Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

mkuu tunafanana sana:
Mimi mwaka 2010 wakati npo chuo cha cbe dar mzee wangu alikua anaumwa amelazwa muimbili hospital.

Ilikua Mara kwa Mara haipiti wiki lazima nimuote mzee wangu amefariki,basi nlikua nalia sana tena sana ukumbuke nipo ndotoni nikistuka najikuta ninamachozi mengi sana.
Basi nikiamka tu lazima niende hospital kuakikisha je amekufa kwel au laa lkn nlikua namkuta mzima.

siku namaliza tu mitihan ya mwisho ndo siku hiyo hiyo amefariki hakika nililia sana tena sana.

KUHUSU MAONO NDOTONI
Mimi Nina staili mbili za kuota nikiwa nimelala.
Huwa naota kwa kuona tukio kamili lkn pia huwa naota kwa kusikia sauti ya mtu masikioni mwangu akiniambia kitu.
Kuna siku niliota sauti ya mtu ikiwa IPO siriazi inaniambia kwa umakini kabisa kua utaenda kua manager katika kampuni hii theni nikaanza kuoneshwa laivu mazingira ya hiyo kampuni.
Nilivostuka niliomba mungu iyo ndoto na iwe kwel maana nilikua kweli sina kazi ya kuajiriwa naendesha bodaboda yangu.
Ikapita kama miezi mitatu mbaka nishaanza kusahau hiyo ndoto siku moja natoka kwenye interview ya kampuni flani dar wakat nipo chalinze baba yangu mdogo akanipigia simu akaniambia upo tayar kuajiriwa nikamwambia ndio mzee akaniambia nitumie CV yako kuna MTU nimtumie

Nlivotuma baada ya wiki nikaitwa kusailiwa nikaambiwa wiki ijayo niende kuanza kazi tanga.
Huwezi amini nilivofika mazingira ya pale kwenye ile kampuni ndo yaleyale ambayo niliyoyaota nankuoneshwa kwenye ndoto ambayo ilitokea zaidi ya miezi mitatu nyuma

Nilishangaa sana kwa kwel.na mengine mengi tu sitaki kuwachosha na wengine wachangie

Sent using Jamii Forums mobile app
ungekua umeokoka ungeweza kuifuta hiyo ndoto mzee wako asingefariki


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kisa kingine cha Kaka yangu mtoto wa Mama yangu mdogo.

Yeye kipindi hicho alikuwa amemaliza chuo akarudi Kijijini nyumbani kwao.
Huko akawa na mahusiano na binti fulani,baada ya muda alipata kazi akaja huku mjini..Mambo yakakaa sawa akataka kumuacha yule mwanamke, yaani alirogwa mdomo ulipinda .. Sasa Kuna siku alikuja nyumbani kwetu(kwa mamkubwa wake) kusalimia nikawa namshangaa mdomo upo pembeni kabisa ila haumwi chochote.
Kumuuliza mama ndiyo akanihadithia kwamba huko kwao familia ya binti ilimroga.

Ilibidi aendelee na yule mwanamke,baadaye akamuoa..tukafunga safari Hadi huko Kijijini tukacheza harusi.
Akamchukua mkewe wakaenda kuishi mjini.Yule dada alikuwa mrembo jamani huwezi amini Kama ni mchawi.
Mkewe akapata ujauzito,wanaendelea kuishi na mimba ilikuwa kubwa tu Kama miez 6-7.

Kumbe usiku wakilala yule dada alikuwa anaondoka kimazingara anaenda anakoenda asubuhi anarudi.
Wachawi wao kanuni yao akiondoka usiku ,mwili unabaki pale kitandani na inabidi usimuamshe.
Sasa yule Kaka alistuka usiku akamstua akaona mtu hatikisiki.
Yule dada aliondoka akaenda Kwenye anga ya sumbawanga huko na mama yake ,wameenda kuwanga huko wakazidiwa nguvu.(haya yalikuwa maelezo ya mama ya huyo dada)..huku Kaka alivyozidi kumuamsha ndipo alipoharibu Mambo.
Amsha dada haamki,kuita majirani amsha mtu haamki,kumpeleka hospital kumpima amekufa yeye na mtoto tumboni.

Mama wa huyu dada msibani alilia Sana,akaanza kumlaumu huyu Kaka kwanini alimuamsha mwanawe,alivyoona Mara ya kwanza hajatikisika angemuacha na asingeita watu.
Yule dada akawa amekufa hivyo,mtoto akatolewa tumboni ..wakazika.
Huyo binti ndiye alikuwa anaenda naye safari zake zote.

Baadaye mama mtu anamwambia yule Kaka kwamba ampe binti yake mwingine aliyebakia..
Huyo Kaka aligoma kabisa.
Hicho Kijiji hakijaendelea bado.. yaani Kuna wachawi hatari.

Sent using Jamii Forums mobile app
kabila gani hao??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa kipindi Niko shule,ndoto za kifo zikawa zinanijia Ila Mara napotezea...
Sometimes nikikaa mawazo yananijia kwamba uliota ndoto hii..nikawa sitilii maanani ukizingatia kipindi hicho bado umri mdogo na nilikuwa sijakomaa Sana kiimani.

Nikawa Tena napata mawazo ya nguo, yaani Kama ndoto inanijia dadangu ameshona nguo yake halafu ikapotea(Dada yangu alikuwa fundi cherehani)

Nimerudi likizo mwezi June nikaambiwa dada kihoma kinamsumbua.
Nikafunga safari kwenda kwake kumsalimia...hakuwa serious Sana yaani ilikuwa homa ya kawaida tu alienda hospital wakampima wakakuta ana typhoid,wakampa dozi ya typhoid.
Bado aliendelea kuugua ,akaenda hospital nyingine akapimwa akaambiwa vidonda vya tumbo.
Huo Ni mwezi June.
Hali ikazidi kuendelea..

Yale mawazo yakawa yananijia Tena lakini masikini sijui Ni kutokutambua au utoto,nikawa siyatilii maanani.

Mwezi huo huo akapelekwa Tena hsp akakutwa na tatizo la figo,japo alikuwa fiti tu,hajawahi kuugua ugonjwa wa Figo nyuma,familia hazina historia za magonjwa hayo,kwamba ana HIV hakuna..ilikuja tu from no where.

Tukawa tumeanza maombi,
Binafsi nikaanza maombi kwa ajili yake.
Shida ikawa upande wa mume,wakampeleka kwa waganga wa kienyeji..wakawa wanaambiwa maneno mengi,mwingine anasema Mara fulani alikuroga ,mwingine fulani (dereva)amekuroga,,Huyo dereva alikuwa dereva wa gari la familia la biashara,baada ya kuona anaingiza loss sana akapokonywa gari na likaenda kupakiwa pale nyumbani kwa dada maana Yeye ndiye alikuwa msimamizi wa hayo mapato.
Alipogundulika na Hilo tatizo alianzishiwa tiba ya hosp.

July Mimi nikarudi shule nikimuacha Dada yangu anaendelea vizuri,shida ikawa hiyo michanganyo..Mara waganga,Mara maombi na hosp.

Kuna mtumishi aliongea naye akamuombea akafunuliwa hayo ya nguo.
Kipande Cha nguo kilichukuliwa kikaenda kufanyiwa Mambo huko na kikazikwa.

Nilijitahidi weekend moja kuomba ruhusa na kurudi kumuona dada ..ilikuwa October..nikakuta Hali yake SI nzuri.

Baadaye naye alichoka Yale madawa ya kienyeji ..nilirudi hiyo siku nilikuta wametoka hsp kufanyiwa dialysis.. Hali yake ikazidi kuwa mbaya..
Alinambia mdogo wangu nashindwa kula,nashindwa kuongea vizuri,nashindwa kutembelea,niombee

Niliomba Sana,nilirudi shule ratiba yangu ilijikita Kwenye kumuombea dada...
Walikuja watumishi wanaojiita manabii akaomba kupelekwa.
Kweli nabii alimpitia akamwambia una shida ya Figo, akamwambia ndiyo..akamtazama baadaye akaondoka.
Mara wakawa wanasema kuonana naye Hadi utoe hela laki 3 ..hizo taarifa nilizipata baada ya kuwapigia simu kuongea nao.

Tuliendelea kuomba,,nilipata Tena muda nikarudi nyumbani,aliniomba nimuombee..nikamuombea.

Wiki hiyo alizidiwa akarudishwa hsp,akawa anapumulia machine,siku tatu mfululizo..ya nne akapata nafuu,wanaenda kumuona yaani Hadi anaongea vizuri.
Hiyo wiki nipo Kwenye mfungo..
Asubuhi nimeamka Mara bega likawa linanicheza Sana.
Nikakaa nikatulia Sana mawazo yakawa yananijia kwamba nyumbani Hali SI nzuri Kama Kuna tatizo.

Mchana matron alipigiwa simu na shemeji kumpa taarifa za kifo Cha dada yangu(shemeji yangu mume wa dada yangu mwingine(Sio Huyo mgonjwa ) alikuwa mwalimu pale shule ninayosoma.

Matron akamtafuta rafiki yangu, akamwambia anirudishe nyumbani bila Mimi kujua chochote, wakapanga mpango hapo..rafiki akaja akasema matron ameniruhusu nikamuomba tutoke wote..kweli? Namuuliza ananijibu ndiyo..kwenda kumuuliza matron akakubali,sikustuka kwa sababu matron alikuwa ananiruhusu Mara nyingi kwenda home.
Yule rafiki akasema twende kwanza kwenu tukawasalimie halafu tupike na chakula Cha kurudi nacho shule.

Tumefika mitaa ya home nashangaa jirani ananiambia msiende hivyo,njoo mchukue vitenge mvae..nikajua hapa tayari.
Nikawa najiuliza,nimalizie mfungo au nikate tu muda huo ,ninayemuombea amekufa asubuhi



USHAURI WANGU
Ukiamua kusimama upande wa Mungu,Basi simamia huko.
Changamoto huja pale wengine wanaamini Hiki,wengine kile,
Hamuwezi kufikia mafanikio.

Usipuuze mawazo yanayokujia.
Mara nyingi Mungu anasema na sisi kwa njia ya mawazo na ndoto lakini tumekuwa tukipuuzia.
Ile sauti unayoisikia akilini jifunze kuisikiliza.

Jifunze kuombea ndoto.
Ndoto nyingine huwa zinatokea kweli.
Mimi niliota na nikaipuuza licha ya kukumbushwa Mara nyingi.

mahondaw
Yna aika
Heaven Sent
Sent using Jamii Forums mobile app
hiyo nguo yake kupotea inamaanisha nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baba yangu alishawahi mwadhibu mwanafunzi kwa fimbo..yule mtoto hakufanya kazi(homework)

Alivyorudi kwao akaenda kumsemea kwa babu yake.
Babu yake aliwahi asubuhi akamwambia mwalimu utanitambua.
Mara ghafla baba mkono ulivimba.
Akaenda hospital wapi hakuna kitu..
Ulivimba ulijaa maji.

Alikuwa halali usiku kwa maumivu.
Aliombewa Sana (familia yangu ilikuwa wale wanaosali uamsho wa wakristo tz UWATA)
Baadaye baada ya maombi akarudishwa Tena hospital akatibiwa akapona.


Mama yangu pia alishawahi kuugua..baada ya maombi yule aliyemroga akaanza kuropoka maneno.
Alimroga alikuwa anataka ndoa ivunjike amuue mama ili aolewe Yeye
Sent using Jamii Forums mobile app
[/QUOTE]
 
Kwa simulizi hizi, hakika Watanzania tupo vizuri sana upande wa pili wa shilingi. Hakika Uchawi upo, lakini Serikali haiamini Uchawi! Ifike mahali serikali yetu ibadili mtazamo juu ya hili.
Aliyekuambia Serikali haiamini uchawi ni nani, ni watu hujisemea hivyo tu. Tanzania tuna Sheria ya mambo ya uchawi, sasa jiulize serikali inaweza kutungia sheria jambo ambalo hailiamini??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu tunafanana sana:
Mimi mwaka 2010 wakati npo chuo cha cbe dar mzee wangu alikua anaumwa amelazwa muimbili hospital.

Ilikua Mara kwa Mara haipiti wiki lazima nimuote mzee wangu amefariki,basi nlikua nalia sana tena sana ukumbuke nipo ndotoni nikistuka najikuta ninamachozi mengi sana.
Basi nikiamka tu lazima niende hospital kuakikisha je amekufa kwel au laa lkn nlikua namkuta mzima.

siku namaliza tu mitihan ya mwisho ndo siku hiyo hiyo amefariki hakika nililia sana tena sana.

KUHUSU MAONO NDOTONI
Mimi Nina staili mbili za kuota nikiwa nimelala.
Huwa naota kwa kuona tukio kamili lkn pia huwa naota kwa kusikia sauti ya mtu masikioni mwangu akiniambia kitu.
Kuna siku niliota sauti ya mtu ikiwa IPO siriazi inaniambia kwa umakini kabisa kua utaenda kua manager katika kampuni hii theni nikaanza kuoneshwa laivu mazingira ya hiyo kampuni.
Nilivostuka niliomba mungu iyo ndoto na iwe kwel maana nilikua kweli sina kazi ya kuajiriwa naendesha bodaboda yangu.
Ikapita kama miezi mitatu mbaka nishaanza kusahau hiyo ndoto siku moja natoka kwenye interview ya kampuni flani dar wakat nipo chalinze baba yangu mdogo akanipigia simu akaniambia upo tayar kuajiriwa nikamwambia ndio mzee akaniambia nitumie CV yako kuna MTU nimtumie

Nlivotuma baada ya wiki nikaitwa kusailiwa nikaambiwa wiki ijayo niende kuanza kazi tanga.
Huwezi amini nilivofika mazingira ya pale kwenye ile kampuni ndo yaleyale ambayo niliyoyaota nankuoneshwa kwenye ndoto ambayo ilitokea zaidi ya miezi mitatu nyuma

Nilishangaa sana kwa kwel.na mengine mengi tu sitaki kuwachosha na wengine wachangie

Sent using Jamii Forums mobile app
Una maono makubwa sana
Fanyia kazi utafika mbali sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau naomba tujuzane

Mbali ña watu wa kigoma kuwà watafutaji, na wapambanaji sana linapokuja suala la biashara, huwa najiuliza kuna siri gani ya ziada imejificha?

Muha akifungua biashara yoyote sehemu ambayo biashara ni ngumu kwa wengine kupata wateja, yeye (au wao waha) atajaza sana na kuuza sana huku wengine wakiyumba!

Wenzetu hawa ni wagum sana kueleza siri ya mafanikio zaidi ya kusema kauli.

Watàalam tunaomba ufafanuzi hasa wa kina tufaham ni siri gani hasa inatumika!

Nina mfano hai hapa, kuna duka la msukuma mmoja na muha mmoja yote yametazamana.
Lakini cha ajabu msukuma kapotea hauzi tena kama zamani, muha anauza sana na mpaka akifunga wateja wanamsubiri huku duka la msukuma likiwa wazi tu!!!!


Karibuni tujadili

Sent using Jamii Forums mobile app
Angalia bei ya vitu, muda anaofungua na kufunga, hakuna kitu kinauzi kama uende duka fulani ukute limefungwa bora nitembee kilomita mbili kufuata huduma ya uhakika kuliko mita50,ambayo unaweza kuta kafunga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wabongo kwa visingizio...halaf ukienda hapo golini kwake fulu ngendembwe na kaulimbovu kwa wateja hlf utegemee kupata wateja
Wadau naomba tujuzane

Mbali ña watu wa kigoma kuwà watafutaji, na wapambanaji sana linapokuja suala la biashara, huwa najiuliza kuna siri gani ya ziada imejificha?

Muha akifungua biashara yoyote sehemu ambayo biashara ni ngumu kwa wengine kupata wateja, yeye (au wao waha) atajaza sana na kuuza sana huku wengine wakiyumba!

Wenzetu hawa ni wagum sana kueleza siri ya mafanikio zaidi ya kusema kauli.

Watàalam tunaomba ufafanuzi hasa wa kina tufaham ni siri gani hasa inatumika!

Nina mfano hai hapa, kuna duka la msukuma mmoja na muha mmoja yote yametazamana.
Lakini cha ajabu msukuma kapotea hauzi tena kama zamani, muha anauza sana na mpaka akifunga wateja wanamsubiri huku duka la msukuma likiwa wazi tu!!!!


Karibuni tujadili

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilikuwa naamini uchawi upo lakini nilikuwa naona kama haunihusu yaani hayo mambo sio kwa ajili yangu ,ila in 2012 wakti ni watoto wawili chini ya miaka mi 4 wote haka kakubwa she was 3yrs kalikuwa kananambia baba mtu ,sisi hatumuoni kwa wakati huo tulikuwa tumebaki mimi ,shemeji wa kike ,na watt wangu wawili ,wife alikuwa china kibiashara ,..alikuwa akirudia mara kwa mara nilikuwa nachukulia masihara ila baadae niliyokutana nayo hii dunia ndani yake kuna dunia nyingine yaani nimeishi maisha ya ajbu sana 2018, 2019 ni story ndefu from 2012 uhalisia ukaja dhihiri 2018 tayari mtt ameshakuwa yaani tumepitia vitu vya ajabu sana,tumeona mambo ambayo tulikuwa tukiyasikia tu ila Alhamdulillah M/mungu mkubwa sana tumepiga hatua kubwa Alhamdulillah
Wakuu habari zenu, ni matumaini yangu kuwa hamjambo.

Leo nataka kuweka ushuhuda wangu kwa niliyoyashuhudia live juu ya nguvu za giza, kwa wasioamini nadhani uzi huu hautakuwa na thamani kwao, kama na wewe unao ushuhuda usisahau kushea nasi.

1. Ushuhuda wangu unaanzia mwaka 1992 nikiwa nafundisha shule X wilaya ya Sengerema, kuna mwalimu nilikuwa nafundisha naye kituo kimoja.

Siku hiyo kuna kamvua kalinyesha sana, baada ya kupungua mwalimu mwenzangu alimuagiza mtoto wake wa kiume aliyekuwa akisoma darasa la kwanza kwenda kuchuma maharage shambani.

Bahati mbaya mtoto akiwa shambani aligongwa/aliumwa na nyoka na kupeleka kifo, tulifanya taratibu za mazishi na kumsitiri mtoto huyo.

Cha kushangaza mwaka 2008 mtoto huyo alionekana akiwa uchi na nywele ndefu sana alikuja moja kwa moja nyumbani na kupitiliza ndani nyumbani kwao, alikuwa ameshakuwa baba mzima, nywele zilikuwa ndefu sana pamoja na mikono iliyofikia usawa wa magoti.

Watu walistaajabu sana lakini hakudumu sana alifariki baada ya kukaa uraiani kwa wiki mbili.

2. Ushuhuda wangu bado unabaki huko huko Sengerema katika kijiji cha Bubandwamhela.

Nikiwa nafundisha shule X, kuna binti kijijini aliyekuwa akisoma darasa la saba aliugua ghafla baada ya kutoka shuleni.

Wazazi wake walipompeleka hospitali daktari aliwaambia mtoto hana ugonjwa, wazazi waliamua kujiongeza na kumpeleka kwa mganga wa jadi.

Cha kushangaza kesho yake shangazi ya binti alikutwa kwa mganga akiwa uchi, huku akiweweseka na akili zimemruka, shangazi mtu alikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi lakini kwa kuwa serikali haiamini ushirikina aliachiwa huru, lakini hadi leo hii alishakuwa chizi. Binti yeye alipona kabisa.

3. Kisa cha tatu na mwisho ni hiki kilichotokea Liwale shule ya sekondari X nikiwa na walimu wenzangu ambao tulikuwa tunasoma chuo cha SAUT-Mtwara.

Tulipangiwa field katika wilaya ya Liwale ilikuwa mwaka 2009, mwanachuo mwenzetu akiwa zamu siku hiyo alikumbana na mtoto ambaye kwao iliaminika kuwa bibi yake alikuwa mtaalamu wa mambo ya giza.

Mwanafunzi huyo alichelewa kufika shule, mwalimu alipotaka kumuadhibu aligoma, wakasumbuana sana mwisho wa siku akamuadhibu yakaisha, jioni tukiwa uwanjani tunafanya mazoezi yule mwanachuo mwenzangu alianguka na kupoteza fahamu, ikawa jumla hadi kifo.

Kama na wewe umewahi kukutana/kushuhudia live ushirikina share nasi kisa chako watu tupate ilimu.

Mungu ni mwema siku zote.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom