Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kiranga wewe kusema uchawi haupo that is upon you, not all of us.

Binafsi nimeishi Korogwe Vijijini huko kuelekea Mashewa.

Nimezishuhudia matendo ya Kichawi kama Zongo. Maziwa Fresh kugandishwa within a minute tu yalipotoka kukamuliwa.

Nimeshuhudia mwenyewe shule moja ya msingi, mida ya saa 1 jioni madawati yakiwa yanapigizwa pigizwa huku ndani haonekani kiumbe yoyote.

All in all mikoa ya Kigoma, Rukwa, Tanga, Shinyanga na Mwanza ndio inaongoza kwa imani za kishirikina.

Kiranga naomba uelewe hizi ni 'imani' zinazoaminika na baadhi ya watu...
Wasioamini ni kwamba 'hayajawakuta'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nishawahi sikia kisa kinschohusishwa na uchawi

Kuna masela wawili walienda kwa mganga ili wapate utajiri

Mganga akawapa dawa akawaambia wakaoge usiku makaburini na wakitoka mlangoni kwa mganga hawatakiwi kugeuka nyuma

Basi unaambiwa safari yao iliandamwa na misukosuko yakutisha, mara wasikie muungurumo wa simba akiwa nyuma yao na vimbwenga vingi lakini walijitahidi kukaza ili kutovunja sharti la kugeuka nyuma

Sasa ulipofika usiku majira ya saa 8 ikabidi waende makaburini kuoga ili kumalizia zoezi lao la mwisho ili wawe mamilionea

Walipofika makaburini wakavua nguo wote nakubakia uchi kisha wakapanda juu ya kaburi ili waoge

si unajua ukiwa katika ile mood flani hivi unaoga halafu umefumba na macho ili maji yasiingie machoni.

wakastukia tu paap! wameshikwa makalio kwa nyuma.

Aaah unaambiwa wote ilibidi wageuke nyuma kwa haraka huku wanakimbia na kupiga makelele

Kesho yake kijiweni wakaanza kulaumiana "aaah wewe ndiye ulizingua, we ungekausha bila kupiga mikelele mi nisingechochora kwani kushikwa tako kitu gani bwana" yani leo nisingekua nakunywa kahawa hapa ningekua nimejikoki huko kwenye hotel zinazotambulika na dunia"
Mwana umetisha sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Orbit si topic ya thread. Na mimi sijataja orbit.

Uchawi ni topic ya thread. Na wewe umetaja uchawi.

Umetaja uchawi bila kujua uchawi ni nini?

Uchawi ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Siwezi kuelezea uchawi ni ilhali sijawahi kuloga wala kujifunzabkuloga. Nachojua uchawi upo (ni kama tunavyoamini kuwa kuna upepo ilhali hakuna aliyewahi kuuona zaidi ya kuona effects zake. Vivyohivyo na uchawi ndivyo ulivyo)
 
Effects za uchawi ni zipi, na unajuaje hizi ni effects za uchawi tu, si kitu kingine chochote, ikiwa hata kuu define uchawi huwezi?
 
Effects za uchawi ni zipi, na unajuaje hizi ni effects za uchawi tu, si kitu kingine chochote, ikiwa hata kuu define uchawi huwezi?
Walawi 19: 28
“Msile nyama yoyote yenye damu. Msipige bao wala kufanya uchawi.

Nitatokomeza matendo yenu ya uchawi, nanyi hamtakuwa tena na wapiga ramli.
Mika 5:12

Wachawi wa Misri, kwa uchawi wao, wakajaribu kuyageuza mavumbi yawe viroboto, lakini hawakufaulu. Viroboto hao wakaenea juu ya watu na wanyama.
Kutoka 8:18

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nishawahi sikia kisa kinschohusishwa na uchawi

Kuna masela wawili walienda kwa mganga ili wapate utajiri

Mganga akawapa dawa akawaambia wakaoge usiku makaburini na wakitoka mlangoni kwa mganga hawatakiwi kugeuka nyuma

Basi unaambiwa safari yao iliandamwa na misukosuko yakutisha, mara wasikie muungurumo wa simba akiwa nyuma yao na vimbwenga vingi lakini walijitahidi kukaza ili kutovunja sharti la kugeuka nyuma

Sasa ulipofika usiku majira ya saa 8 ikabidi waende makaburini kuoga ili kumalizia zoezi lao la mwisho ili wawe mamilionea

Walipofika makaburini wakavua nguo wote nakubakia uchi kisha wakapanda juu ya kaburi ili waoge

si unajua ukiwa katika ile mood flani hivi unaoga halafu umefumba na macho ili maji yasiingie machoni.

wakastukia tu paap! wameshikwa makalio kwa nyuma.

Aaah unaambiwa wote ilibidi wageuke nyuma kwa haraka huku wanakimbia na kupiga makelele

Kesho yake kijiweni wakaanza kulaumiana "aaah wewe ndiye ulizingua, we ungekausha bila kupiga mikelele mi nisingechochora kwani kushikwa tako kitu gani bwana" yani leo nisingekua nakunywa kahawa hapa ningekua nimejikoki huko kwenye hotel zinazotambulika na dunia"
Duuh hii balaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikulazimishi ukubali ila nikwambia jambo moja tu ndugu, kwenye maji kuna vimbwanga hujawahi kufikiriaa. Hii alinihadithia mama yangu kipindi wanakwenda Bukoba miaka ya themanini ambapo meli ya Mv Bukoba ilikuwa ikifanya safari zake mchana.

Kuna pahali walifika wakawaona watu kila mtu na shughuli zake, wengine wakawa wanacheza tenis mixer tenis inagonga mpaka meli, wengine wanashughuli nyingine.
Kuhusu mauza uza ya ziwa Victoria naelewa mkuu, kwenye maji kuona mtu amekaa juu ya maji ananyonyesha ama anapeta Mchele ni Jambo la kawaida, but nilichokataa Mimi ni hiyo story yako maana hata Mimi nilishaisikia hivo hivo kama wewe but ilikua Katika context tofauti na yako kitu kinachonifanya nione ni story ya kutungwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa alitoka Jijini DSM, kwenda kusalimia kwao kijiji x, alipofika akaona aingie mahali apunguze uchovu kwa kupiga pombe ya kienyeji ya kwao huko,basi kulikua kuna wazee pembeni wamekaa na wao wanakula ugimbi, akawasalimia freshi akaagiza na yeye chupa yake, kati ya wale wazee akamwita kijana kwa jina lake maana ni kijana aliekulia kijiji hichohicho akamwomba awanunulie na wao angalau chupa mojamoja, si unajua ukitoka Town,kijiji kinaamini unahela. Dogo akaona wasimzengue yani yeye hajafika hata home kuwatoa wazazi wale wazee wanataka kumtoa upepo mapema, jamaa akawajibu hana kitu,mzee akamuuliza kweli mwanangu then kila mtu akaendelea na hamsini zake, dogo kueka chupa mdomoni hamna pombe akajua labda alijichanganya atakua alishamaliza, akaita chupa ya pili nayo akionja kidogo, akinywa mara ya pili mzigo empty haha haha.. Ilibidi awahi home bila Kuaga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom