakuri ya juu sana. Miaka mitano inajyo, si mchezi. Mjiandae kukaa kwa mtutu. Kwa sababu naamini wananchi hawatafanya makaosa kama haya. Watahakikisha wanapiga na kulinda kura zao kwa gharama kubwa. Lakini pia wanaCCM waadilifu watapata wakati mgumu, wanaweza kulazimika kuhamia upinzani ili wachagulike.
 
Back
Top Bottom