warumi
R I P
- May 6, 2013
- 16,273
- 18,380
Kumbe uchawi mpaka wajue detail zako, na uchawi hauwezi kufanyika bila kua na hizo detail
Kama haiwezekani kupata detail kwa kutumia uchawi, sasa mbona vijiweni kuna stori mingi kua waganga wanaagua bila wewe kusema chochote wewe hii unaizungumziaje? Kwako mwalim kashasha
It's Scars
Waganga wanatumia details kama nguo za ndan , kucha, nywele, majina kamili na wengine hupiga ramli na kupata info zote za kitu au mtu anayemtaka.
Miaka kadhaa iliyopita niliwahi kwenda Tanga kwa mara ya kwanza kufanya ushirikina, nilienda tu kwa kuwa Rafiki yangu alishaenda pia akafanikiwa mambo yake.
Kutokana na tatizo langu kuwa kubwa kiasi , mganga aliniambia natakiwa kufanya kafara ya mbuzi , Bahati nzuri nilikua na vijisenti, nitatoa kafara , nikafanyiwa visomo pamoja na mambo mengine mengi ya kishirikina
Kwa kweli nilikua Naona mambo ya ajabu kwa kuwa ushirikina nilikua nauona kwenye movie tu .
Basi baada ya kutoka Tanga nikarudi home , ndan Ya siku Tatu tu , haja yangu ile ile niliyoitaka ikaja kwa njia ya ajabu mno, nakumbuka usiku wa ile siku sikulala kabisa , nikawa nawaza kumbe uchawi upo ?
Basi toka miaka hiyo had leo maisha yangu ni ushirikina tu na sijawahi kujuta kwa kweli wala kutapeliwa, labda kwa kuwa mtu aliyenipeleka huko ni mshirikina sana na ameenda sehem nyingi so anajua mganga yupi mzuri.
Ila kitu kimoja ukishaingia kwenye ulimwengu wa giza, roho ya kibinadamu inakutoka, mtu akikuudhi kidogo tu unaweza hat kumdhuru au kumtoa roho kwa ushirikina
Ogopa sana kugombana na watu hovyo, wengine wana nguvu za kiroho , unajikuta unagombana nao, wao wanaenda kukumaliza kwenye ulimwengu wa roho , tena hawakuumizi wala nini, wanakuacha uishi ila kwenye ulimwengu wa roho wameshakuua, hat ufanye nini huwez kufanikiwa.
Sent from my iPhone using JamiiForums